SoC01 Mapinduzi ya Kilimo

Stories of Change - 2021 Competition

JOSEPHAT OPONDO

New Member
Sep 18, 2021
1
1
Kilimo ni uti wa mgongo katika nchi nyingi za dunia ya tatu, kwa bahati mbaya sana serekali za nchi zetu hazijaweka mikakati juu ya uwezeshaji wananchi wake katika swala zima la kilimo. Katika hali ya kawaida kilimo namna inavyotajwa kama uti wa mgongo kwa wananchi walio wengi kwa takriban asilimia 70% sivyo inavyopewa kipaombele wala hakuna mikakati ya mda mfupi na mrefu katika secta hii nyeti. Yafuatayo ni changamoto zinazokabili secta ya kilimo hasa kwa nchi zetu za dunia ya tatu

1. Kutegemea kilimo cha mvua. Kutokana na mabadiliko ya hali ya nchi kilimo cha kutegemea mvua hakiwezi kuleta tija kwa jamii.

2.ukosefu wa pembejeo za kutosha. Wakulima wengi wanakosa pembejeo zilizo bora hivyo kushindwa kuzalisha vya kutosha na kujikwamua kiuchumi

3. Ukosefu wa mashamba darasa kwa wakulima. Wengi wa maafisa kilimo wamekuwa ni watu wa ofisini badala kwenda vijijini na kuanzisha mashamba darasi kuwasaidia wananchi kuondokana na kilimo cha mazoea.

4.Kukosekana kwa masoko ya uhakika. Mfano bei ya mahindi kwa takribani miaka mitatu sasa imekuwa chini hivyo kutowanufaisha wakulima kwasababu uzaliashaji umekuwa mkubwa na mahitaji kuwa madogo hivyo kufanya wakulima wengi kuuza mazau yako kwa bei ya chini kwa kiwango kisichowezi kuwakwamua kwenye umaskini

5.kukosekana kwa mfumo wa kuwawezesha wakulima kiuchumi. Wakulima wengi wa nchi zetu ni maskini. Ni ndoto kuendelea katika secta ya kilimo kwa kutegemea kwa kutegemea wakulima wadogo ( small scale)

6. Ubovu wa miundombinu. Mkulima anaweza akalima ila kutokana na ubovu wa miundombinu akashindwa kufikisha mazao yake sokoni kwa wakati na yakamuozea na kupata hasara.

MAPENDEKEZO YA MSINGI YA NAMNA YA KUBORESHA SECTA YA KILIMO.

1. Uanzishwaji wa scheme za umwagiliaji ili kuondokana na utegemezi wa mvua kutokana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa. Kama misri ni jangwa Ila wameweza kutumia vyema maji ya mto Nile kuendesha kilimo, sisi Tanzania wenye mito na maziwa tunaweza kufanya zaidi tukiamua na kuwa na mikakati.

2.urahisi wa upatikanaje wa pembejeo za kilimo na, kwa bei nafuu na bila ukiritimba mwingi. Serekali iwawezeshe wakulima kupata pembejeo za kilimo kwa wakati na kwa gharama nafuu, ikiwezekana kodi zipumbuzwe sana kwenye uzalishaji na uingizwaji wa pembejeo hizo ili kuleta urahisi wa wananchi kuzipata.

3.maafisa ugani na kilimo wawepo kuanzia ngazi za vijiji na wafanye kazi na wakulima. Wakulima wengi hata hawajui jukumu la afisa ugani ni nini kwasababu wengi wamekuwa ni wa kukaa maofisini na sio kuwasaidia wakulima .

4. Serekali kuimarisha soko la ndani na ikiwezekana kutafuta hata soko nje ya nchi ili mazao ya wakulima yasikose masoko na kuingia hasara.

5.Uwezeshaji wa wakulima kiuchimi uimarishwe.kuna benki ya wakulima ila sijui kama hiyo benki inawanufaisha wakulima na kuwawezesha kiuchumi na kwa kiwango gani? Lakini wakulima wengi hasa Tanzania wana vipato duni sana. Hivyo serekali zetu lazima ziangalie namna ya kuwawezesha wakulima.

6. Kuboresha miundombinu ya vijijini. Barabara zetu vijijini kwakweli hazipitiki na inasababisha wakulima wengi kuingia hasara kubwa sana.

Kama nchi lazima pawepo na mikakati ya makusudi kabisa kuwezesha secta ya kilimo na kuimarisha secta ya kilimo kwa ujumla wake.

Kama taifa lazima tujiulize tunahitaji nini kwenye kilimo na kama wadau, viongozi na wakulima tunamikakati hiyo au imekuwa kwenye midomo na majukuani.
nikipata platform ninapenda kuwa kijana atakayefanya mapinduzi katika secta ya kilimo

Asante nawasilisha.
 
Back
Top Bottom