SoC03 Mapungufu na mapendekezo usafiri wa Mabasi yaendayo kasi(UDART) nchini Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Saint Anne

JF-Expert Member
Aug 19, 2018
73,801
225,571
Mapungufu na mapendekezo usafiri wa Mabasi yaendayo kasi(UDART) nchini Tanzania

Heshima zenu wote Wakuu,

UTANGULIZI

Binafsi nikiwa mmoja kati ya wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo kasi, ningependa kupongeza juhudi zilizofanywa na serikali katika kubuni mradi wa mabasi yaendayo kasi, hivyo kurahisisha changamoto ya foleni ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Bandiko langu nitazungumzia jiji la Dar es Salaam lakini miaka ya mbeleni linaweza kutumika pia kuboresha Mikoa mingine ambayo itafikiwa na huu mradi wa mabasi yaendayo kasi almaarufu kama mwendokasi.

PONGEZI

• Kwanza kabisa, ningependa kupongeza jitihada zilizofanywa katika kuratibu mradi, hadi leo hii unafanya kazi na una mabasi mengi ya kutosha hivyo kuwezesha uharaka wa abiria kufika mapema waendako.

• Pia, ningependa kupongeza juhudi katika uajiri wa madereva wa haya mabasi. Madereva wengi wanaofanya kazi katika haya mabasi, asilimia kubwa wanaendesha yale magari kwa weledi na kwa tahadhari ya hali ya juu. Tofauti kabisa na madereva wa magari mengine, licha ya kwamba hakuna changamoto sana katika njia hizi za mwendokasi, lakini pia madereva wapo makini sana.

CHANGAMOTO NA NJIA ZA KUTATUA CHANGAMOTO

Yafuatayo ni mapungufu ninayoyaona katika mradi huu na hatua ninazopendekeza zichukuliwe ili kuboresha;-

*Uzembe katika kutoa na kuleta magari kwa wakati hasa wakati wa jioni
- Nitolee mfano Mzunguko wa Gerezani -Mbezi, Kivukoni Mbezi, Kimara- Mbezi.
Sote tunajua, nyakati za jioni abiria wanaorudi Mbezi ni wengi sana ukilinganisha na wanaotoka Mbezi kwenda maeneo mengine lakini inachukua muda mrefu sana kutoka gari moja hadi nyingine.

Abiria wanatumia muda mwingi kusubiri gari, wengine waliokosa siti huamua kusimama tu ili wawahi, lakini cha ajabu gari hilohilo lililoenea watu hadi wa kusimama, haliondoki pale kwa wakati, linasubiri abiria wengine pia wa kusimama ambao kwa wakati huo wanakuwa hawajafika bado kituoni.

Hii ni kero kwa abiria walioamua kusimama maana muda mrefu unapotea na wakati vituo vya mbele kunakuwa na abiria wengi sana wanasubiri kupanda.

Hii changamoto ya kuchelewa kuletwa gari hupelekea pia watu kuleta vurugu mara tu gari linapofika, mwisho wa siku gari linaondoka kabla watu hawajapanda. Siungi mkono vurugu, lakini endapo magari yangeletwa kwa wakati basi hii changamoto isingekuwepo.

Ikumbukwe kuwa kuna abiria walishasimama ndani ya gari na wanasubiri kuondoka. Sasa watu wengine wamesimama wanasubiri gari la siti lije, ila gari lililojaa tayari linasubiri watu zaidi wasimame na watu wenyewe hawapo hapo kwa muda huo.

Suluhisho
Ningependa kushauri walengwa kwamba, waondoe magari na kuleta kwa wakati ili kuepuka haya yote. Magari mengi yapelekwe sehemu yenye uhitaji. Mfano wakati wa jioni magari yanapaswa kupelekwa kwa wingi gerezani na kivukoni ili kuepuka kadhia zote za vurugu na watu kugombana.

Pia, gari ikishaenea wajitahidi kuondoka kwa wakati kwani abiria wengine hupanda vituo vya mbele.

*Utaratibu mbovu hasa wakati wa kukata tiketi
- Hili nitaliongelea hasa stendi kubwa ya Mbezi na gerezani na Kivukoni kwa kiasi chake.

Kuna madirisha kadhaa kwa ajili ya kukata tiketi lakini utakuta mkata tiketi yupo mmoja tu (Hili tatizo lipo pale Mbezi stand). Abiria wote wanajazana hapo na muda huo gari linaweza kuwa limeshafika ila katika kukata tiketi, ubaha wa wahudumu wakata tiketi unapelekea abiria wanacheleweshwa sana na gari linaondoka.

Kiuhalisia, kila dirisha linapaswa kuwa na mtu. Hali hii inapelekea abiria kuchoka sana maana zoezi la kukata tiketi ni foleni, kusubiri gari ni foleni nyingine. Kupanda gari ni foleni na gari linasubiriwa kwa muda mrefu..Hata kuondoka baadhi ya magari huwa ni foleni pia.

Suluhisho
Rai yangu kwa wasimamiaji, nina mawazo mawili ambayo nadhani yatatatua hili tatizo la sehemu hii ili kupunguza foleni;

*Kwanza; vijana wengi sana wapo mtaani wamesoma masomo ya fedha na wanaweza kufanya hii kazi vizuri.
Kama Kuna uhaba basi ajirini vijana hawa.Hii itasaidia pia kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira.

*Pili; uwekwe mfumo wa kadi kama ulivyo mfumo wa vivuko vya maji kwenda na kurudi Kigamboni. Kadi inaokoa muda, tofauti na tiketi ambazo zinapoteza muda mrefu.

*Kuna usimamizi mbovu pia kwa wakata tiketi hasa pale magari yanapokuwa yanachelewa kufika na umati wa watu kuwa mkubwa sana.

- Abiria huamua kuvuruga foleni hivyo wanapata shida wale wasiokuwa na vurugu. Walinzi na wachana tiketi hawafanyi jitihada zozote kuzuia hili na matokeo yake huruhusu gari kuondoka bila abiria na wakati watu walikaa muda mrefu sana wakisubiri kupanda. Hii changamoto imepelekea baadhi ya abiria na wachana tiketi kuingia makubaliano ya kupeana nafasi kinyemela bila kupanga foleni.Hii hali inachochea rushwa.

Suluhisho;
Rai yangu katika hili,

~ Uwekwe ulinzi imara utakaoweza kusimamia hili vizuri.

~ Vijana wengi wakakamavu wa jkt wapo mtaani,waajirini hao.

*Pia, baadhi ya hawa wachana tiketi hasa pale Kituo cha Kimara, wana lugha mbaya kwa abiria, hasa abiria wasio wazoefu wa kutumia kile kituo siku za Jumapili.

Wasimamizi wajitahidi kufanya maboresho katika haya ili kuweza kufanya huduma kuwa bora zaidi.

Hitimisho

Mwisho kabisa napenda kutoa maoni kuhusu kuongeza muda wa mabasi kusafiri kama ifuatavyo;

1) Usiku inapofika saa tatu usiku, mabasi huwa mwisho wa kusafiri wakati bado kuna abiria wengi sana wapo kituoni wanasubiri kusafiri.

2) Kama haiwezekani kuongeza muda wa mabasi kusafiri basi serikali iangalie uwezekano wa kuweka muwekezaji anayekidhi vigezo, atakayeweza kuingiza mabasi yatakayosaidia kutoa huduma, na hili pia litapelekea ushindani na kupelekea ubora wa huduma.

Karibuni wadau kwa maoni.
 
Kwa mara ya kwanza jana usiku nimeona mwendokasi zinaletwa kwa wakati pale kivukoni.
Inatoka moja,inakuja nyingine muda huohuo.

Kumbe inawezekana.
 
Jioni kwa kiasi kikubwa tatizo limerekebishwa
Kasheshe ni asubuhi na usimamizi mbovu wa walinzi Hasa pale Mbezi.

Wale walinzi hawafai kuwa kazini.

Na hili suala la tiketi limekuwa tatizo kubwa jamani
Utaratibu wa tiketi ni mbovu mno.,wahudumu wachache
Dirisha linafunguliwa moja wakati huo Kuna mamia ya watu wanasubiri tiketi.

Pia hizi tiketi ujanja ni mwingi,Kuna hela zunapigwa hapo nyingi tu.
Suluhisho ni kuweka Kadi kama ilivyo kwenye Vivuko baharini.
 
Hivi huwa najiuliza,
Mamlaka husika hazioni uzembe unaoendelea kituo Cha Mbezi mwisho Hasa kwa upande wa tiketi.

Kundi la watu lililopo Mbezi mwisho, halafu wakata tiketi wanafungua dirisha moja!

Mwisho wa siku wanakuja kutoa kauli chafu kwa abiria na wakati makosa ni yao kutokufungua dirisha zote.

Wale wakata tiketi wa Mbezi kwa upumbavu wao wanachelewesha wanafunzi na watu wazima kupata huduma,kifuatacho ni kuchelewa.
Hawastahili hata kuwa kazini pale..wawekwe watu wenye uwezo wa kufanya kazi aisee hii nchi Ina vijana wengi sana hawana ajira.
 
Mapungufu na mapendekezo usafiri wa Mabasi yaendayo kasi(UDART) nchini Tanzania.

Heshima zenu wote Wakuu,

UTANGULIZI

Binafsi nikiwa mmoja kati ya wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo kasi ,
Ningependa kupongeza juhudi zilizofanywa na serikali katika kubuni mradi wa mabasi yaendayo kasi,hivyo kurahisisha changamoto ya foleni ndani ya jiji la Dar es salaam.

Bandiko langu nitazungumzia jiji la Dar es salaam lakini miaka ya mbeleni linaweza kutumika pia kuboresha Mikoa mingine ambayo itafikiwa na huu mradi wa mabasi yaendayo kasi almaarufu kama mwendokasi.

PONGEZI

•Kwanza kabisa,ningependa kupongeza jitihada zilizofanywa katika kuratibu mradi,hadi leo hii unafanya kazi na una mabasi mengi ya kutosha hivyo kuwezesha uharaka wa abiria kufika mapema waendako.

•Pia ,ningependa kupongeza juhudi katika uajiri wa madereva wa haya mabasi.
Madereva wengi wanaofanya kazi katika haya mabasi, asilimia kubwa wanaendesha yale magari kwa weledi na kwa tahadhari ya hali ya juu,,,tofauti kabisa na madereva wa magari mengine,licha ya kwamba hakuna changamoto sana katika njia hizi za mwendokasi,lakini pia madereva wapo makini sana.

CHANGAMOTO NA NJIA ZA KUTATUA CHANGAMOTO.

Yafuatayo ni mapungufu ninayoyaona katika mradi huu na hatua ninazopendekeza zichukuliwe ili kuboresha;-

*Uzembe katika kutoa na kuleta magari kwa wakati hasa wakati wa jioni.

-Nitolee mfano Mzunguko wa Gerezani -Mbezi,Kivukoni Mbezi,Kimara- Mbezi.
Sote tunajua ,nyakati za jioni abiria wanaorudi Mbezi ni wengi sana ukilinganisha na wanaotoka Mbezi kwenda maeneo mengine.
Lakini inachukua muda mrefu sana kutoka gari moja hadi nyingine.

Abiria wanatumia muda mwingi kusubiri gari, wengine waliokosa siti huamua kusimama tu ili wawahi , lakini cha ajabu gari hilohilo lililoenea watu hadi wa kusimama,haliondoki pale kwa wakati, linasubiri abiria wengine pia wa kusimama ambao kwa wakati huo wanakuwa hawajafika bado kituoni.

Hii ni kero kwa abiria walioamua kusimama maana muda mrefu unapotea na wakati vituo vya mbele kunakuwa na abiria wengi sana wanasubiri kupanda.

Hii changamoto ya kuchelewa kuletwa gari hupelekea pia watu kuleta vurugu mara tu gari linapofika, mwisho wa siku gari linaondoka kabla watu hawajapanda.
Siungi mkono vurugu,lakini endapo magari yangeletwa kwa wakati basi hii changamoto isingekuwepo.

Ikumbukwe kuwa kuna abiria walishasimama ndani ya gari na wanasubiri kuondoka
Sasa watu wengine wamesimama wanasubiri gari la siti lije,ila gari lililojaa tayari linasubiri watu zaidi wasimame na watu wenyewe hawapo hapo kwa muda huo.

Suluhisho ;
Ningependa kushauri walengwa kwamba,waondoe magari na kuleta kwa wakati ili kuepuka haya yote.
Magari mengi yapelekwe sehemu yenye uhitaji.
Mfano wakati wa jioni magari yanapaswa kupelekwa kwa wingi gerezani na kivukoni ili kuepuka kadhia zote za vurugu na watu kugombana.

Pia,gari ikishaenea wajitahidi kuondoka kwa wakati kwani abiria wengine hupanda vituo vya mbele.

*Utaratibu mbovu hasa wakati wa kukata tiketi.

-Hili nitaliongelea hasa Stendi kubwa ya Mbezi na gerezani na Kivukoni kwa kiasi chake.

Kuna madirisha kadhaa kwa ajili ya kukata tiketi lakini utakuta mkata tiketi yupo mmoja tu !(Hili tatizo lipo pale Mbezi stand)
Abiria wote wanajazana hapo na muda huo gari linaweza kuwa limeshafika ila katika kukata tiketi,ubaha wa wahudumu wakata tiketi unapelekea abiria wanacheleweshwa sana na gari linaondoka.

Kiuhalisia,kila dirisha linapaswa kuwa na mtu.
Hali hii inapelekea abiria kuchoka sana maana zoezi la kukata tiketi ni foleni ,kusubiri gari ni foleni nyingine,Kupanda gari ni foleni na gari linasubiriwa kwa muda mrefu..Hata kuondoka baadhi ya magari huwa ni foleni pia.

Suluhisho;-

Rai yangu kwa wasimamiaji ,Nina mawazo mawili ambayo nadhani yatatatua hili tatizo la sehemu hii ili kupunguza foleni;

*Kwanza;
Vijana wengi sana wapo mtaani wamesoma masomo ya fedha na wanaweza kufanya hii kazi vizuri.
Kama Kuna uhaba basi ajirini vijana hawa.Hii itasaidia pia kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira.

*Pili;
Uwekwe mfumo wa kadi kama ulivyo mfumo wa vivuko vya maji kwenda na kurudi Kigamboni.

Kadi inaokoa muda,tofauti na tiketi ambazo zinapoteza muda mrefu

* Kuna usimamizi mbovu pia kwa wakata tiketi hasa pale magari yanapokuwa yanachelewa kufika na umati wa watu kuwa mkubwa sana.

-Abiria huamua kuvuruga foleni hivyo wanapata shida wale wasiokuwa na vurugu.
Walinzi na wachana tiketi hawafanyi jitihada zozote kuzuia hili na matokeo yake huruhusu gari kuondoka bila abiria na wakati watu walikaa muda mrefu sana wakisubiri kupanda.
Hii changamoto imepelekea baadhi ya abiria na wachana tiketi kuingia makubaliano ya kupeana nafasi kinyemela bila kupanga foleni.Hii hali inachochea rushwa.

Suluhisho;
Rai yangu katika hili,
Uwekwe ulinzi imara utakaoweza kusimamia hili vizuri.

Vijana wengi wakakamavu wa jkt wapo mtaani,waajirini hao.

*Pia, baadhi ya hawa wachana tiketi hasa pale Kituo Cha Kimara,wana lugha mbaya kwa abiria ,Hasa abiria wasio wazoefu wa kutumia kile kituo siku za jumapili.

Wasimamizi wajitahidi kufanya maboresho katika haya ili kuweza kufanya huduma kuwa bora zaidi.

Hitimisho;

Mwisho kabisa
napenda kutoa maoni kuhusu kuongeza muda wa mabasi kusafiri kama ifuatavyo;

1)Usiku inapofika saa tatu usiku, mabasi huwa mwisho wa kusafiri wakati bado kuna abiria wengi sana wapo kituoni wanasubiri kusafiri.

2)Kama haiwezekani kuongeza muda wa mabasi kusafiri basi serikali iangalie uwezekano wa kuweka muwekezaji anayekidhi vigezo, atakayeweza kuingiza mabasi yatakayosaidia kutoa huduma.
Na hili pia litapelekea ushindani na kupelekea ubora wa huduma.

Karibuni wadau kwa maoni.
Tunashukuru kwa Pongezi na ushauri wako pia , kwa sasa juhudi za maksudi zinafanyika kuhakikisha usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka unakuwa wa uhakika na wakuaminika kwa wakazi wa Dar es Salaam, ikiwemo kurudisha huduma ya kadi janja, sambamba na kuongeza idadi ya Mabasi itakayokidhi mahitaji. Mapendekezo yako yenye tija tumeyapokea asante sana na endelea kutumia usafiri wetu.
 
Kumbe mpo huku!

Aiseee leo nashuhudia abiria akitupiwa nauli na dada mmoja mkata tiketi,na anaanza kutoa maneno ya ukali.
Hii ni haki kweli?

Na huwa inakuwaje madirisha yote yanafungwa,dirisha moja tu au mawili ndio huwa yanatoa huduma?

Ni kwamba wafanyakazi pale Mbezi hawatoshi au ni vipi Mkuu??

Muda mwingine gari hadi inaondoka bila watu,ila watu wamejazana kwenye foleni ya tiketi.

Na pia hizi tiketi wakataji wakazichakachua sana,Hasa vituo vya njiani kama hamjui

Wanawapa watu tiketi ambazo tayari zimeshachanwa.,na Watanzania walio wengi,hata kuhoji hawawezi.

Sasa sijui mnasimamia kitu gani Mkuu,,Huu usafiri uzembe wa wazi ni mwingi mno.

Akhsante Mkuu kwa kupokea ushauri
Na nakutakia utekelezaji mwema,ikiwezekana Anza na huyu dada wa Mbezi aliyemtupia abiria nauli yake.
 
Mwarobaini wa tatizo hili umeshapatikana kwa sasa Kadi janja zimekamilika na mfumo upo tayari tunasubiri mageti yakuingilia yakamilike ndani ya kipindi kifupi yatatua nchini na kufungwa vituoni, suala la kukutana na watu litapungua sana itakuwa system kwa system tu. Kwa kipindi hiki unaweza kupakua programu ya Mwendokasi App kwenye simu janja yako itakurahisishia kukata tiketi ya safari, utakua huna haja ya kupanga foleni mbili yaani foleni ya tiketi na ya kuingia kwenye Basi, kwa msaada zaidi usisite kutupigia mara kwa mara unapopata changamoto kwa namba yetu ya bure 0800110147.
 
Akhsante Mkuu.

Ngoja nidowload hiyo,itanifaa.
 
Hivi huwa najiuliza,
Mamlaka husika hazioni uzembe unaoendelea kituo Cha Mbezi mwisho Hasa kwa upande wa tiketi.

Kundi la watu lililopo Mbezi mwisho, halafu wakata tiketi wanafungua dirisha moja!

Mwisho wa siku wanakuja kutoa kauli chafu kwa abiria na wakati makosa ni yao kutokufungua dirisha zote.

Wale wakata tiketi wa Mbezi kwa upumbavu wao wanachelewesha wanafunzi na watu wazima kupata huduma,kifuatacho ni kuchelewa.
Hawastahili hata kuwa kazini pale..wawekwe watu wenye uwezo wa kufanya kazi aisee hii nchi Ina vijana wengi sana hawana ajira.
Kumbe unakaa mbezi hee
 
Back
Top Bottom