Yanga SC kuwasomea ' Albadiri ' Waandishi wa Habari za Michezo wanaoiandikia, kuisemea na kuihujumu

Status
Not open for further replies.

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Hivi Klabu inawezaje Kuwatishia Waandishi wa Habari za Michezo hasa kuwataka wawe tu Wanaandika na Wanatangaza Mema (Mazuri) tu ya Yanga SC ila yale mabaya Wawe wanayaficha kwa Umma wa Wanamichezo?

Haya sasa kwa taarifa ( zisizo rasmi bado japo nimezikisikia hivi punde kutoka Clouds FM Kipindi chao cha Michezo cha Hili Game ) kutoka kwa baadhi ya Mashabiki wa Yanga SC waliohojiwa zinasema kwamba leo hii Klabu hii inapanga kuwaombea Dua baya la ' Albadiri ' Waandishi wa Habari za Michezo nchini wanaoichafua Klabu yao hii (hiyo)

Sijui na Mimi Generalist nimejumuishwa humo au nimesahaulika, ila niseme tu nilifanya Maamuzi sahihi ya Kuipenda Simba SC na kuwa Mshabiki Mwandamizi wa Simba SC Timu bora na iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Haya sasa wana Yanga SC nasubiri mmalize Kutosemea hiyo ' Albadiri ' ili mkimaliza tu baadae mniambie Generalist nije na Taarifa ' very exclusive ' ya kuihusu Yanga SC hasa Viongozi wao wa juu Msolla na Mwakalebela kisha nimalizie na Suala la Wachezaji akina Sarpong, Ntibanzonkiza, Mukoko, Kaseke na Niyonzima.

Mmetuchokoza wenyewe tuvumiliane!!!
 
Juzi wamekutana na viongozi wa BMT wakawa wanalalamika wanavyoujumiwa na TFF na waamuzi, BMT walipowaita TFF wakaelezwa maamuzi yote yanatolewa na kamati zake kwa mujibu wa katiba na kanuni.

BMT ikaamua waende wakakae wamalize tofauti zao. Yanga wanasahau mpaka sasa wapo kileleni kwa hisani ya maamuzi mabovu ya waamuzi, pia wanataka serikali iingilie kati ili tufungiwe na fifa maana wameshaona siku zimeenda na hakuna kinachofanyika.

Hayo madeni wanayodaiwa hadi fifa ni nani anawahujumu tena yanazidi kuongezeka maana Ngassa naye anasema anawadai.

Imefika wakati tumpe Eymael tuzo kwa kusema ukweli
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom