Mapigano dhidi yako mwenyewe 💪

Mapigano dhidi yako mwenyewe 💪

Andiko zuri na linaleta uamsho wa nguvu ya mtu ulio ndani yake. ShesRise_1 punguza kuweka Viimoji kwenye nyuzi zinakuwa zinaleta feelings nyingi ambazo zipo mchanganyiko. Kwa ambao tunaelewa baadhi ya emoji zina maanisha nini
 
Vita ya ndani ni ile unajua unapaswa kufanya nini lakini unaogopa watakuonaje.
Kujua unachopaswa kufanya hiyo sio vita kamili hua ni mwanzo tu wa kuenda vitani na kuandaa silaha za kutumia
Vita kamili ni ile kuchukua hatua

Wengi hawana filter ya kujua nini wanahitaji, wanafwata maneno ya viumbe wengine wanaishia kuwa ma zombie tu humu duniani
hili ni mada nyingine kabisa
It's funny but true. Kama unajua wewe ni nani basi vita umeiahinda nusu ila kulifanya lile unalotaka ndo mtihani thabiti
Asante karibu tena
 
Natoa angalizo kwa wale wa unashinda JF full-time
Huu ni kama ushauri tu kwamba hii mada inakuhusu isome yote ili uanze leo kupigana na hiyo tabia isiyopendeza ya kufatilia ni nani anaingia online sa ngapi na anatoka saa ngapi

Sisi wengine kuandika ni moja wapo ya enjoyment 😊

Na hii platform sio kama hizo zingine za kupost makalio au kutafuta attention hapa tulio wengi hatufahamiani

na hii inatupa uhuru wa ku share kujifunza kupiga story na kufurahia maisha kwa mtindo huo

kwa wale wote wanaovutiwa na nyuzi zangu guys nipo in love kwenu 🥰 nawapenda sana😊😊

Twende zetu sasa 🤪👇

Mapigano yapo ya aina nyingi Umewahi kusikia nchi fulani ikiwa vitani?
Watu husema nchi A inapigana na nchi B. Hayo huitwa mapigano

Pia kuna mapigano kati ya watu wawili, mtu A na mtu B, kama vile yanavyotokea ulingoni( mtu anapigwa hata kwa TKO)

Hata wanyama nao hupigana mfano kuku, mbuzi na wengine

Lakini je, umewahi kujiuliza kama inawezekana mtu kupigana dhidi ya yeye mwenyewe?

Jibu ni ndiyo, inawezekana kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe

Haya ni mapigano ambayo hayapiganwi kwa ngumi wala silaha, bali ni mapambano ya ndani ya nafsi

Ni pale unapogundua kuna kitu ndani yako ambacho hakikufanyi kuwa mtu unayetaka kuwa, hivyo unaamua kukikabili

Mfano unaweza kujijua kabisa una tabia fulani kama wivu, hasira au kutokuwa na subira

Baada ya muda unagundua tabia hiyo haikusaidii wewe wala jamii inayokuzunguka

Hapo ndipo vita vinaanza siyo dhidi ya mtu mwingine, bali dhidi ya hiyo tabia iliyopo ndani yako

Unaanza kujifunza kujizuia kujirekebisha na kuikataa ile hali ambayo haikupi thamani

Kwa mfano, kama zamani ulikuwa huwezi kukaa nyumbani na kila mara ulitamani kutoka, siku moja hamu hiyo inapokuja unaweza kujikuta ukisema

Hapana, siendi leo(unakaza)

Hapo unakuwa umeanza kupigana dhidi yako mwenyewe unayashinda matamanio yako kwa ajili ya lengo kubwa zaidi

Sasa swali la mjadala👇

Wewe umewahi kuwa na vita au mapigano dhidi yako mwenyewe?
Ni nini kilishinda wewe au kile ulichokuwa unapambana nacho?

Ulipigana kwa muda gani, na ulitumia njia gani kushinda?

Nyongeza👇
Kabla hujaanza mapambano hayo, ni muhimu kujifanyia utafiti wa nafsi yako Jifahamu, tambua tabia zako, haiba yako na vitu vinavyokufanya uwe wewe

Baada ya hapo utaweza kuona kama kuna mambo ndani yako unayoyapenda au kuna mengine ambayo yanahitaji kubadilishwa

Kwa sababu wakati mwingine ushindi mkubwa wa mtu siyo kumshinda mwingine, bali ni kujishinda mwenyewe na kuwa yule mtu ambaye anatamani kuwa

Happy weekend 🔥
ShesRise_1 ✋️
Kama hii idea hauja copy popote basi wewe ni mwanamke mwenye thamani kubwa sana, unajielewa sana uwezo wako wa kufikiri mkubwa.

Hata kama sio mrembo.
 
Mimi nilikuwa napigana na tabia ya pombe,Nina mwezi nimeishinda yaani nilikuwa Niko radhi nishinde na Njaa ili nibugie konyagi, Mungu Mwema nimeishinda Mwenyewe!
Hongera sana una haki ya kujivunia ushindi wako
 
Andiko zuri na linaleta uamsho wa nguvu ya mtu ulio ndani yake. ShesRise_1 punguza kuweka Viimoji kwenye nyuzi zinakuwa zinaleta feelings nyingi ambazo zipo mchanganyiko. Kwa ambao tunaelewa baadhi ya emoji zina maanisha nini
Asante mkuu mfano wa hizo emoji?
 
Kujua unachopaswa kufanya hiyo sio vita kamili hua ni mwanzo tu wa kuenda vitani na kuandaa silaha za kutumia
Vita kamili ni ile kuchukua hatua
Na ndicho nilicho ainisha mwishoni.
Vita hii ni rahisi sana, kuacha kile nafsi haipendi, na kufuata kile nafsi inapenda

Kumbuka ni nafsi, na sio mwili, akili au roho
 
😜 mizaha, mahaba , ucheshi kwenye uzi kama huu inakuwa haina maana
Sure hizi emoji zinakufanya mleta mada aonekane ni mtoto to some extent, au ana utoto fulani... Maana kuzitumia katika context ya mada sensitive kama hii inakua kama unachukilia mzaha. Ingekuwa hoja za mapenzi sawa
 
Kama hii idea hauja copy popote basi wewe ni mwanamke mwenye thamani kubwa sana, unajielewa sana uwezo wako wa kufikiri mkubwa.
Mkuu asante kwa pongezi zako nimezipokea 🙏🙏

Swali kwako wewe ni mgeni wa nyuzi zangu?
Nakujibu hivi👇

Naamini hakuna maneno mapya duniani yote yapo tokea zamani

Lakini namna ya kuyatumia hayo maneno ndio hua tunatofautiana

Maneno niliyoandika hapa yametoka kicwani kwangu kama ambayo hua naandika na nitakavyoendelea kuandika huko baadae

Ukikuta bandiko lolote huko mitandao mingine kinalofanana na hili kwa kila kitu basi angalia ni la muda gani then rudi hapa linganisha

Hata kama sio mrembo.
Hii haina umuhimu sana
 
Sure hizi emoji zinakufanya mleta mada aonekane ni mtoto to some extent, au ana utoto fulani...
Mara nyingi unaniambia nina utoto

Ila nakushauri pima utoto au utu uzima. Wangu kupitia hoja zangu na sio Emoji
Maana kuzitumia katika context ya mada sensitive kama hii inakua kama unachukilia mzaha. Ingekuwa hoja za mapenzi sawa
Asante kwa maoni
Hakika siwezi kufurahisha jukwaa zima
Ushauri wako ikibidi nitaufanyia kazi
 
Mara nyingi unaniambia nina utoto

Ila nakushauri pima utoto au utu uzima. Wangu kupitia hoja zangu na sio Emoji
That's the issue with you, huku soma vizuri comment yangu?
Sure hizi emoji zinakufanya mleta mada aonekane ni mtoto to some extent, au ana utoto fulani... Maana kuzitumia katika context ya mada sensitive kama hii inakua kama unachukilia mzaha.
Sikusema wewe ni mtoto nilisema zinakufanya uonekane kama mtoto zingatia hilo next time
Hakika siwezi kufurahisha jukwaa zima
Ushauri wako ikibidi nitaufanyia kazi
Ni kweli ila unatakiwa kupunguza au kujaribu kupunguza Misconception au kudhani mtu anaku attack kila wakati.
 
That's the issue with you, huku soma vizuri comment yangu?

Sikusema wewe ni mtoto nilisema zinakufanya uonekane kama mtoto zingatia hilo next time

Ni kweli ila unatakiwa kupunguza au kujaribu kupunguza Misconception au kudhani mtu anaku attack kila wakati.
Kijana nimesema una ni attack ?
please
Unajua kabisa mimi na wewe hatujawahi kua na mitazamo sawa

Na hilo nimekili mara nyingi ikiwemo kujiepusha na mada zako hata quote zako

Na hili ni ombi lingine naleta kwako kwa mara ya pili tafadhari sana sijisikii happy kujibishana na wewe popote 🙏
 
Mkuu asante kwa pongezi zako nimezipokea 🙏🙏

Swali kwako wewe ni mgeni wa nyuzi zangu?
Nakujibu hivi👇

Naamini hakuna maneno mapya duniani yote yapo tokea zamani

Lakini namna ya kuyatumia hayo maneno ndio hua tunatofautiana

Maneno niliyoandika hapa yametoka kicwani kwangu kama ambayo hua naandika na nitakavyoendelea kuandika huko baadae

Ukikuta bandiko lolote huko mitandao mingine kinalofanana na hili kwa kila kitu basi angalia ni la muda gani then rudi hapa linganisha

Hii haina umuhimu sana
Of course me sijawahi kufuatilia nyuzi zako. Lakini leo nilivyo soma hii nimeona umegusia jambo kubwa sana ambalo watu wengi tunapitia especially self discipline, self control, Faith, bad habits, positive attitude n.k.

 K
iufupi hili jambo ulilo_liandika hapa ni tiba lakini pia ni jambo muhimu na pana sana (nimewahi kufundisha mahali kuhusu hili jambo watu wengi sana walipona vidonda walivyo kuwa wana jiumiza wao wenyewe bila kujua). So hongera sana.

Yes urembo sio muhimu ukiwa na uwezo mzuri wakufikiri kama hivi unakuwa umesha kamilika.
 
Back
Top Bottom