SoC04 Mapinduzi ya Teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence) katika kilimo nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

lyren

New Member
May 21, 2024
1
2
Screenshot-132.png
UTANGULIZI
Kuelekea Tanzania tuitakayo,

Sekta ya Kilimo nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kukuza Uchumi wa nchi, kupunguza umasikini kwa kuboresha maisha ya watu. Sekta hii inachangia kwa 23% katika pato la Taifa, na ndiyo sekta iliyoajiri watanzania wengi takribani 65.5% ukilinganisha na sekta nyingine nchini.

Sekta ya kilimo ndiyo sekta inayozitegemeza sekta nyingine za kiuchumi kama vile sekta ya usafirishaji, sekta ya viwanda na sekta nyingine. Pamoja na jitihada kubwa zilizofanya na zinazofanywa na serikali yetu kupitia Wizara ya Kilimo na wadau wengine wa maendeleo katika kilimo, bado kuna changamoto katika sekta ya kilimo nchini.

Zipo changamoto za masoko, uzalishaji duni, teknolojia ya kiwango cha chini, huduma hafifu za ugani ambazo kwa pamoja zinakwamisha kufikia Malengo na matarjio ya Serikali na wakulima katika kilimo.

Changamoto hizi zinatokana na njia,mbinu tunazotumia, maarifa kidogo tuliyonayo kuhusu kilimo pia mitaji tunayowekeza kwenye kilimo ni ya kiwango cha chini.

Teknolojia ya akili mnemba, huu ni uwezo mkubwa wa kufanya kazi au mambo ambao unawekwa kwenye mashine hasa mifumo ya kompyuta kutoka kwa mwanadamu na hivyo kufanya mifumo hii ifanya kazi kama binadamu, ikihusisha kujifunza, kukusanya taarifa, kufikiri na kufanya maamuzi. Teknolojia hii ya akili bandia huziwezesha mashine kutekeleza kazi ambazo kawaida zinahitaji kufanywa na binadamu tena kwa ufanisi mkubwa.

Mfano mzuri ni teknolojia ya mtandao wa vitu (Internet of things ,IoT);

Huu ni muunganiko wa mtandao wa vifaa vilivyounganishwa na sensor, programu, ambazo huwezesha kukusanya na kubadilishana taarifa kupitia mtandao. Vifaa hivi vinaweza kutofautiana kama vifaa vya nyumbani, magari hadi mashine za viwanda na vifaa vya kilimo.

Endapo taifa letu litakubali kuyapokea na kutumia mapinduzi haya ya teknolojia ya akili mnemba katika kilimo, sekta ambayo inagusa Maisha ya kila mwananchi, ni dhahiri kuwa taifa letu litakuwa limekubali kuondoa changamoto zilizopo na hivyo kuwapatia watanzania walio wengi Maisha bora na hata kuongezeka kwa ukuaji wa Uchumi na maendeleo.

MATARAJIO LA ANDIKO HILI
(i) Kuongeza Tija na Uzalishaji
Mifumo hii inao uwezo wa kufanya Uchambuzi wa Takwimu: AI inaweza kutumika kuchambua takwimu za hali ya hewa, udongo, na mazao ili kutoa miongozo sahihi kwa wakulima. Kwa mfano, mfumo wa AI unaweza kutumia taarifa ya hali ya hewa na udongo ili kutoa tahadhari kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kutoa mapendekezo juu ya mbinu bora za kilimo.

Kudhibiti na Kusimamia Mifumo ya Umwagiliaji: IoT inaweza kutumika kuunganisha vitu kama vile matanki ya maji, mabomba, na sensorer za unyevu katika shamba. Hii inaruhusu wakulima kudhibiti na kusimamia umwagiliaji kwa njia ya kiotomatiki hata pasipo mkulima kuhangaika na kwa usahihi zaidi. Kwa mfano, mfumo wa IoT unaweza kufuatilia unyevu wa udongo na kutoa maji kwa kiwango kinachohitajika, hivyo kuokoa maji na kuboresha tija.

Uchunguzi wa Afya ya Mazao: AI inaweza kutumika kutambua magonjwa na wadudu kwenye mazao kwa kutumia picha na taarifa nyingine. Kwa mfano, mfumo wa AI unaweza kutumia picha za mazao ili kutambua dalili za magonjwa na kutoa mapendekezo ya matibabu. Hii inasaidia kugundua mapema na kudhibiti magonjwa, hivyo kupelekea ongezeko la uzalishaji.

(ii) Upatikanaji wa masoko
Utambuzi wa Mahitaji ya Soko: AI inaweza kutumika kuchambua taarifa za masoko, tabia za watumiaji, na mwenendo wa mahitaji. Hii inaweza kusaidia wakulima kuelewa vizuri mahitaji ya soko na kuzalisha mazao yanayohitajika zaidi. Kwa mfano, mfumo wa AI unaweza kutumia taarifa za mauzo na mitandao ya kijamii kubaini mwelekeo wa mahitaji ya watumiaji.

Uboreshaji wa Mnyororo wa Ugavi: Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inaweza kuchambua mnyororo wa ugavi wa mazao kutoka shambani hadi sokoni. Hii inasaidia kubaini maeneo yanayoweza kuboreshwa kwa ufanisi zaidi. Kwa mfano, mfumo wa AI unaweza kutoa mapendekezo ya njia bora za usafirishaji na kuhakikisha kuwa mchakato wa ugavi unakuwa wa haraka na wa ufanisi.

(iii) Ushiriki wa Vijana na wanawake katika Kilimo
Tekonolojia ya AI inaouwezo wa kutoa elimu na ushauri kwa vijana na wanawake kuhusu fursa zilizopo katika kilimo na jinsi wanavyoweza kuchangia. Pia kwa Kupunguza Kazi za Mikono kutafanya kilimo kiwe cha kuvutia zaidi kwa vijana na wanawake. Kwa mfano, matumizi ya roboti au drones katika shughuli za shamba.

(iii) Kupunguza gharama za kilimo
Kupunguza Gharama za Ufuatiliaji na Uchambuzi: AI inaweza kuchambua taarifa kutoka kwa sensorer za IoT na kutoa taarifa za kina kuhusu hali ya mazao na udhibiti wa magonjwa na wadudu. Hii inaweza kusaidia kugundua mapema matatizo na kuchukua hatua stahiki, badala ya kutegemea ufuatiliaji wa kawaida ambao unaweza kuwa ghali zaidi.

Kupunguza Hasara za Mazao: Kutumia AI na IoT, wakulima wanaweza kugundua mapema dalili za magonjwa au matatizo ya mazao na kuchukua hatua za kuzuia. Hii inaweza kupunguza hasara za mazao na hivyo kuongeza mapato yao na kupunguza mzigo kwa serikali katika kusaidia wakulima walioathiriwa.

Matumizi ya pembejeo bora za kilimo
Matumizi ya teknolojia ya Akili mnemba na IoT katika kilimo hayatahusisha wakulima tu, wanahitajika wataalamu wa fani mbalimbali ambao watatumia maarifa yao katika sekta ya kilimo kama wafuatao: Wahandisi wa kilimo, Wataalamu wa taarifa (Data analysts), Developer Watafiti, Watu watakaohusika na mchakato wa kuongeza thamani katika mazao ya kilimo na Watu wa masoko.

Hivyo program hii haitoi fursa kwa wakulima tu kufanikiwa lakini inatoa fursa ya ajira kwa watu wenye taaluma tofauti na kilimo pia. Hii itasaidia Serikali kupunguza idadi ya watu wasio na ajira.

WATEKELEZAJI WA MRADI
Program hii inaweza kutekelezwa na watanzania wote kwa kushirikiana na mamlaka /taasisi zifuatazo;
Mamlaka za Serikali na taasisi zisizo za kiserikali.
Taasisi za Utafiti na Elimu;
Makampuni ya Teknolojia
Food and Agriculture Organization (FAO)

HITIMISHO
Proram hii inaweza kutekelezwa kwa miaka mitano, kumi, hata ishirini kwa awamu tofauti katika maeneo tofauti kote nchini, endapo serikali itaadhimia kwa dhati kutekeleza jambo hili mhimu. Nitoe wito kwa watanzania wote, wadau mbalimbali, taasisi za kifedha na asasi za kiraia na Serikali yote kuona umhimu wa mradi huu na kusaidia kimawazo au rasilimali fedha ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali yetu kupitia wizara ya kilimo kuelekea Tanzania tuitakayo.
 
Changamoto hizi zinatokana na njia,mbinu tunazotumia, maarifa kidogo tuliyonayo kuhusu kilimo pia mitaji tunayowekeza kwenye kilimo ni ya kiwango cha chini.
Tusaidie, tuongeze uzalishaji na ubora hatimaye masoko ya bidhaa tutatue changamoto.
. Pia kwa Kupunguza Kazi za Mikono kutafanya kilimo kiwe cha kuvutia zaidi kwa vijana na wanawake. Kwa mfano, matumizi ya roboti au drones katika shughuli za
Swali kadogo hapa, je hata hapa ambapo watu wanalilia kazi na wafanyakazi si gharama bado tunahitaji akili mnemba na maroboti?

: Wahandisi wa kilimo, Wataalamu wa taarifa (Data analysts), Developer Watafiti, Watu watakaohusika na mchakato wa kuongeza thamani katika mazao ya kilimo na Watu wa masoko.

Hivyo program hii haitoi fursa kwa wakulima tu kufanikiwa lakini inatoa fursa ya ajira kwa watu wenye taaluma tofauti na kilimo pia.Hii itasaidia Serikali kupunguza idadi ya watu wasio na ajir
O oooh? Ahsante, kiufupi imeongeza wigo wa watu kama jukwaa la watu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Ahsante
 
Back
Top Bottom