Ndugu watanzania wenzangu!! Tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia jinsi nchi yetu yenye neema zote ambazo taifa lolote linaloweza kuclaim kama limejaaliwa tunazo, jinsi inavyoendeshwa; Huku ikiwaacha wananchi wengi tukiishi katika lindi kuu la umasikini linaloendelea kuwa compounded na
1. Unprecedented power shortage - Ni full kiza, shughuli zinazotegemea umeme hazifanyiki tena kwa uhakika, watu wamekosa kazi kwa kutokana na hilo
2. Bei Za nishati zipo juu, Petroli bei juu, mafuta ya taa bei juu, gesi bei juu, gunia la mkaa ni zaidi ya elfu 35
3. Bei za vyakula zimepanda kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji
4. Wabunge wetu walioteuliwa kutuwakilisha, wamejkalia kuwakilisha vyama vyao na si maslahi ya taifa, hoja inayolenga kumkomboa mtanzania ikitolewa na mtu ambaye si chama cha waliowengi bungeni kinachofuata ni kuzomewa na kejeli, huku watanzania tunaendelea kuumia na hali ngumu ya maisha.
Jamani ndugu watanzania wenzangu, tutaendelea kunung'unika mpaka lini, ni lazima tutangaze mwisho wa hii hali kwa faida yetu na watoto wetu na vizazi vijavyo.
Je ni nini kifanyike ndugu watanzania wenzangu???. Ninaomba tujadiliane mpaka tupate Muafaka. EWakati ni huu.
Kuna mwanafalsafa alisema, Mwenye kosa si anayefanya uovu, bali ni yule anayekaa kimya wakati uovu unafanyika!!