Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 59
Mapenzi uwanja mpana,
Ya sasa tofauti na ya jana,
Wakati ule mimi kijana,
Vijana wakipendana,
Huishia kuoana.[/SIZE]
Pesa haikuwa kitu cha maana,
Starehe na mapenzi wala havikulandana,
si lazima mrembo awe msichana,
Ili apate bwana,
wala pesa awenazo mvulana,
Mapenzi yapate kufana.
Namkumbuka Rumi Mavlana,
alisema mapenzi si kubaguana,
na wala si nani wa maana,
Hakuana aliye bora sana,
Na ndivyo ilivyo mbinguni kule kwa Bwana.
siku hizi ni kurumbana,
Uvumilivu hakuna,
kubembelezana sio tena,
Ohh!!! Mapenzi hayana maana,
Ndivyo msemavyo vijana.
Namkumbuka mzee Kenyatta na yule mama Ngina,
Nyerere na mama Maria kweli walipendana,
Mlima na mabonde vyote vya ujana,
Mapenzi yakawazidia,ishia rekebishana,
Wakapata elewana, Uzeeni kuzikana.
Siku hivi mwabomoa kila kona,
Nauliuliza sababu, eti kuzinguana,
Mapenzi hamana tena, Eti mnamegana,
Mmeacha kupendana, na sasa mnarumbana,
Mna nini nyie vijana??????
mwinjuma na Asha walishachumbiana,
Uchumba mwaka wa tatu,kila siku wagombana,
Wazazi wanataka ndoa, tena itakayofana,
Majibu wazazi wakawapa, huku wakizozana,
Bado tupo tupo sana, ...................................
Tena tunasomana,....................................
Itaendelea.
By Domokaya lisilo changua neno.
Ya sasa tofauti na ya jana,
Wakati ule mimi kijana,
Vijana wakipendana,
Huishia kuoana.[/SIZE]
Pesa haikuwa kitu cha maana,
Starehe na mapenzi wala havikulandana,
si lazima mrembo awe msichana,
Ili apate bwana,
wala pesa awenazo mvulana,
Mapenzi yapate kufana.
Namkumbuka Rumi Mavlana,
alisema mapenzi si kubaguana,
na wala si nani wa maana,
Hakuana aliye bora sana,
Na ndivyo ilivyo mbinguni kule kwa Bwana.
siku hizi ni kurumbana,
Uvumilivu hakuna,
kubembelezana sio tena,
Ohh!!! Mapenzi hayana maana,
Ndivyo msemavyo vijana.
Namkumbuka mzee Kenyatta na yule mama Ngina,
Nyerere na mama Maria kweli walipendana,
Mlima na mabonde vyote vya ujana,
Mapenzi yakawazidia,ishia rekebishana,
Wakapata elewana, Uzeeni kuzikana.
Siku hivi mwabomoa kila kona,
Nauliuliza sababu, eti kuzinguana,
Mapenzi hamana tena, Eti mnamegana,
Mmeacha kupendana, na sasa mnarumbana,
Mna nini nyie vijana??????
mwinjuma na Asha walishachumbiana,
Uchumba mwaka wa tatu,kila siku wagombana,
Wazazi wanataka ndoa, tena itakayofana,
Majibu wazazi wakawapa, huku wakizozana,
Bado tupo tupo sana, ...................................
Tena tunasomana,....................................
Itaendelea.
By Domokaya lisilo changua neno.