Mara: Polisi yawashikilia Wafuasi wa CHADEMA Waliokuwa wanafanya Usafi kabla ya Kongamano la Katiba

Hawa chadema ni kama kenge,kusikia kwake Hadi damu zimtoke masikioni,waanze kwanza na makongamano ya kubadili katiba ya chadema ili gaidi aliyepo nyuma ya nondo aondoke madarakani
Haya mnayowafanyia ndio kuonyesha viwango vya usikivu wa walio na mamlaka na vyombo saidizi, vitekelezavyo unyanyasaji na uvunjifu wa katiba kwa makusudi. Tunataka Katiba mpya.
 
Ccm kufanya mikutano ni sawa,lakini wakifanya Chadema wanakamatwa
Mtawala anayejua aliiba kura ndipo akaweza kushika madaraka hawezi kukuelewa unapodai katiba na tume huru. Unampokonya madaraka!!! ebo... siyo rahisi hivyo eti.

Kama ilivyo kwa mwizi au tapeli kukiri na kurudisha alichoiba au alichotapeli, ndivyo hawa wezi walivyo wagumu kukubaliana na matakwa ya wananchi.

Hii safari imeanza na wachache, lakini siku zinavyosonga mbele, watawala wasipokubaliana na sauti ya umma, NGUVU ya umma itawasagasaga. Tungoje tuyaone.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA

Leo jumamosi tarehe 04/09/2021 kulikuwa na kongamano la Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Bavicha Taifa katika Mkoa wa Mara wilaya ya Musoma mjini.

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Mara akatangaza kuwa Leo itakuwa siku ya usafi Mkoa wa Mara na hivyo kila Mwananchi ambaye hatashiriki atapigwa faini ya shilingi elfu hamsini, Bavicha wakawatangazia wanachama na wananchi waje na vifaa vya usafi ili washiriki kufanya usafi na Mkuu wa Mkoa na baadaye wataendelea na kongamano Lao lililokuwa lifanyike katika ofisi ya Chama Wilaya.

Usiku wa saa Saba na nusu Jeshi la Polisi walivamia ofisi za Chama Wilaya na kuchukua mahema na Viti vilivyokuwa vimeandaliwa Kwa ajili ya kongamano hilo .

Leo Jumamosi asubuhi polisi wamezingira na kufunga Kwa kufuli lao Geti la kuingia ofisini na kuizingira ofisi , na hakuna dalili kuwa wanafanya usafi na badala yake wanawakamata wananchi ambao walikuwa tayari kushiriki zoezi la kufanya usafi.

Waliokamatwa mpaka sasa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Musoma Mjini ni pamoja na;

(1). PATIRICK MWENGE NYABAGWE.
(2). GEORGE BURUMA RUBARE.
(3). NAHIMA MZURI KWAO SELEHIMAN.
(4). MAGRET EMANUEL.
(5). MUSILA JUMA.

Tunaendelea kufuatilia ukiukwaji na ukandamizaji wa Haki dhidi ya raia unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi wakishirikina na vyombo vingine vya Dola .

Tunalaani na kukemea ukiukwaji na uvunjaji huu wa Katiba NA Sheria za Nchi unaoendelea kufanywa na kupandikiza mbegu za chuki ,ubaguzi,uhasama na mgawanyiko ndani ya jamii ya Watanzania Kwa misingi ya kiitikadi.

Tunaendelea kusisitiza kuwa ni Haki ya Watanzania kukusanyika na kujadiliana kuhusu Katiba Mpya na kufanya hivyo hakuna kipengele chochote cha Katiba au sheria kimevunjwa au kukiukwa ,isipokuwa wanaozuia ndio wanavunja Katiba na sheria za Nchi yetu.

Tunaendelea kuvitaka vyombo vya Dola kutimiza majukumu Yao Kwa weledi na kufuata sheria badala ya kutumia mabavu kupambana na wananchi ambao wanataka kujadiliana kuhusu Katiba ya Nchi Yao Kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Tunajiuliza Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora iko wapi ? Au haioni wala kusikia ukiukwaji huu wa Haki za Binadamu unaoendelea kutendeka nchini?

Imetolewa Leo Jumamosi tarehe 04 Septemba,2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki,, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Tusonge mbele watanzania ipo siku hakuna kisichowezekana kwa Mungu mbona yule bwana hayupo leo hii? Wataondoka wote waikandamizao nchi hii kwa maslahi binafsi.
 
Watanzania ni makondoo, kila wanachofanyiwa na serikali ndio.
Wapinzani wakiinuka kupinga wananchi wanakuwa upande wa serikali
 
Msajili wa vyama afanye nini sasa?awawekee dhamana au?
Msajili haoni kuwa vyama vya upinzani havitendewi haki?Huwa ni mwepesi kujitokeza pale vyama vinapokosea,ila vinapotendewa vibaya anakuwa kama amekalia gundi matakoni!
 
Shida ni weledi wa kitanzania
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA

Leo jumamosi tarehe 04/09/2021 kulikuwa na kongamano la Katiba Mpya lililokuwa limeandaliwa na Bavicha Taifa katika Mkoa wa Mara wilaya ya Musoma mjini.

Juzi Mkuu wa Mkoa wa Mara akatangaza kuwa Leo itakuwa siku ya usafi Mkoa wa Mara na hivyo kila Mwananchi ambaye hatashiriki atapigwa faini ya shilingi elfu hamsini, Bavicha wakawatangazia wanachama na wananchi waje na vifaa vya usafi ili washiriki kufanya usafi na Mkuu wa Mkoa na baadaye wataendelea na kongamano Lao lililokuwa lifanyike katika ofisi ya Chama Wilaya.

Usiku wa saa Saba na nusu Jeshi la Polisi walivamia ofisi za Chama Wilaya na kuchukua mahema na Viti vilivyokuwa vimeandaliwa Kwa ajili ya kongamano hilo .

Leo Jumamosi asubuhi polisi wamezingira na kufunga Kwa kufuli lao Geti la kuingia ofisini na kuizingira ofisi , na hakuna dalili kuwa wanafanya usafi na badala yake wanawakamata wananchi ambao walikuwa tayari kushiriki zoezi la kufanya usafi.

Waliokamatwa mpaka sasa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Musoma Mjini ni pamoja na;

(1). PATIRICK MWENGE NYABAGWE.
(2). GEORGE BURUMA RUBARE.
(3). NAHIMA MZURI KWAO SELEHIMAN.
(4). MAGRET EMANUEL.
(5). MUSILA JUMA.

Tunaendelea kufuatilia ukiukwaji na ukandamizaji wa Haki dhidi ya raia unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi wakishirikina na vyombo vingine vya Dola .

Tunalaani na kukemea ukiukwaji na uvunjaji huu wa Katiba NA Sheria za Nchi unaoendelea kufanywa na kupandikiza mbegu za chuki ,ubaguzi,uhasama na mgawanyiko ndani ya jamii ya Watanzania Kwa misingi ya kiitikadi.

Tunaendelea kusisitiza kuwa ni Haki ya Watanzania kukusanyika na kujadiliana kuhusu Katiba Mpya na kufanya hivyo hakuna kipengele chochote cha Katiba au sheria kimevunjwa au kukiukwa ,isipokuwa wanaozuia ndio wanavunja Katiba na sheria za Nchi yetu.

Tunaendelea kuvitaka vyombo vya Dola kutimiza majukumu Yao Kwa weledi na kufuata sheria badala ya kutumia mabavu kupambana na wananchi ambao wanataka kujadiliana kuhusu Katiba ya Nchi Yao Kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Tunajiuliza Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora iko wapi ? Au haioni wala kusikia ukiukwaji huu wa Haki za Binadamu unaoendelea kutendeka nchini?

Imetolewa Leo Jumamosi tarehe 04 Septemba,2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki,, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Wangekwenda kufanya usafi kwenye kambi za polisi ambazo ni chafu.
 
CHADEMA nendeni mahakamani mahakamani itafasiri sheria hebu acheni kulalamika kila kukicha,mbona mna mawakili wasomi shida ipo wapi mnaonewa kila siku na polisi.
 
Back
Top Bottom