Harufu ya pesa inatufata tulipo yani automatically tu wala hamna nguvu!
Na ukisikia harufu ya pesa ya bure mahali hata kama ni wewe hutaenda?
[emoji3] [emoji3] [emoji115]Umetisha, kwahiyo upepo wa pesa mnaujuwa?
Mimi kwa mbali naanza kuamini pesa ni sehemu ya ufalme wa shetani na mama zetu ni branch of satan.
Sisi waislam tunaomba dua na kumchomea ubani,hapo inamaanisha umemsahau,mm Dada yangu hunijia amenuna halafu ananitizama anakaa kwenye angle nikichoma ubani haji anafurahi,wanasema ubani ni chakula cha wafu.Nna dada yangu alifariki nikiwa shule na kwa bahati mbaya sikuweza kuhudhuria msiba wake. Niliporudi nyumbani kuna siku nikamuota, alikuja huku akiwa na furaha na aliponiona alitaka kunikumbatia. Mimi nikamkwepa nikamwambia wewe mbona ulishakufa kitambo sasa umefuata nini huku? Alinijibu hivi ,'ni kweli nimekufa ila huko niliko nakukumbuka sana ndo maana nimekuja kukusalimia'. Akaendelea kusema, kama unaniogopa basi ntajiziba usoni na kanga then nipe mkono tusalimiane. Kweli akajiziba usoni na kanga nikampa mkono tukasalimiana then akapotea nikastuka usingizini. Ukapita kama mwaka hivi akaja tena, akaniambia maneno yaleyale kuwa huko aliko ananikumbuka sana ndo maana huja kunisalimu na akaniambia kila nikija ntakua najifunika usoni tunasalimiana kwa kupeana mikono then anaondoka. Kweli tulipeana mikono then akaondoka nikastuka usingizini. Nilimsimulia hii kitu mama angu, alikasirika sana akasema akuache kabisa asikufatefate na kweli hajaja tena kwa style ile ila huwa namuota endapo kuna jambo muhimu sana nimemfanyia mmoja wa ndugu zake ndo huja kama kutoa shukrani. Hii hali inanitisha mno
Mara nyingi hutokea ndotoniHawaji moja kwa moja, huwaoni moja kwa moja kwakuwa wao si mwili tena wao ni roho...utahisi tu hali tofauti utahisi uwepo wake harufu yake ama hata kumuona sura isiyo kamili
Mim kwa ulewa wangu kwa asilimia 99 utakacho ona ndotoni bas jiandae na kinyume chake kukipata duniani,mfano ukiota harus basi ukiamka jiandae na msiba au janga zito,ukiota unashika mavi jiandae kushika pesa ,mara nyingi kinyume chake ,ila kuna zingine zinaenda mbali zaidi mfano ukiota unakula manannas bas ujue unapata mpenz mpya au kuna jambo lako ulikua unalifatilia sasa linaenda kukubalika,yaan ulimwengu wa ndoto yaan balza unakua na msg nying mno tusipuuze sana tuulize na tupate majibu sahihi.....ilo la kukabidhiwa pesa jiangalie ndani ya mwez mmoja unaweza pata jambo usilolipenda ila ukifanya ibada sana Mungu akaondoa kikombe kilicho mbele yako na kukupa jema zaidi.Mkuu Mshana Jr Mimi niliota baba mzazi marehemu akinipa pesa nyingi sana ndotoni, hii inamaanisha nini.
Dua ni jambo la msingi sana sana ,kwa mfano Mungu ktk maandiko amesema siku ya kihama watu watakao pata kivulichake jua litakaposhuka ni mtoto atakae kua anawaombea dua wazazi wake wapate pumziko jema, sasa pia wanasema alikufa ajapotea kwani ata sisi tunaelekea uko yaweza kua leo au ata baada ya dakika moja kutoka sasa ,hivyo tujue dhumuni letu la kuwepo dunian na nin tunaoaswa kufanya na nani katuleta na kwa dhumun lipi na kisha tufanye kama alietuleta anavyotaka bas tutakua ni bora sana....Sisi waislam tunaomba dua na kumchomea ubani,hapo inamaanisha umemsahau,mm Dada yangu hunijia amenuna halafu ananitizama anakaa kwenye angle nikichoma ubani haji anafurahi,wanasema ubani ni chakula cha wafu.
Kumbe uliota???Mimi kuna mtu alikufa akiwa mbali hatukuonana kama mwaka kabla hajafa
baada ya mazishi nilimuota kaja kwangu kuniaga...na kwangu alikuwa hapajui
Mtu yupo usingizini anaota atapigaje picha??Ungekuwa na kamera karibu ungepiga hata picha?
Bado hujaanzisha kanisa mkuu? Maono hayo tayari, ungeendelea kidogo ungeanza kunena kwa lughaNimekusoma vema, ila hata Mimi nikiwa mdogo kati ya miaka 8-10 kuna vitu vilikuwa vinatokea nikiota usiku jambo kesho lzm litokee, mfano wakati mmoja tulimwangiza baba flani atuletee viatu nje ya nchi,akaa kama wiki2. usiku nimeota nimeletewa viatu, kweli asubuhi yake nililetewa viatu. wakati mwingine tena nilikuwa nimelala katika mkeka usiku nikaota nampiga nyoka fimbo na kumuua. kulipo kucha asubuhi kweli nilimkuta nyoka pembeni yangu katika mkeka amekufa, Sikujua alifikaje pale
Duh ni kweli mkuu. Hata mm nilikuwa nafanya kazi na dada mmoja alietokea kunipenda sana. Kuna kipindi nikaenda masomoni kwa muda wa miaka miwili. Niliporudi kazini dada yule kama kawaida yake alikuwa akipenda kuniita tupige story wateja wakipungua, lakini sasa story zake zikawa zimebadilika. Alikuwa akinionya kuwa mdogo wangu umerudi kutoka masomoni ila ukae vizuri na watu humu ndani maana kuna watu wabaya sana na usingenikuta maana walijaribu hata kuniua. Basi akawa anarudia kila mara kuniambia hivi japo hakuwa ananitajia hao watu na mm sikuwa nauliza. Ilienda mpaka na mm nikaanza kuingiwa hofu na wakati mwengine nikawa namkwepa nikihisi labda ameanza kuchanganyikiwa.Mkuu mshana jr hii imenigusa sana. Kuna jamaa yangu wa karibu sana, kama ndugu. Tulimzika last October, alifariki baada ya wiki moja tangu tuachane maeneo ya Kibaha, japo wote tulikuwa tunaishi DSM. Cha ajabu, si mara moja ama 2, mitaani nakutana na watu ambao wajihi wao ni kama jamaa yangu yule. Huwa nashtuka. Nasimama. Natuliza akili. Namuombea jamaa maghfirah. Naendelea.
Mmh!!!Pengine kupunga upepo joto likizidi huko ndani ama kuosha macho[emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji115]kufumania pengine[emoji23]View attachment 456648
Huyu sijui huwa anaenda wapi?
Huyo ni mzururaji hahaha[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji115]
Nafikiri pia inategemea na eneo husika, haya yalikuwa yakinitokea wakati tupo Zambia sehemu camp ya wavuvi ilikuwa inaitwa Mweru wa Ntipa, nikama kulikuwa na mambo fulani ya miujiza hivi, hata mama wakati fulani alikuwa anapatwa na vitu fulani kama kupandisha mizimu, na ili atulie dawa yake ilikuwa ni udongo fulani unakaa katika miamba upo kama chaki ama chokaa, akilamba tu basi ile hali hutoweka kabisa. lkn tulivyorudi huku home Tanzania ile hali ilikwisha kabisa mpaka leo.Bado hujaanzisha kanisa mkuu? Maono hayo tayari, ungeendelea kidogo ungeanza kunena kwa lugha