Maradona Aharibiwa Sura Yake na Mbwa Wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maradona Aharibiwa Sura Yake na Mbwa Wake!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, Apr 1, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maradona Aharibiwa Sura Yake na Mbwa Wake
  [​IMG]
  Diego Maradona amejeruhiwa vibaya mdomo wake na mbwa wake Wednesday, March 31, 2010 10:39 PM
  Diego Maradona aliwahishwa hospitali na kufanyiwa operesheni ya dharura kurekebisha sura yake baada ya kung'atwa vibaya na mbwa wake alipojaribu kumbusu. Madaktari nchini Argentina walilazimika kumfanyia operesheni ya dharura gwiji wa soka duniani, Diego Maradona ambaye alijeruhiwa vibaya na mmoja wa mbwa wake.

  Maradona alishonwa nyuzi 10 kwenye mdomo wake wa juu baada ya kung'atwa na mbwa wake mwenye sura ya kutisha anayeitwa Bela ambaye ni jamii ya mbwa wa kichina wanaoitwa Shar-Pei.

  Inadaiwa kuwa Maradona alijaribu kumbusu ili kumliwaza mbwa wake huyo aliyekuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo ndipo mbwa huyo kwa hasira alipomshambulia mdomoni.

  Maradona alipata majeraha makubwa kwenye mdomo wake wa juu na alikimbizwa hospitali huku akivuja damu nyingi.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Maradona atalazimika kupumzika kwa siku tatu baada ya kutumia masaa 15 hospitalini.

  Maradona hakuzungumza na waandishi wa habari lakini Fernando Molina, mpenzi wa dada yake Maradona, Dalma, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa Maradona anaendelea vizuri na amepumzika nyumbani kwake.

  Maradona aliwahi kulazwa kwenye hospitali hiyo hiyo mwaka 2007 kutokana na maradhi aliyopata kutokana na unywaji pombe uliokithiri.

  Maradona mwenye umri wa miaka 49 ndiye anayetarajiwa na Waargentina kuiongoza timu ya taifa ya Argentina kulinyakua kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

  Maradona alichaguliwa kuwa kocha wa Argentina mwaka 2008 baada ya kujiuzulu kwa kocha Alfio Basile.

  Pamoja na Argentina kutoonyesha uwezo mkubwa katika mechi za hatua ya awali ya kufuzu fainali ya kombe hilo, hatimaye ilifanikiwa kupata tiketi ya kuja Afrika baadae mwaka huu.

  Argentina ipo kundi moja na Nigeria pamoja Ugiriki na Korea Kusini.
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Apr 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Siku ya wajinga.
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama ni ya kweli hadithi hii, tutumie kesho
   
 4. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hahahahahahahahahahahahahahahahah!!!!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,183
  Trophy Points: 280
  Manyang'au ni wawtu watungao maneno ya uwongo na kuyasambaza kwa watu.
   
 6. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ni habari ya kweli kabisa.......kama huamini jaribu ku google utajionea source mbali mbali
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndo faida ya kuabudu hayawani.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  habari hii ni kweli angalieni soccernet, skysport etc
   
 9. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Ooohoooo,bwabwa huyooo!!!
   
Loading...