thubutuuuuu.. hiyo sheria inatekelezwa barabara mkuu. ukikiuka inategemea na boss wako yuko vipi ila wanasainigi mkataba kuwa hutooa/kuolewa wala kuzaa mpaka miaka mitatu ipite. watu wanafukuzwa kazi kabisa. na kuhusu suala la mkataba wa.ndoa sheria inakiukwa kwa kuzoana bila utaratibu ila ipo na inafanya kazi. kuna masharti ya kuishi na huyo mkeo.. tafuta mwanasheria au askari polisi akuelezee hii kitu mkuu
Utakua askar wewe naomba uni pm
sio askari mkuu
Kujiamini ni sana tu ila sasa mtu kavaa mabaka dah!!!
katongoze mjeda uishie kurushwa kichura na kupigwa mabuti...
Mngojee akiwa amevaa nguo za kiraia ndio umtongoza,akiwa na magwanda yake ukimtongoza tu utakuwa umemvunjia heshima kwa mujibu wa sheria za jeshi la polisi na ana uwezo wa kukuarest kama akiamua na ukashitakiwa,hivyo kuwa makini mkuu
wote wanaolewa na raia ila unaeoa unapaswa kuandika barua ya maombi mkuu... then baadae utapewa masharti ya kuishi na huyo bibie
Nani anataka mlolongo wote huu???
Sitaki stress na umri huu,wapo mabinti wazuri tu uraiani naweza kuoa na moyo ukawa swaaafi.mambo ya vichura,mara awe anaondoka saa 6 usiku mpk asbh anakuambia kaitwa na mkuu.utafanye?
mbona watu wanafuata??? we unataka kuchezea sio kuoa mkuu