Marafiki wasiokupenda wako hivi

Marafiki wasiokupenda wako hivi

Habari za jukwaa hili.
Nadhani hamjambo kabisa.

Mara nyingi watu kwa maelfu hudhani kuwa na marafiki wenye mtizamo chanya,
lakini wengine huangukia katika kundi la marafiki wasio na upendo ndani yao.

Hizi ni baadhi ya ishara zitakazo kuonesha kuwa rafiki zako ni bora ama laa.


(1)Marafiki walio wanafiki mara nyingi hawatakualika katika shughuli yoyote watakayoifanya.

(2)Mtapiga picha ya pamoja iwe watu kumi na kuendelea lakini katika mitandao wataweka picha ambayo wewe haumo.

(3)Mara nyingi wanakufanya kuwa kichekesho kwao

(4)Ukiongea pointi za hali ya juu watacheka na hujui kwanini.


Pole kwa ku-snitch-iwa.
 
mi nilikuwa na frnd wangu, nilimwamini na kumpenda,mzee wake akafungua biashara flani hivi, basi ikabidi nitumie mgongo wake kumwombea kazi ma msapu wangu..siku zikasogea, jamaa akaanza kunisaliti na kulimega tunda langu. Niliumia sana, nikamuuliza mchizi, akakataa na kusema wanamzushia, ma msupu naye akakataa, nilichunguza kama miezi 3 nikapata ushaidi, nikamwagia ushaidi frnd wangu. Alilia kama mtoto lakini niligundua ni mnafiki. Tangu hapo sina tena haja ya kumwamini rafiki yeyote yulee.
 
Ni kwl marafiki wanafiki wanaumiza sana ila maumivu yao mm naona nitofauti nayandugu wa damu kbs unaowaamini kuliko marafiki na umewasadia alafu kesho wanakugeuka wakishapata mwelekeo wa maisha inaumaa sana mm bora maumivu ya rafiki mnafiki
 
(5) Watachukua mawazo yako iwe ya biashara au chochote chema na kufanya pasipo kukushirikisha
(6) Watakuwa nawe wakati wa raha na kukukimbia( nduki) pindi unapohitaji msaada wao.

Uko sahihi kabsaaaa JC. Yalishanikuta hayaaa
 
  • Thanks
Reactions: J C
Na sisi ni marafiki wa watu wengine, ni wanafiki kama wanavyo tufanyia wengine huku tukiona hatustahili ivyo wakati twawatendea wenzetu ivyo ivyo.mtenda akitendewa
 
Mm ndo sisemi mana ninaishi nao rum moja na wengn majiran
Napita zanguuu
 
Jamani mwasu big up.unabusara sana

Nimejifunza siku zote jitahidi kuutuliza moyo wako unapoumizwa na mtu kulikoni kutaka kupambana na mtu yako maana ni kuzidi kujiongezea machungu na kuwapa watu faida kuendeleza chokochoko. Mimi hili watu hawelewi ilikuwaje wengi wanadhani niliamua mwenyewe kuacha, na hivyo hakuna anaeuliza kitu kwa kuwa hakukua na malumbano. Jitahidi kila unapoweza kutotengeneza uadui na binadamu.
 
Mie nilijionaga kama nime lack kitu fulani hivi kutokuwa na eti rafiki wa damu....kumbe nipo katika mstari sahihi enhee?
 
Kuna rafiki nilimpenda kweli kweli cijui kwa mini alifanyayale yasionipendza machon hahaha yeye na familia yakewalijipanga kunidanganya na sikuona sababu ya kunidaganya aiseee citaki kukumbuka mimi hats cijui ilikuwaje urafiki kazi kweli kweli
 
Habari za jukwaa hili.
Nadhani hamjambo kabisa.

Mara nyingi watu kwa maelfu hudhani kuwa na marafiki wenye mtizamo chanya,
lakini wengine huangukia katika kundi la marafiki wasio na upendo ndani yao.

Hizi ni baadhi ya ishara zitakazo kuonesha kuwa rafiki zako ni bora ama laa.


(1)Marafiki walio wanafiki mara nyingi hawatakualika katika shughuli yoyote watakayoifanya.

(2)Mtapiga picha ya pamoja iwe watu kumi na kuendelea lakini katika mitandao wataweka picha ambayo wewe haumo.

(3)Mara nyingi wanakufanya kuwa kichekesho kwao

(4)Ukiongea pointi za hali ya juu watacheka na hujui kwanini.


Who cares hata kama atajiengua kwangu
 
Nadhani tatizo lililopo ni kwa kila mmoja kutaraji kupita kiasi kutoka kwa mwenziwe...hakuna aliyetayari kujiona yeye ndiye awe msaada kwa mwenzie plus elimu "za kisasa" za kushauriana kuchagua marafiki wenye maendeleo (vyovyote wanavyoisema) lakini kwa mfumo huo tayari tutarajie udhaifu tunaokabiliana nao hivi sasa...kwani ni rahisi kuwakwepa marafiki wa ukweli (moyoni) na kukimbilia marafiki kwa kigezo cha uwezo.

Na kama ilivyo ngumu kwa dunia ya leo kumpata mwenza wa ukweli wa ndoa, vivyo hivyo bado (ingawa ni kwa kiwango kidogo sana) wapo marafiki wa ukweli na dhati....rafiki aliye tayari kupoteza kwa ajili ya mwenzake...anayemfaa mwenzake kuliko hata ndugu wa kuzaliwa.
 
Hivi kweli MTU unaweza usiwe na shost hata mmoja eti mid rafiki angu mume wangu tusiibiane hapa kuna siku tu utatamani kutoka na rafiki
 
Back
Top Bottom