Kwa kifupi baada ya Mshana Jr kuongelea kuhusu wafu kuonekana iwe kwa hisia, ndoto, harufu au kwa macho kabisa. Hiyo sasa ndio ile hali ambayo biblia inaiongelea, na ule ndio mwili au nafsi isiyokufa na kwa wale wenye imani kama mimi ni kuwa unapokufa unazikwa mwili, huu mwili ndio uliotoka mavumbini. Sasa huo mwingine ndio ule sasa ukifa huku ukiwa huna dhambi, nimeongelea huna dhambi, maana ningesema umeokoka wapo wapinga kristo. Biblia inasema tutavalishwa mwili usio haribika tena, usiohitaji funguo kuingia ndani, wala nauli kupanda gari. Niseme tu Mshana Jr umeleta somo zuri sana, mwenye macho na aone, na mwenye masikio asikie Mshana Jr awafundisha jf.