Mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Domo Kaya, Aug 7, 2008.

 1. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mapenzi uwanja mpana,
  Ya sasa tofauti na ya jana,
  Wakati ule mimi kijana,
  Vijana wakipendana,

  Huishia kuoana.[/SIZE]

  Pesa haikuwa kitu cha maana,
  Starehe na mapenzi wala havikulandana,
  si lazima mrembo awe msichana,
  Ili apate bwana,
  wala pesa awenazo mvulana,
  Mapenzi yapate kufana.

  Namkumbuka Rumi Mavlana,
  alisema mapenzi si kubaguana,
  na wala si nani wa maana,
  Hakuana aliye bora sana,
  Na ndivyo ilivyo mbinguni kule kwa Bwana.

  siku hizi ni kurumbana,
  Uvumilivu hakuna,
  kubembelezana sio tena,
  Ohh!!! Mapenzi hayana maana,
  Ndivyo msemavyo vijana.

  Namkumbuka mzee Kenyatta na yule mama Ngina,
  Nyerere na mama Maria kweli walipendana,
  Mlima na mabonde vyote vya ujana,
  Mapenzi yakawazidia,ishia rekebishana,
  Wakapata elewana, Uzeeni kuzikana.

  Siku hivi mwabomoa kila kona,
  Nauliuliza sababu, eti kuzinguana,
  Mapenzi hamana tena, Eti mnamegana,
  Mmeacha kupendana, na sasa mnarumbana,
  Mna nini nyie vijana??????


  mwinjuma na Asha walishachumbiana,
  Uchumba mwaka wa tatu,kila siku wagombana,
  Wazazi wanataka ndoa, tena itakayofana,
  Majibu wazazi wakawapa, huku wakizozana,
  Bado tupo tupo sana, ...................................
  Tena tunasomana,....................................

  Itaendelea.

  By Domokaya lisilo changua neno.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,549
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Dunia njema wawili wawili
  Hata ndege hukaa wawili

  Siukumbuki vizuri huu wimbo nadhani uliimbwa na Dar Jazz au Kilwa Jazz. Ulikuwa unapendwa sana na wasikilizaji wengi wa vipindi mbali mbali vya RTD na baadaye kwenye kipindi cha zilipendwa.
   
 3. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mama Ngina ni wa Kenyata :)
   
 4. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  You got it right Buddy.
  Thanks for pep up my memory
   
 5. K

  Kinto Senior Member

  #5
  Aug 9, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakubwa mmenikumbusha mbali, wacha niweke tape zangu za afro70 nizikumbuke
   
 6. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0  ........Inaonekana kama haya mapenzi yanaendelea bado DOMO lete vitu.........
  Naona umejaribu kuleta yaliyopita na kizazi kipya pamoja Bravo.
  Kama kijana yule wa Clauds FM na kpindi chake cha top 20 ananikumbusha wakati ule wa RTD na MISAKATO (kama sikosei) nyimbo zinatengeneza stori nzuri ya kupendeza,mjanja sana kijana lkn ni nzuri kutukumbusha tulipotoka
   
 7. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nimefanya H\W yangu nilikosea hapo kwenye hilo jina la kipindi baada ya Misakato ni HISIA KATIKA MUZIKI na bado kipo hewani mpaka leo kwenye TBC TAIFA kina rudiwa kila siku ya jumanne asubuhi nadhani kuanzia saa nne mpaka saa tano kamili asubuhi.

  Na kwako ndugu DOMO KAYA mbona utamu umeukatisha hiyo ni hadithi nzuri ya mapenzi embu lete vitu..................
   
 8. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwaka watatu mwasomana,mapenzi mnatia doa.
  Elimu kwenu ilishindikana,masomo yaliwaboa.
  Sasa mna tatizana,hakuna mnacho jua.
  Mapenzi kuyafanya somo,huo kweli ni ujuha.

  Labda yawe hisabati,mapenzi kuya kokotoa.
  Mapenzi yana majedwari,kujumlisha na kutoa.
  Sufwa namba witiri,kipenyo kuyatafutia.
  Mabanoni mtayari,hakuna wa kuwafungua.

  Mapenzi yana thamani,hata kwenye Biologia.
  Hutoa viumbe hai,na vile msivyo vijua.
  Kushavishana mimeani,ndege wana totoa.
  Ni kuutafuta muhari,mapenzi kuyasomea.

  Mapenzi yana ukweli,hata kwenye fizikia.
  Myapime kwenye mizani,majibu yata wajia.
  Umeme ule mapenzini,wala hauku somewa.
  Ford,Newton wametii,hawa kuweza vumbua.

  Kemia imesha feli,majibu haita toa.
  Nyekundu kua kijani,ndio kazi jaliwa.
  Nyie mwaleta utani,madawa mwachanganyia.
  Wala si maabarani,au mganga kilingeni.

  Mapenzi hayana ramani,kuyawakea mipaka.
  Milimani na mabondini,huko kote yamefika.
  Angani na aridhini,nusu kwa nusu kama ikweta.
  Hiyo wote mnajua………………….
  Jogolafia……………………  Itaendelea…………………………

  Nakaribisha maoni
   
 9. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwakwetu na wewe umo.....safi sana .
  Bravo.
  lete utamu zaidi
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mmmmhhh sio utani...hii imetulia sana mkuu..........mwaga uhondo zaidi mwanawane
   
 11. s

  sikazi New Member

  #11
  Aug 15, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko kamili ...
   
 12. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu Sikazi,
  mbali ya kupenda kutuma ULE UCHAFU pia unapenda mashairi.
  Hongera baba.
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu DK,

  ndio mwisho wa utamu hapa?mbona hamna hapo.............kiswahili,civics, sayansi kimu(kwa sisi tuliyo soma muda kidogo) nasikia sikuizi linaitwa MAARIFA YA JAMII NA MENGINEYOO?

  LETE VITU............MKUU
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  DK,haya mapenzi yako hayawezi kumjibu Mchongoma!?
  Naona nayeye pia anatatizwa na haya mapenzi jaribu kumjibu kwa utenzi maridhawa tuone malingo yako..........
   
 15. H

  Haika JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  asante kwa tenzi nzuri za kuburudisha akili na hisia.
   
 16. s

  swahili state JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2014
  Joined: Oct 14, 2014
  Messages: 245
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Umeona eeh
   
 17. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2016
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sanda matuta katika ubora wake
   
Loading...