Mapepo ya Harusi: Hivi inakuwaje wasiotuthamini wanatupa thamani wakiwa na shida ya kuoa au kuolewa?

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Wasalaam JF

Niende kwenye mada straight, hivi inakuwaje katika jamii, sehemu za kazi, ujirani, au ndugu, mtu ambae haoni thamani yako anatambua uwepo wako nyakati zake za kuolewa au kuoa hasa michakato ya kuchangia pesa za harusi?

Kuna uhusiano gani kati ya harusi na kuwatafuta watu ambao huwa unawadisi ila unawatafuta nyakati za michakato ya harusi.

Huo ni utamaduni ulioigwa toka nchi gani tufahamishane.

Kwangu mimi mtu akiwa hana ukaribu na mimi anaejikuta akija na shida zake wala siongei nae, najisemesha akiwa anasikia wagalatia wanaonekana kwenye mipango ya utumwa na ufala. Mimi ni yuleyule Mungu aendelee kusimama katikati.

Wadiz ni hayo tu.
 
Mimi nadhani inanikera sana kuliko hata wewe,mtu mpk mnakuwa maadui kisa hujamchangia harusi yake,tena upumbavu na unyonyaji zaidi mtu hamna ukaribu kivile but bado anakulazimisha mchango tena kwa kukuwekea kiwango.

Nimechangia wengi 2022 but 2023 acha nikosane nao,wengine washenzi kweli unamchangia 100000/200000 siku ya harusi unakutana na soda na maji 500 halafu bado unalazimishwa kutoa zawadi kabla ya kula huku ukisimamiwa na wanakamati wanapoasha mmojammoja kutoka nyuma kupeleka zawadi.
 
Wasalaam JF

Niende kwenye mada straight, hivi inakuwaje katika jamii, sehemu za kazi, ujirani, au ndugu, mtu ambae haoni thamani yako anatambua uwepo wako nyakati zake za kuolewa au kuoa hasa michakato ya kuchangia pesa za harusi?

Kuna uhusiano gani kati ya harusi na kuwatafuta watu ambao huwa unawadisi ila unawatafuta nyakati za michakato ya harusi.

Huo ni utamaduni ulioigwa toka nchi gani tufahamishane.

Kwangu mimi mtu akiwa hana ukaribu na mimi anaejikuta akija na shida zake wala siongei nae, najisemesha akiwa anasikia wagalatia wanaonekana kwenye mipango ya utumwa na ufala. Mimi ni yuleyule Mungu aendelee kusimama katikati.

Wadiz ni hayo tu.
Michango
 
Ni hela tu inatakwa, watu wanaingizwa kwenye kamati za harusi ili tu hela zao zitolewe, usishangae hata kwenye ualiko ukaachwa na hela umetoa. Tena siku hizi mpaka send off hela inatakwa. Mambo menine ni upuuzi wa kuchosha watu kwa michango ya kifahari na anasa
 
Kiufupi jamii yetu inapaswa kubadilika na tunaibadilishaje kuacha changia harusi mtu akiwa na harusi ajiandae yey na familia yake arike watu wale pilau wapige makofi sherehe iishe
 
Kiufupi jamii yetu inapaswa kubadilika na tunaibadilishaje kuacha changia harusi mtu akiwa na harusi ajiandae yey na familia yake arike watu wale pilau wapige makofi sherehe iishe
Msimamo wangu ndio huo , japo kuna ndugu wawili watatu wa karibu nitawachangia kwa mara ya mwisho mwisho.
Sitachangia tena harusi bali matibabu na mazishi
 
Kuna wengine wanachangisha michango mijini, wakishachukuwa hela wanaenda kufanyia hiyo shughuli mkoa mwingine tofauti na pale walipokusanya hela, sasa unajiuliza hawa watu walitaka tuudhurie kweli?
 
Back
Top Bottom