Mapinduzi yaja Tanzania

Mapinduzi yaja Tanzania

Habari ndugu zangu wana JF!Leo naomba kwa pamoja tujadili juu ya mstakabari wa taifa letu hususani katika suala la amani na uwepo wa CCM,...Viongozi wa nchi mbalimbali barani Afrika na vyama vyao mashuhuri wameangushwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukosekani wa haki na maendeleo kwa wananchi pamoja na kutotimizwa kwa ahadi kedekede walizo ahidiwa,Angalia pale Libya,Tunisia,Misri,syria,Ivory coast,na kwingineko ambako waafrika waliamua kuchukua jukumu la kuirudisha amani yao iliyopotea,kila mtu ameshuhudia madhara yaliyotokana na uzembe tu pamoja na kiburi cha viongozi.Ikumbukwe tu kwamba viongozi waliopinduliwa walieshimika saana nchini mwao na katika bara la Afrika,mfano:Gaddafi aliaminika kuwa mkombozi wa Libya,haya leo yuko wapi?...Ikiwa mti mbichi watendewa hivi vipi kwa mti mkavu?....Je! CCM inaamini itatawala milele?kama sivyo ni nini Je CCM imejifunza?...Nawasilisha.
 
huku bongo inaezekana kuendeleza mfumo huu wa kiutawala kwa kakitambo kidogo kwani viongozi washawasoma watanzania na kuwaona ni mabwege wa kulaghaiwa hata kwa sahani ya wali wakainga kingi(reffer kwa yaliyotokea juzi kwa wanafunzi wa udom wakati wanafungua blog ya ccm, buku tano tano walizopewa juzi watu kwa kuja pale jangwani na sasa sanakuja na benki ya vijana na wakulima)
ninachojua mimi tatizo ni njaa njaa zetu tusitegemee mabadiliko ya hivi karibuni kwa watanzania hawa maybe baadae sana
 
Serikali yetu imetudharau kiasi cha kutosha, imetupuza kiasi cha kutosha, imetupeleka utumwani.....................Sasa sisi tumekataa unyoge wetu..............Tuitoe madarakani.............

Nakuunga mkono ndg'
 
Unapozungumzia kupanda kwa uchumi ukatoa takwimu za world bank na IMF na kupungua kwa inflation n.k that is merely academic exercise! Watanzania wao kupanda kwa uchumi ni kuboreka na unafuu kwe huduma za afya! shule usafiri, kupatikana chakula, mishahara ya wafanyakazi kukidhi mahitaji yao! kupatikana maji safi, barabara, kupungua au kwisha kwa magonjwa kama malaria kipindipindu n.k huko ndiko kukua kwa uchumi hizi asilimia sijui 12% sijui 13.5 % hazina maana kama hazi reflect kwenye social services!!
 
Kweli kabisa,yan magamba wana tokwa na jasho ile mbaya.
 
katika kupata haki lazima kujitoa muhanga sababu kutakuwa na kila aina ya vikwazo kama wanavyopata wapinzani wa leo so just a challanges of going to the salvation*victory *
 
["To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why? When the majorities don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools (wapumbavu). Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools (wapumbavu). So Tanzanians would be fools (wapumbavu), ****** (mazuzu), if they continue to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?"].

Per MWALIMU NYERERE [in Shivji, Issa: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa, 2000]: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/332793-mdahalo-m4c-hatima-ni-mageuzi-au-mapinduzi.html
 
sijawahi kuona mtu asiye na aibu kama jk. hivi kila siku unaaga unakwenda MAREKANI,na anatumia bilions of tshs for nothing halafu wazungu wamemchoka.siku moja watamtuma office attendant kwenda kumpokea kwani hawana muda wa kupoteza tena.
 
kuna watu wanatukwaza kufikia malengo yetu hao si wengine bali wanao kubali kushonewa magauni na kupewa khanga halafu wanatoa shahada zao kwa ccm.lakini mwisho wao umekaribia
 
nasubiri kwa hamu hiyo siku!!View attachment 34265

Niliwahi kumwambia mtu kuwa lingetokea hili huenda watu wengi wangepata ahueni sana. Lakini alinijibu kuwa, jue JK ni mume na baba wa watu pia ambao nao watapata uchungu. Nikajiuliza, kumbe kina Mwangosi na wengine wengine sio watu vile
 
Nguvu ya mabadiliko Tanzania inakuja kwa kasi ya ajabu. Hakuna kinachoweza kuzuia nguvu ya umma.

Kila sehemu ya maisha wananchi wa kada zote wanaonyesha kutofurahia serikali iliyopo madarakani. Ugumu wa maisha na kushamiri kwa rushwa ni kero kubwa kwa Mtanzania wa kawaida.

Pamoja na hayo yote wengi wao bado wameipigia kura CCM. You wonder.
 
Tuanze kwanza na kutengeneza vyama ( chama) vya siasa vyenye uzalendo na demokrasia ya dhati, vyenye nia ya kweli ya kumkomboa mtanzania..!! Tukifanya hivyo kweli tutafanikiwa lakini kwa maigizo yanayoendelea ni ngumu sana kutafunika...
 
Tatizo kwa social media mko wachache sana kuliko hao ambao wameirudisha tena CCM madarakani
 
Back
Top Bottom