Marafiki, ndugu na wadau wote wa jukwaa hili

Marafiki, ndugu na wadau wote wa jukwaa hili

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,042
Reaction score
16,872
Habari JamiiForums

Siku zinakimbia, miaka inageuka, na umri unasogea.

Nakumbuka ni kama juzi tu Mh. Lowasa alivyotikisa Tanzania kwenye kampeni za Urais 2015.

Ni kama juzi tu tangu hayati Magufuli na itikadi zake, pamoja na misimamo mikali kwenye uongozi.

Miaka inakimbia, watu waliozaliwa mwaka 2000 ni watu wazima, si watoto tena; wengi wao wanafamilia kabisa.

Mtoto aliyezaliwa 2005, wakati Mh. Kikwete anachukua nchi kama kiongozi wa awamu ya nne, tayari ukimzingua anakuzingua, haogopi tena. Sasa ewe mtu mzima mwenzangu, fanya haya:

  1. Punguza ulevi na kujiamini kupita kiasi.
  2. Acha kupost status za WhatsApp zisizoeleweka; mara nyingi hushusha heshima yako.
  3. Punguza kutongoza ovyo, haswa mabinti wadogo.
  4. Tenga muda wa kusimamia miradi yako binafsi kuliko kubase sana na hiyo ajira.
  5. Mke ni muda wa kumuheshimu na kumpenda mume; na mume mjali na kumpa heshima mkeo.
  6. Epuka kuamua mambo magumu peke yako, kama vile ukidhulumiwa au kutapeliwa; badala yake shirikisha mamlaka za utetezi au usuluhishi.
  7. Kwa wenye vipato vikubwa, ajiri dereva akuendeshe, pamoja na kuwa na mwanasheria, japo si lazima.
  8. Jitoe, acha kiburi, shiriki kwenye misiba, makongamano na vikao mbalimbali; shiriki mambo yote ya kijamii ikiwa nafasi inaruhusu.
  9. Anza kusali au kuswali.
  10. Ishi maisha yako uliyochagua, ila usivunje sheria za nchi.
Miaka 56 si michache, alhamdulillah.
 
Habari jamiiforum.

Siku zinakimbia,miaka inageuka na umri unasogea.

Nakumbuka ni kama juzi tu Mh lowasa alivyotikisa Tanzania Kwenye kampeni za Urais 2015.

Ni kama juzi tu tangu hayati Magufuli na itikadi zake pamoja na misimamo mikali kwenye uongozi.

Miaka inakimbia,watu waliozaliwa mwaka 2000 ni watu wazima si watoto tena wengi wao wanafamilia kabisa.

Mtoto aliyezaliwa 2005 wakati Mh kikwete anachukua nchi kama kiongozi wa awamu ya nne.tayari ukimzingua anakuzingua haogopi tena. Sasa ewe mtu mzima mwenzangu fanya haya.

1.Punguza ulevi na kujiamini kupita kiasi

2.Acha kupost status WhatsApp zisizoeleweka mara nyingi hushusha heshima yako.

3.Punguza kutongoza ovyo haswa mabinti wadogo

4.Tenga muda wa kusimamia miradi yako binafsi kuliko kubase Sana na hiyo ajira.

5.Mke ni muda wa kumuheshimu na kumpenda mume.na mume mjali na kumpa heshima mkeo.

6.Epuka kuamua mambo magumu peke yako kama vile ukidhulumiwa au kutapeliwa.badala yake shirikisha mamlaka za utetezi au usuluhishi.

7.kwa wenye vipato vikubwa ,ajiri Dereva akuendeshe,pamoja na kuwa na mwanasheria,japo si lazima.

8.Jitoe, Acha kiburi shiriki kwenye ,misiba,makongamano na vikao mbalimbali, shiriki mambo yote ya kijamii ikiwa nafasi inaruhusu.

9.Anza kusali,au kuswali.

10.Ishi maisha yako uliyochagua ila usivunje Sheria za nchi.

Miaka 56 si michache alhamdulillah
Nimefurahi sana kuwa mmoja ninayesema happy birthday Engineer Jack Daniel ,nimeyapenda sana haya maneno .
Ahsante nayaishi ,mkuu Seran naendelea kujifunza mengi you just wait the new version of me
 
Subiri ata week ndio urudishe shukrani mkuu😂 unaweza ishia njiani ohoo..
Niogope sana ukiona nimezungumza jambo nikacode mix kingereza dada jua hilo jambo niko serious.

Toka asubuhi nisome yale madini baada ya kurudi kwangu ,nilikuwa napanda sofa napachungulia kwa mzee saidi kuna roho inasema nenda sasa mkewe atakuwa anapika ila nimekataa katakata nikaishia kumchungulia yeye na mkewe wanavyokulq na mwisho kakoga huyo anaenda kijiweni .

Ni mtihani ila nitaweza kikubwa nishaamua
 
Niogope sana ukiona nimezungumza jambo nikacode mix kingereza dada jua hilo jambo niko serious.

Toka asubuhi nisome yale madini baada ya kurudi kwangu ,nilikuwa napanda sofa napachungulia kwa mzee saidi kuna roho inasema nenda sasa mkewe atakuwa anapika ila nimekataa katakata nikaishia kumchungulia yeye na mkewe wanavyokulqna mwisho kakoga huyo anaenda kijiweni .
a m
Ni mtihani ila nitaweza kikubwa nishaamua
Jitahidi uwe unapika cha kwako mkuu na mnaishije unaona mpaka kwa jirani wanavyopakuana jmn😆😆hapo ss zamu yako nawe nenda ukajaribu bahati🤌🏾
 
Jitahidi uwe unapika cha kwako mkuu na mnaishije unaona mpaka kwa jirani wanavyopakuana jmn😆😆hapo ss zamu yako nawe nenda ukajaribu bahati🤌🏾
Nimejenga nyumba yangu iko juu kidogo hivyo kuna dirisha moja linanipa mambo mengi sana hasa umbea wa majirani nikiamua kuwafuatilia kwa kina dada
 
Back
Top Bottom