Marehemu Swetu: Shukrani toka kwa familia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marehemu Swetu: Shukrani toka kwa familia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JamiiForums, Feb 4, 2010.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot

  #1
  Feb 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,104
  Likes Received: 2,302
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Marehemu Swetu Fundikira

  Inaniwia vigumu sana kutoa shukran kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi kutokana na ushiriki wenu kuanzia kujeruhiwa mpaka mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira. Basi pale nitakapokuwa nimekosea kwa kumsahau kumtaja mhusika naomba radhi.

  Kwa niaba ya familia ya Mzee Ramadhan Said Fundikira na ukoo wa Fundikira kwa ujumla, tunapenda kutoa shukran za dhati kwa watu wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa ndugu yetu mpendwa. Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini pia ningependa kutoa shukrani za pekee kwa uongozi na timu nzima ya Mango Garden Veteran Team kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwetu hata mpaka baada ya mazishi, shukrani pia ziende kwenye vyombo vya habari vyote kwa ujumla yakiwemo magazeti mbalimbali, televisheni na radio zote walioshiriki katika kuupasha umma unyama aliofanyiwa ndugu yetu, naomba niishukuru sana Radio Clouds FM kwa kurusha mwenendo wote tangu mwanzo hadi mwisho wa mazishi, Uongozi wa ASSET Entertainment, Madaktari na wafanyakazi wa MOI, Vituo vya Polisi cha Salender Bridge na Oyster Bay, Mkuu wa kitengo cha maabara cha Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Masheikh wa Masjid Jamia Kinondoni na kila mmoja aliyeshiriki kwa hali na mali katika mchakato mzima wa mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira.

  Sisi wana familia hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu atawalipa Inshaallah.

  Inna Lillah wa Inna Illah Rajiun

  Ismail R. Fundikira

  Msemaji wa Familia
   
 2. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Amen.Jina la Bwana Yesu libarikiwe na mpewe amani.
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0


  heeee dearest, nilikuwa cjakumanya!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...