Alikuwa na mtaalamu wake wa kufungua mifuko yote na kupunguza kiasi cha saruji kati ya kg 5 hadi 10

BRN

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
4,229
5,260
Salaam,

Re bagging kwa tafsiri ya kiingereza…to unbag an item and put it in another bag, or to put an item back into its bag na kwa tafsiri isiyo rasmi ya lugha ya kiswahili ni kutoa kitu kwenye mfuko wake wa awali na kuweka kwenye mfuko mwingine, au kurudisha kwenye mfuko wake wa awali.

Nisiwachoshe kwa hizo tafsiri, lengo la Uzi huu ni kuwafungua macho kile nilichoshuhudia miaka 15 iliyopita kwenye duka la kuuza saruji kwa rejareja Tandika Dar es Salam.

Ilikuwa inafanyika hivi; mara baada ya kupokea shehena ya saruji kutoka kiwandani, kijana aliyekuwa anasimamia mauzo alikuwa na mtaalamu wake wa kufungua mifuko yote na kupunguza kiasi cha saruji kati ya kg 5 hadi 10 na kuifunga upya na ile aliyoipata baada ya kupunguza kwenye mifuko pia huiweka kwenye mifuko mingine hivyo kuwa na mifuko ya ziada.

Hata kwa mangumi wauzaji wa duka hilo hawakuwa tayari kuuza saruji kwa mteja ikitokea mteja amefika wakati mzigo unateremshwa kwenye gari, zitatafutwa sababu za uongo na kweli ili aondoke kwani hawakuwa tayari kuuza mzigo kabla hawajautia vidole.

Hii ilikuwa miaka 15 iliyopita na kwa vile ilikuwa inawapa faida sidhani kama watakuwa wameiacha.

Tahadhari: Nawaomba mchunguze uzito wa saruji mnapoenda kununua.

Wasalam.
 
Back
Top Bottom