Marando: Nitatangaza Matokeo kabla ya Kuchakachuliwa

Marando: Nitatangaza Matokeo kabla ya Kuchakachuliwa

Kitendo cha serikali kuogopa matokeo ya uchaguzi kutangazwa live lazima wadau waelewe kuwa kina nia ovu. Vinginevyo, kuna ubaya gani kama matokeo yanayorushwa live ni sawa na yale yaliyobandikwa vituoni?

Na hili suala la kukosa katiba mpya ya wananchi na kulazimika kuendesha uchanguzi kwa tume hii hii ambayo haijawahi kutoa matokea yasiyo na utata ni hatari sana. Na wakishapata sheria mpya ya kulazimisha vyombo vyote vya habari vya binafsi kujiunga na TBC ndiyo basi tena!!

Laiti watu wote wangekuwa na macho...!
 
Mimi ninampongeza Marando kwa kauli yake ya kupambana na mpango ovu wa ulaghai wa CCM! Amesema atatangaza hesabu halali zilizobandikwa vituoni, kabla hazijachakachuliwa na walaghai. Uovu hapa uko wapi? Huu ni zaidi ya mpango mwema!!! BIG UP MARANDO!!!!! We, Tanzanian patriots are behind you, every step of the way!
 
Tuivunje basi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kazi zote zilizokuwa zinafanywa na Tume afanye Mabere Marando
 
Kauli ya Mabere Marando kuwa atatangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka wazi mpango wa UKAWA wa kujitangazia ushindi hata kama ikitokea kuwa umoja huo haujashinda uchaguzi mkuu wa oktoba, 2015 na kutimiza azma yao ya nchi hii kutokutawalika hivyo inapaswa kulaaniwa na wapenda amani nchini kote.
Mkuu kwani kabla ya kauli hii ya marando nani huwa anatangaza matokeo?kwa sababu wote tunafahamu Kuwa tume ya uchaguzi imekuwa ikitumika kama kipaza Sauti tu?refer kauli za katibu wako Mkuu,mr.tembo za 2010.
 
Tuivunje basi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kazi zote zilizokuwa zinafanywa na Tume afanye Mabere Marando
hata pale wapinzani walipoonekana kushinda tulikuwa tunawaambia watangaze.kinana 2010
 
Tuivunje basi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kazi zote zilizokuwa zinafanywa na Tume afanye Mabere Marando

Tutashukuru sana ili nije kutenda haki.Na ole wake mgombea wa ccm
 
Maneno haya wakisikia vijana wa rombo watamuelewa marando
 
Tuivunje basi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kazi zote zilizokuwa zinafanywa na Tume afanye Mabere Marando

Mkuu hii inanikumbusha mwaka 2009 kule DR Congo ambapo kiongozi mmoja wa upinzani maarufu kama Etienne Shikedi alipojitangaza mshindi na kumtafuta jaji wake wa kumuapisha, mwisho wa siku akanywea
 
Kinachoonekana hapa ni muendelezo wa mpango mkakati wa CHADEMA na UKAWA kuwaaanda wafuasi wao kisaikolojia, ili ikitokea wameshindwa watumie turufu hii kuwaaminisha mashabiki wao kuwa kuna "hila" zimefanyika.
 
akiwa kwenye majukwaa ya kisiasa anawataka watanzania kundamana na kupinga EPA, akiwa mahakamani anawatetea mafisadi wa EPA, huyo ndio marando tunaomfaham wala hatusumbui
mkuu wezi halisi wa EPA au ESCROW hawapelekwi mahakamani sijui kama unalijua Hilo?au upofu umekuzidi umri?
 
Kwani Marando amezaliwa 2015?Alitangaza 2000,2005,2010?Tena 2010 wanadai walishinda mbona hakuthubutu kutangaza?Misukule rahisi sana kudanganywa.
 
Nnakumbuka DTV enzi hizo waliwahi kutangaza mshindi wa uchaguzi Zanzibar kuwa ni Maalim Sefu kabla ya tume, tumuite Pasco atukumbushe kama ana kumbukumbu ya hilo.
Kansome hapa
[h=3]Maalim Seif akishinda urais Zanzibar, Shein atakuwa makamu
Mkuu Candid, ingekuwa matokeo ya uchaguzi ni yale ya kwenye ballot, labda hili ndio lingewezekana!, rais anapatikana by vetting and not by voting!, Seif wameisha m vet out kitambo!, Zanzibar ni nchi ya Mapinduzi!, kamwe hawawezi kuirudisha Zanzibar kwa Sultani, au kwa watu ambao hawakushiriki Mapinduzi!. Shida ya Seif sio kuutaka urais, shida yake ni vingora!, kapata katulia!.

Utaratibu ni ule ule wa upigaji kura ya kupitisha katiba, kura za ndio zisipotosha, zitatosheshwa!, kura za urais zisipotosha kumpatia ushindi mgombea wa CCM, zitatosheshwa, na hiki ndicho kitu kilichokikifanyika huko siku zote!.

Endelea kusubiria kwa hamu, ila ukweli ndio huo, kamwe, haitakaa itokee wairudishe Zanzibar kwa mwarabu!. Wanaoamua Rais wa Zanzibar awe nani ni system ya bara, Maalim siku zote huwa anashinda kwenye ballot but not kwenye vetting!, kwa usalama wa hili koloni letu la visiwa vya Zanzibar na Pemba, Maalim Seif is a liability!, vetting imemgomea, ataendelea kuwa makamo wa kwanza, vigora na marupurupu manene!, katulia tuli!.

Mapinduzi Daima!.

Pasco
[/h]
 
wakili maarufu na shushu aliyebobea tangu enzi za mwalimu jk nyerere amesema mwaka huu atajitoa muhanga kutangaza matokea ya urais kabla ya matokeo hayo kuchakachuliwa. Hii ni ishara ya wazi kuwa watanzania mwaka huu hawatakubali kuburuzwa na tume ya watawala.

Chanzo: Gazeti la tanzania daima
kwani nani asiyejua kuwa huyu ni shushu wa kudumu wa ccm kila anapokwenda chama kinaingia kwenye migogoro na kusinyaa kama nccr,cdm
 
Wakili Maarufu na shushu aliyebobea tangu enzi za Mwalimu JK Nyerere amesema mwaka huu atajitoa Muhanga kutangaza matokea ya Urais kabla ya matokeo hayo kuchakachuliwa. Hii ni ishara ya wazi kuwa Watanzania mwaka huu hawatakubali kuburuzwa na tume ya watawala.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Kwa hiyo mwezi October jamaa atakuwa mwenyekiti wa NEC taifa?
 
Wakili Maarufu na shushu aliyebobea tangu enzi za Mwalimu JK Nyerere amesema mwaka huu atajitoa Muhanga kutangaza matokea ya Urais kabla ya matokeo hayo kuchakachuliwa. Hii ni ishara ya wazi kuwa Watanzania mwaka huu hawatakubali kuburuzwa na tume ya watawala.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Hivi yupo wapi huyu?
 
Back
Top Bottom