Thailand
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 262
- 778
1. Kuinua na kuhimiza kilimo cha umwagiliaji.
Hiki ni kitu muhimu kutoka kutegemea mvua za msimu, serikali iweke na kuwezesha UKUAJI WA SEKTA YA KILIMO.
Tanzania tuna fursa ya maeneo bora ambayo sasa yametelekezwa kama mapori, yana udongo wa rutuba vyanzo vya maji ya mito na underground. Kinachotakiwa ni serikali kuwezesha channel ya upatikanaji wa maji hayo huko mashambani ili kilimo kiweze kuwa ni non stop in Tanzania.
Tanzania ina kopa pesa nyingi nje lakini pesa yote hiyo maranyingi inakwenda kwenye matumizi yanayochochea mwishoni mfumuko wa bei na hivyo ongezeko la gharama za maisha unakuwa mkubwa, lakini kama serikali ingejitaidi kununua hata tractors na mashine kama hizi za kilimo.
Vifaa hivyo ndo vingekuwa vipau mbele vyetu kila tunapopata pesa za mikopo kutoka nje. Kwa maana katika Uchumi kama mkopo unaupeleka kwenye uzaliahaji ina maana kiuchumi haina shida kwa sababu hivyo utakavyozalisha hapo kwenye kilimo vitasaidia nchi kujikwamua kutoka utegemezi wa nchi tajiri.
Mfano wa hivi karibuni, masokoni bei ya vyakula inazidi kupanda na endapo kama hakutakuwa na serious measure wananchi wanaenda kuteseka sana kwa kukosa chakula, ukosefu wa chakula hauumizi wapinzani pekee hata wana chama wa Ccm wanapitia kipindi hichohicho. Maumivu yakiendelea hivi kwa wananchi hata serikali iliko madarakani haitakuwa na amani maana kila kona ni kilio cha njaa kima ilivyo somalia inavyoteseka now.
2. Serikali wezesha upatikaji wa nishati ya umeme kwa urahisi.
Hakuna ndoto ya nchi ya viwanda pasipo UMEME WA UHAKIKA. Fikiria baada ya kutoka kwenye kilimo kikubwa( Agrarian Revolution kama Europe na USA walivyoanza ndo wakaja kwenye Industrial revolution) kama tulivyo ona hapo juu unahitaji umeme wa uhakika ili kuwezesha usindikaji wa bidhaa za kilimo katika ubora unaofaa kwa ajili ya masoko ya kimataifa. Hatuwezi kwenda kimataifa kama nchi, kama umeme wetu ni wa kusua sua kama ilivyo sasa.
Hivyo kwa kuwa bwawa la nyerere limeshakula pesa zetu watanzania, NAKUOMBA SANA SANA MAMA SAMIA PIGA KAMBI HAPO BWAWANI ILI KUONA LINAKAMILIKA KWA WAKATI. Pinga siasa kwenye jambo hilo, umeme sio swala la mwendanzake hilo ni jukumu lako likifanikiwa sifa zitarudi kwako na watanzania wote. Watanzania tunaitaji umeme wa uhakika kwa bei nafuu japo najua kuna shinikizo bei ya umeme kupandishwa juu na kukatika hovyo hovyo, HII INAUWA UCHUMI WA NCHI NA WA WAJASIRIAMALI WADOGO kama vinyozi na mashine za kusaga na viwanda vidogo.
3. ELIMU, ELIMU, ELIMU.
Nchi ya Tanzania inaitaji maabadiliko ya Elimu ya haraka ili kuona nchi inapiga hatua,
Kama nchi haitakiwa kuendelea kulea mifumo mibovu ya elimu kama iliyopo hivi sasa. Mfano haiwezekani nchi ikaruhusu wananchi wake wakawa na mifumo miwili tofauti katika kutoa elimu kwa watoto wake.
Kama taifa inabidi kufuta hiki kitu kinachoitwa shule za English medium na kayumba au Swahili medium.
Napendekeza tuwa na ENGLISH MEDIUM kwa shule zote za serikali na binafsi ili kufuta matabaka yanayozalishwa kwenye elimu yetu na elimu mbovu kwa watoto wanaotoka shule za serikali. Kiswahili libaki kama somo wakati English itamalaki kwenye ufundishaji wa masomo yetu hasa ya sayansi. Nasisitiza English kwa sababu kama nchi bado tunategemea biashara na technology kutoka katika nchi zilizoendelea.
Elimu yetu ya kidato cha sita inaitaji mabadiliko makubwa sana. Haiwezekani mwanafunzi aliyefeli kidato cha nne anakutwa kazini baada ya kusoma certificate na diploma huku aliefaulu na kwenda kidato cha tano na sita hana ujuzi wowote anaorudi nao mtaani.
Ikibidi elimu ya kidato cha tano na sita inaweza badilishwa iwe ni ya practical base, mfano unakuta shule kama ya Bagamoyo Sec ipo pembezoni mwa bahari kwanini elimu ya watoto isiwe either kutengeneza mangalawa, meri, uvuvi baharini, uwekezaji kwa kutengeneza vyombo vya utalii kwenye fukwe.
Nadhani tusaidie elimu yetu iwe inayowasaidia vijana kuona fursa zinazowazunguka kwenye mazingira yenye practical case nyingi sana. Hapo tutakuwa tumetoka kwenye ile elimu ya kikoloni ambayo haisapoti mazingira sasa na mwisho watoto wetu wanapitia wakati mgumu wa ukosefu wa ajira kisa maamuzi ya viongozi wetu.
Kwa leo naomba kuishia hapo karibu kwa mjadala.