Mapinduzi Cup: Waandishi wa habari za michezo mnatia aibu,pamoja na wale wa Azam media

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,410
36,560
Kwa anayefuatilia michuano ya Mapinduzi Zanzibar atakuwa shahidi wa hili,post match interview kwa makocha,hasa mfano wa yule wa Azam,George Lwandamina anayetumia lugha ya malkia (English),waandishi wanashindwa kumuuliza maswali na hata wakimuuliza unaona kinyaa kabisa ukizingatia inakuwa Live.

Najiuliza mtu kama mwandishi wa habari unashindwa hata kuangalia wanachofanya wenzio kwenye vituo vikubwa vinavyorusha mchezo wa mpira? Nikweli hiyo lugha si yetu ila kwanini hata usijiandae kwa maswali yako mawili au matatu......yaani wanamuuliza maswali Lwandamina mpaka anacheka kwasababu hayaeleweki.Kuna vijana wengi wenye uwezo mzuri sana mtaani wapo,hasa nyie Azam media fanyeni recruitment vizuri,mnatia aibu sana inapotokea mahojiano na asiye mswahili.

Na nyie waandishe acheni uvivu,jifundisheni basi......saizi dunia ni kama kijiji ingieni You tube huko mjifunze.
 
Kiingereza ni lugha ya wenzetu....kuijua vyema inahitaji JITIHADA KUBWA.....

Sasa ndio vijana wenzetu walio wengi...wasiajiriwe?!!

Unashangaa waandishi wa habari mbona hatushangai wanasheria waliosemwa wanamaliza vyuo vikuu huku wakiwa HAWALIJUI YAI VYEMA?!!!
 
Nikweli siyo lugha yetu,ila lazima kila kitu ujifundishe hata kwa kukariri maswali ya msingi,kupata ajira ni suala lingine na kujibidiisha kwa kazi uliyonayo nijambo lingine
 
Kwa nini tusiwe kama Uingereza?
Kocha au mchezaji ukisajiliwa Tanzania lazima ujifunze kiswahili.
England hakuna kocha au mchezaji anayehojiwa kwa lugha yake, lugha ni moja tu, English.
 
Waandishi wengi wa Azam hawajui kiingereza.

Ukitaka kuliamini hilo, tazama na usikilize wanapokua wanawahoji makocha wanaotumia lugha ya kiingereza, yaani unaweza kucheka

Kiingereza ni mziki mnene,unaweza kusikia neno am trying but i can’t reach you.
 
Kwa nini tusiwe kama Uingereza?
Kocha au mchezaji ukisajiliwa Tanzania lazima ujifunze kiswahili.
England hakuna kocha au mchezaji anayehojiwa kwa lugha yake, lugha ni moja tu, English.
kocha wa leeds hajui kingereza hadi leo anatumia mtafasiri wakati wamahojiano
 
Waandishi wengi wa Azam hawajui kiingereza.

Ukitaka kuliamini hilo, tazama na usikilize wanapokua wanawahoji makocha wanaotumia lugha ya kiingereza, yaani unaweza kucheka
Acheni Ulimbukeni nyie pimbi. Kwani mmeambiwa Azam anarusha Matangazo kwa Kiingereza???
Nendeni CNN ya Marekani mtutajie Watangazaji wanaojua Kiswahili basi maaana naona mishipa ya Shingo imewatoka sana.
 
Back
Top Bottom