Marehemu wanaofunga ndoa Tanzania

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Habari za asubuhi wapendwa wote. Katika kupitia ukurasa wa BBC news niliweza kukutaba na taarifa kuwa jamii ya wakurya mkoani mara marehemu huoa na kufunga ndoa. Jf hakiharibiki neno. Hebu naomba mtujuze hii imekaaje na na marehemu hufunga vipi ndoa na mtu aliye hai?
========================================================
Bara la Afrika husifika kwa utajiri wa tamaduni mbalimbali, zipo tamaduni za kufanana baina ya makabila lakini pia kuna tamaduni za kushangaza na kukuacha mdomo wazi, sasa je umewahi kusikia marehemu kutafutiwa mchumba na kuoa.
4d3212996ac583f5033c157d3266e225.jpg


Hiyo ni moja ya taratibu katika baadhi ya koo za jamii ya wakurya nchini Tanzania.
Kwa wale wakurya. Tunaomba ufafanuzi juu ya hili swala jinsi linavyotekelezwa

Karibuni tujadili pamoja.
Source:BBC
 
Back
Top Bottom