Mara: Mifuko 600 ya saruji iliyoibwa shuleni yapatikana

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Zaidi ya Mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni inadaiwa kuibwa katika mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara.

Mifuko hiyo imepatikana ikiwa imehifadhiwa katika nyumba moja katika kijiji cha Karukekere umbali wa zaidi ya kilomita 15 kutoka unapotekelezwa mradi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara inayojengwa katika kijiji cha Bulamba wilayani Bunda mradi ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh4 bilioni huku serikali ikiwa tayari imetoa Sh3 bilioni kwaajili ya mradi huo.

Akizungumza leo Oktoba 29, 2023 kijijini Karukekere baada ya kuiona mifuko hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo ni la aibu na halikubaliki.
"Hii saruji iliyohifadhiwa humu tumejiridhisha pasipo na shaka ni mali ya Serikali kwa sababu kwanza miradi ya Serikali inajengwa kwa saruji yenye kiwango cha 42.5,tofauti na ile saruji ya mtaani ambayo ni 32.5."Pia saruji ya Simba imeadimika mtaani na sisi tulitoa oda moja kwa moja kiwandani, lakini pia mazingira tuliyoyakuta hapa ni kiashiria tosha huu mzigo ni wa wizi," alisema.Alifafanua mzigo huo wa saruji ambao bado haujajulikana namna uliondolewa eneo la mradi,ulifikishwa kijijini hapo Oktoba 24,saa 9 alasiri na ulikuwa umeanza kuuzwa kwa Sh21,000 kvwa mfuko tofauti na bei ya jumla ya Sh24,000.Kutokana na hali hiyo,mkuu huyo wa wilaya aliagiza kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba iliyotumika kuhifadhi mifuko hiyo,huku msako ukiendelea wa kumtafuta mdogo wa mmiliki huyo, Maise Magesa anayedaiwa kuleta mzigo huo katika eneo hilo.Naamini kuna watu wetu wanahusika moja kwa moja kwenye hili tukio,sasa tumeanza uchunguzi sambamba na ukaguzi wa vifaa vyote kila kitu tutaangalia tulinganishe kile kilichoketwa na kile kilichotumika hatutasamehe hata msumari mmoja, lazima hii tabia ikomeshwe," alisisitiza Awali, akizungumza kabla ya kukamatwa mtuhumiwa wa kwanza,Nyandago Magesa alisema hajui chochote kuhusiana na saruji hiyo kwa maelezo kuwa saruji hiyo ililetwa na mdogo wake.Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Karukekere walisema walishuhudia mzigo wa saruji ukishuswa kwenye nyumba hiyo bila lujua kama ni mali ya wizi."Mzigo wa kwanza ulishushwa saa 9 mchana na baadaye mingine ilifuata,lori lilishusha mzigo mara nne na tulijua mwenzetu amefungua biashara mpya," amesema Joshua Deya. Boniface Maiga, aliitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaohujumu miradi kwa maelezo kuwa tabia hiyo inasababisha miradi kutokuwa na thamani ya fedha halisi.
 
Mbona hatimujasikia nani waliwezesha mchongo huu na wako wapi? Kwamba unaweza Iba semi trailer nzima kizembe hivyo?
 
Zaidi ya Mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni inadaiwa kuibwa katika mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara.

Mifuko hiyo imepatikana ikiwa imehifadhiwa katika nyumba moja katika kijiji cha Karukekere umbali wa zaidi ya kilomita 15 kutoka unapotekelezwa mradi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara inayojengwa katika kijiji cha Bulamba wilayani Bunda mradi ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh4 bilioni huku serikali ikiwa tayari imetoa Sh3 bilioni kwaajili ya mradi huo.

Akizungumza leo Oktoba 29, 2023 kijijini Karukekere baada ya kuiona mifuko hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo ni la aibu na halikubaliki.

Mifuko 600 ya cement haiwezi kuwa na hiyo thamani ya 20M labda kwakua ni ya serikali maana vitu vinavyo nunuliwa kwenye miradi ya serikali bei huwekwa juu sana ili watu wapige.
 
Ripoti haijakamilika. Malizieni uchunguzi ili tujue wahusika, Zilisafirishajwe? Kwa nini zilipelekwa karukekele na si Kijiji kingine? Inamaana mwizi (waizi) wako karukekele?

Hata hivyo, Kwa Halmashauri za Bunda (Mji na vijijini, upigaji ni suala kawaida sana kwao. Kwanza kabisa, Kwa ripoti zote za CAG, halmashauri hizo huwa zinapata(ga) hati chafu.
 
Waweza kuta mradi unahitaji mifuko 200.

Wangeiba mifuko 200 hata wasingetafutwa.

Ila wanashusha mali ya wizi mchana 😄
 
Zaidi ya Mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni inadaiwa kuibwa katika mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara.

Mifuko hiyo imepatikana ikiwa imehifadhiwa katika nyumba moja katika kijiji cha Karukekere umbali wa zaidi ya kilomita 15 kutoka unapotekelezwa mradi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Mara inayojengwa katika kijiji cha Bulamba wilayani Bunda mradi ambao unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh4 bilioni huku serikali ikiwa tayari imetoa Sh3 bilioni kwaajili ya mradi huo.

Akizungumza leo Oktoba 29, 2023 kijijini Karukekere baada ya kuiona mifuko hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo ni la aibu na halikubaliki.
"Hii saruji iliyohifadhiwa humu tumejiridhisha pasipo na shaka ni mali ya Serikali kwa sababu kwanza miradi ya Serikali inajengwa kwa saruji yenye kiwango cha 42.5,tofauti na ile saruji ya mtaani ambayo ni 32.5."Pia saruji ya Simba imeadimika mtaani na sisi tulitoa oda moja kwa moja kiwandani, lakini pia mazingira tuliyoyakuta hapa ni kiashiria tosha huu mzigo ni wa wizi," alisema.Alifafanua mzigo huo wa saruji ambao bado haujajulikana namna uliondolewa eneo la mradi,ulifikishwa kijijini hapo Oktoba 24,saa 9 alasiri na ulikuwa umeanza kuuzwa kwa Sh21,000 kvwa mfuko tofauti na bei ya jumla ya Sh24,000.Kutokana na hali hiyo,mkuu huyo wa wilaya aliagiza kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba iliyotumika kuhifadhi mifuko hiyo,huku msako ukiendelea wa kumtafuta mdogo wa mmiliki huyo, Maise Magesa anayedaiwa kuleta mzigo huo katika eneo hilo.Naamini kuna watu wetu wanahusika moja kwa moja kwenye hili tukio,sasa tumeanza uchunguzi sambamba na ukaguzi wa vifaa vyote kila kitu tutaangalia tulinganishe kile kilichoketwa na kile kilichotumika hatutasamehe hata msumari mmoja, lazima hii tabia ikomeshwe," alisisitiza Awali, akizungumza kabla ya kukamatwa mtuhumiwa wa kwanza,Nyandago Magesa alisema hajui chochote kuhusiana na saruji hiyo kwa maelezo kuwa saruji hiyo ililetwa na mdogo wake.Wakisimulia tukio hilo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Karukekere walisema walishuhudia mzigo wa saruji ukishuswa kwenye nyumba hiyo bila lujua kama ni mali ya wizi."Mzigo wa kwanza ulishushwa saa 9 mchana na baadaye mingine ilifuata,lori lilishusha mzigo mara nne na tulijua mwenzetu amefungua biashara mpya," amesema Joshua Deya. Boniface Maiga, aliitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaohujumu miradi kwa maelezo kuwa tabia hiyo inasababisha miradi kutokuwa na thamani ya fedha halisi.
"Hakuna wizi nyie" jasema minister
 
Back
Top Bottom