Mapya yaibuka sakata la Wakurugenzi DSTV kusimamishwa, mapenzi pia yahusishwa!

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,567
65,408
Wakuu, kama bado hukuwa na taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maisha Magic Bongo ndani ya DSTV Barbara Kambogi na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite, tafadhali pitia hapa

Leo tutaangazia ripoti iliyotumwa Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa filamu nchini bwana Isike Samweli kwa undani.

Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.

Bwana Isike alituma ushahidi usio na chembe ya shaka kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi baina ya Mkurugenzi msaidizi bwana Onesmus Ndarite na mzalishaji mkuu na mwanzilishi wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka almaarufu Pili.

Mapenzi yaliponoga bwana Onesmus akageuka sehemu ya kipindi hicho, na kwa kutumia mamlaka hayo akawaondosha katika kipindi hicho waigizaji wakuu wawili Dullvani ‘Da Zuu’ pamoja na mpenzi wake katika maigizo hayo Masantula.

Waigizaji hao waliondoshwa kwa amri kutoka kwa bwana Onesmus aliyejitwalia madaraka ndani ya kipindi hicho cha vichekesho baada ya waigizaji hao kuomba waongezewe maslahi kwa kuwa kipindi hicho kilipata kukubalika kati ya watazamaji walio wengi nao umaarufu wao kuongezeka.

Hivi ninavyoandika hapa waigizaji hao wawili sio sehemu tena ya maigizo hayo ya vichekesho na ni kwa wao kuomba stahiki zao za nyongeza katika maslahi.

Kupitia madaraka aliyokuwa nayo ndani ya kitengo hicho cha tamthilia za Kiswahili ndani ya DSTV, bwana Onesmus alitumia nafasi hiyo kukipa muda zaidi kipindi hicho cha mahabuba wake Gladness Kifaluka kuliko ambavyo kilistahili kutokana na ufinyu wa ubora wake.

Mpaka sasa kipindi hicho kingalipo, japo msisimko umepungua baada ya waigizaji hao viongozi kuondoshwa kwa maagizo ya mpenzi wa boss wao bwana Onesmus.

Pichani ni muanzilishi na mzalishaji mkuu wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladness Kifaluka.

Video ni muigizaji mkongwe na mtayarishaji nguli wa filamu nchini bwana Deogratius Shija ‘Shija’ akithibitisha tuhuma za rushwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini.

Ni yuleyule ripota kutokea hapa JF, mwenye chanzo chake nyeti.

Nifah.

IMG_4124.jpeg

Wakuu, kama bado hukuwa na taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maisha Magic Bongo ndani ya DSTV Barbara Kambogi na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite, tafadhali pitia hapa

Leo tutaangazia ripoti iliyotumwa Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa filamu nchini bwana Isike Samweli kwa undani.

Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.

Bwana Isike alituma ushahidi usio na chembe kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi baina ya Mkurugenzi msaidizi bwana Onesmus Ndarite na mzalishaji mkuu na mwanzilishi wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladnes Kifaluka almaarufu Pili.

Mapenzi yaliponoga bwana Onesmus akageuka sehemu ya kipindi hicho, na kwa kutumia mamlaka hayo akawaondosha katika kipindi hicho waigizaji wakuu wawili Dullvani ‘Da Zuu’ pamoja na mpenzi wake katika maigizo hayo Masantula.

Waigizaji hao waliondoshwa kwa amri kutoka kwa bwana Onesmus aliyejitwalia madaraka ndani ya kipindi hicho cha vichekesho baada ya kuomba waongezewe maslahi kwa kuwa kipindi hicho kilipata kukubalika kati ya watazamaji walio wengi nao umaarufu wao kuongezeka.

Hivi ninavyoandika hapa waigizaji hao wawili sio sehemu tena ya maigizo hayo ya vichekesho na ni kwa wao kuomba stahiki zao za nyongeza katika maslahi.

Kupitia madaraka aliyokuwa nayo ndani ya kitengo hicho cha tamthilia za Kiswahili ndani ya DSTV, bwana Onesmus alitumia nafasi hiyo kukipa muda zaidi kipindi hicho cha mahabuba wake Gladnes Kifaluka kuliko ambavyo kilistahili kutokana na ubora wake.

Mpaka sasa kipindi hicho kingalipo, japo msisimko umepungua baada ya waigizaji hao viongozi kuondoshwa kwa maagizo ya mpenzi wa boss wao bwana Onesmus.

Pichani ni muanzilishi na mzalishaji mkuu wa kipindi cha vichekesho bibie Gladness Kifaluka.

Video ni muigizaji mkongwe na mtayarishaji nguli wa filamu nchini bwana Deogratius Shija ‘Shija’ akithibitisha tuhuma za rushwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini.

Ni yuleyule ripota kutokea hapa JF, mwenye chanzo chake nyeti…

Nifah.
Ndio maana tamthilia zinazoonyeshwa huko zote mbaya.
 
Wabongo wakikuotea yaani hadi usemee!!
Tukilipata la kukunyoosha ni hadi upepo upite, lazima uteseke kwanza.

Ila katika hili kiwanda cha filamu bongo kimeoza.
Baada ya kutoa taarifa hii nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na jinsi hali ilivyo mbaya na zaidi Azam TV nao kuangaziwa Wakurugenzi wa huko.
 
Ila madam una kipaji cha uandishi
Fanya fanya utupige kwenye kwenye niffa App
Kama dada yetu yule
Asante mwaya, nashukuru.

Tatizo nikisema nifanye hivyo mtaniunga mkono kweli kwenye kunipa maokoto? Lols

Na sasa hivi ndio nina maumbea mazito ya kutikisa nchi! Hayo maubuyu hadi dada yetu yule hana.
 
Kama hicho kipindi cha kitimtim kina uzuri gani?
Ujinga mtupu na huyo Pili wala kuigiza hajui!

Nilikuwa najiuliza sana alikuwa anapata wapi pesa za kumiliki na kuendesha kipindi kama kile? Hili sakata lilipoibuka ndio nimepata majibu.
We acha tu!
Script zao mbayaaa hawajui kuigiza. Yaani ni kichefu chefu. Kazi kubadilisha masebule tu no action.
Mara 200 maigizo ya zamani ya ITV kuliko hizi aibu za siku hizi.
 
Tutakuunga sisi wabongo kwa umbea bora utunyime kula
Na video za connnection tupo tayari kulipia🤣
Ngoja nitaangalia cha kufanya.

Ila, natamani uongozi wa JF kupitia Mkurugenzi wake Maxence Melo wangeleta huduma ya subscription au ile kutuma gift kama instagram na kule Twitter (X)

Lakini mchakato uwe wa hiyari, na anayetuma wala anayetumiwa wasijuane maana hili ni jukwaa huru.
Wao JF waweke namna nzuri ya kunufaika na hilo pia.

Hii sio kwangu, ni kwa members wote watakaoanzisha thread na wasomaji wakivutiwa wakiamua kuwachangia kuwepo na namna rafiki wezeshi.
 
Tamthiliya inakaa zaidi ya mwaka, miaka miwili, au zaidi.

Unaona kabisa hii ilipaswa iishe zamani, haina muunganiko wa kimaudhui kuendelea kuruka hewani ila wana-force.

Wanadhoofisha tasnia. Kumbe kuna watu wamegeuza mradi!
 
Wakuu, kama bado hukuwa na taarifa ya kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi wa Maisha Magic Bongo ndani ya DSTV Barbara Kambogi na msaidizi wake bwana Onesmus Ndarite, tafadhali pitia hapa

Leo tutaangazia ripoti iliyotumwa Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa filamu nchini bwana Isike Samweli kwa undani.

Tofauti na tuhuma za rushwa zenye ushahidi alizotuma makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini, bwana Isike hakuziacha nyuma tuhuma za mapenzi kugubika katika uongozi wa juu wa DSTV na waandaaji, watayarishaji, wazalishaji na hata waigizaji ili kurahisishiwa kupokelewa na kupewa nafasi kwa kazi zao kuonekana DSTV kupitia kitengo cha tamthilia hizo za Kiswahili.

Bwana Isike alituma ushahidi usio na chembe kuhusiana na mahusiano ya kimapenzi baina ya Mkurugenzi msaidizi bwana Onesmus Ndarite na mzalishaji mkuu na mwanzilishi wa kipindi cha vichekesho, Kitimtim bibie Gladnes Kifaluka almaarufu Pili.

Mapenzi yaliponoga bwana Onesmus akageuka sehemu ya kipindi hicho, na kwa kutumia mamlaka hayo akawaondosha katika kipindi hicho waigizaji wakuu wawili Dullvani ‘Da Zuu’ pamoja na mpenzi wake katika maigizo hayo Masantula.

Waigizaji hao waliondoshwa kwa amri kutoka kwa bwana Onesmus aliyejitwalia madaraka ndani ya kipindi hicho cha vichekesho baada ya kuomba waongezewe maslahi kwa kuwa kipindi hicho kilipata kukubalika kati ya watazamaji walio wengi nao umaarufu wao kuongezeka.

Hivi ninavyoandika hapa waigizaji hao wawili sio sehemu tena ya maigizo hayo ya vichekesho na ni kwa wao kuomba stahiki zao za nyongeza katika maslahi.

Kupitia madaraka aliyokuwa nayo ndani ya kitengo hicho cha tamthilia za Kiswahili ndani ya DSTV, bwana Onesmus alitumia nafasi hiyo kukipa muda zaidi kipindi hicho cha mahabuba wake Gladnes Kifaluka kuliko ambavyo kilistahili kutokana na ubora wake.

Mpaka sasa kipindi hicho kingalipo, japo msisimko umepungua baada ya waigizaji hao viongozi kuondoshwa kwa maagizo ya mpenzi wa boss wao bwana Onesmus.

Pichani ni muanzilishi na mzalishaji mkuu wa kipindi cha vichekesho bibie Gladness Kifaluka.

Video ni muigizaji mkongwe na mtayarishaji nguli wa filamu nchini bwana Deogratius Shija ‘Shija’ akithibitisha tuhuma za rushwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini.

Ni yuleyule ripota kutokea hapa JF, mwenye chanzo chake nyeti…

Nifah.
Vita ya maslahi na mambo ya ngono haijawahi wacha watu salama!
 
We acha tu!
Script zao mbayaaa hawajui kuigiza. Yaani ni kichefu chefu. Kazi kubadilisha masebule tu no action.
Mara 200 maigizo ya zamani ya ITV kuliko hizi aibu za siku hizi.
Bado najiuliza Joti na Mwanatumu yake ina karibu na pengine kuzidi miaka 10 kuna namna gani?

Maana hadi waigizaji wakuu mule bwana Jengua na Mama Abdul (wapumzike kwa amani) walishatutoka hadi tumesahau lakini Mwanatumu bado ipo tu!
 
Ngoja nitaangalia cha kufanya.

Ila, natamani uongozi wa JF kupitia Mkurugenzi wake Maxence Melo wangeleta huduma ya subscription au ile kutuma gift kama instagram na kule Twitter (X)

Lakini mchakato uwe wa hiyari, na anayetuma wala anayetumiwa wasijuane maana hili ni jukwaa huru.
Wao JF waweke namna nzuri ya kunufaika na hilo pia.

Hii sio kwangu, ni kwa members wote watakaoanzisha thread na wasomaji wakivutiwa wakiamua kuwachangia kuwepo na namna rafiki wezeshi.
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom