Marehemu wengi hurejea baadhi ya sehemu walizofia?

Marehemu wengi hurejea baadhi ya sehemu walizofia?

Marehemu hawarudi ila mtu anapokufa roho take inabanduka toka mwilini baada ya siku tatu. Pia anaweza kuwepo duniani siku chache kabla ya kuondoka.
Ghost anayekuja mahali alipokufa ni etheric body hasa mtu akifa kifo cha ajali, kifo cha maumivu makali.
Etheric body kama hiyo inaweza kudumu miaka 50 au 100.
Lakini etheric body siyo roho. No mindless ghost.
In fact mtu akifa, physical body na astral body vyote vinakufa.
Ile roho iliyomo ndani ya astral body ndio inakwenda kuishi ahera.
Mwili wa binadamu ni roho moja ndani ya roho nyingine.
Jumla ziko roho tisa.
Alooo

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
nahis babu yangu na bibi yangu kipenz na wajomba zangu huwa wanakuja mana tulipendana sana
 
Duh ni kweli mkuu. Hata mm nilikuwa nafanya kazi na dada mmoja alietokea kunipenda sana. Kuna kipindi nikaenda masomoni kwa muda wa miaka miwili. Niliporudi kazini dada yule kama kawaida yake alikuwa akipenda kuniita tupige story wateja wakipungua, lakini sasa story zake zikawa zimebadilika. Alikuwa akinionya kuwa mdogo wangu umerudi kutoka masomoni ila ukae vizuri na watu humu ndani maana kuna watu wabaya sana na usingenikuta maana walijaribu hata kuniua. Basi akawa anarudia kila mara kuniambia hivi japo hakuwa ananitajia hao watu na mm sikuwa nauliza. Ilienda mpaka na mm nikaanza kuingiwa hofu na wakati mwengine nikawa namkwepa nikihisi labda ameanza kuchanganyikiwa.
Basi kuna siku akaniita na siku hiyo akanitajia majina ya hao watu ambao ni wafanyakazi wenzetu. Ndani ya wiki hiyo baada ya kunitajia dada yule alifariki ghafla. Sasa nikawa kila ninapoenda nakutana na mtu kama yeye, wakati mwengine anakuwa yupo mbele yangu ninapokuwa natembea, mara nyengine kwenye daladala. Nikawa najiuliza ni nini anachokitaka kwangu? Hali hii iliendelea mpaka nilipoamua kuwasimulia watu hii story na kuwataja hao watu alionitajia ndio sasa nikaacha kumuona.
Huenda alitaka watu wajue tu kilichomtokea. Very spooky but real!

Mkuu dunia duara, na Mungu ana siri kubwa sana ktk vifo vya wanadamu, hata mimi huyu ndugu yangu anaenitokea mara kwa mara, kuna kazi yetu ilikuwa haijakamilika, anafanya kunitokea kama ukumbusho wa mimi kukamilisha katika njia iliyo sahihi!
 
Poor IQ, dunia inakimbia kwa kasi wewe bado umesimama, ni lazima uachwe mbali sana.
hahaha mwingine huyuu anaamini kitu asichoweza ku kiprove eti anaenda na kasi ya dunia we ni m. p. umbavu sana hahaha
 
hili halina ukweli wowote kwa mwenye imani ya kiroho!! vitu viwili tu vinaweza kuona mfano wa mtu aliyekufa 1. ni muingiliano wa kimawazo hadi inafika hatua ya kujenga picha kamili either ukiwa umelala(ndoto) au ukiwa macho, na la pili ni kutawaliwa na majini au mashetani ambayo hujigeuza umbile la marehemu!! ila marehemu harudi
 
Tunatofautiana viwango vya ufahamu na elimu na uzoefu
 
Mshanajr kila mara unanigusa, tarehe 30/12/2016 tulimzika mama yetu mzazi, baada ya kumaliza kila kitu nilirudi nyumbani kwangu, siku niliyofika nikiwa kitandani niko macho sijalala usinginzi, nilipitiwa na kitu kilichonizamisha usingizini nikasikia sauti ya mama inaniuliza 'umeniuguza sana si kazi watakufukuza?' nikajibu hapana nilikuwa naomba ruhusa, akauliza tena 'je nyumba umeikuta salama' nikajibu nimeikuta salama. Ile nashangaa hivi naongea na mama, nikarudi kwenye hali ya kawaida;
 
Ila bwana Mshana Jr vip na wale wanafalisafa wa zamani walioamini kuwa mtu akifa roho yake inahamia kwa binadamu mwingine anayetarajiwa kuja hasa mtoto aliyeko tumboni.
Mimi nahisi hii ni kweli kwasababu ni kama nguo zako zinapochakaa nakununua zingine mpya.
Hata wewe siajabu umeshazikwa sana tu
 
Mmh mpaka nimesisimka! Pole mno kwa kuondokewa na mzazi ulimuuguza kwa upendo amerudi kukushukuru
 
Ila bwana Mshana Jr vip na wale wanafalisafa wa zamani walioamini kuwa mtu akifa roho yake inahamia kwa binadamu mwingine anayetarajiwa kuja hasa mtoto aliyeko tumboni.
Mimi nahisi hii ni kweli kwasababu ni kama nguo zako zinapochakaa nakununua zingine mpya.
Hata wewe siajabu umeshazikwa sana tu
Hiyo ni dhana ya reincarnation ambayo nayo ipo na kuna baadhi ya watu wanaamini inafanya kazi kabisa
 
Back
Top Bottom