Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 8,761
- 8,640
Umofia kwenu!!!!!1
Kwanza kabisa niwatakie heri ya mwaka mpya 2022, ni muda mrefu kidogo nimekuwa ndugu mtazamaji lakini kwa leo naomba nilete hili kwenu.
Kwanza kabisa ijulikane taasisi ya mahusiano na ndoa ndio taasisi mama katika kuishape jamii, kumbuka taasisi hii ndiyo inayozalisha familia na familia ndio msingi wa maendeleo katika jamii yoyote, kupitia hii familia tunapata watu mashuhuri,viongozi wa dini,wanasiasa mashuhuri nk.
Lakini upepo unavyoenda hii taasisi imekubwa na dhoruba kuu, kutokana na changamoto zimewafanya vijana wengi wa kike na wa kiume kukata tamaa juu ya ndoa,ni kawaida tu kusikia "mimi nitafuta wa kuzaa naye tu basi, sitaki kuoa au kuoelewa kama mambo yenyewe ndio haya" Sasa kwanini tumefika hapa???....
1. Mahusiano yamegeuzwa ni sehemu ya ujasiliamali
Vijana wengi wa sasa wamegeuza mapenzi ni fursa ya kutoka, sio tena platform ya kuweza kutengeneza familia bora, vijana wakiume nao siku hizi wanatafuta mwanamke anayejiweza ukiwasikiliza wanasema maisha ni kusaidiana, hiyo kauli imewafanya wengi kupenda kitonga, mabinti nao ni hivyo hivyo unaweza kumpenda binti na kutimiza jukumu lako lakini ukaitwa danga na akawa na mahusiano na mtu mwingine kwa kigezo et huyu ndiye wa moyo, kama huyo ni wa moyo kwanini msiweke juhudi ya kutafuta vya mwili pamoja??
2. Mmong'onyoko wa maadili
Maadili yamepungua kabisa miaka ya nyuma mwanaume kutembea na mke wa mtu, suala lilikuwa halikubaliki yaani iweje utembee na mwanamke ambaye mwenzio amemgharamia na kujiwekea usingizi wake ndani wewe ukammendee ili hali wapo wanawake wengi wanahitaji kuhifadhiwa?? siku hizi imekuwa sifa na nyie ni mashahidi humu halafu inaanza kuonekana ni fahari kwa kijana kutembea na mke wa mtu, inaonekana ni ushujaa huku mwenye mke akionekana hajui mambo maarufu kama "kupeleka moto" Sasa kijana ambaye anatembea na mke wa mtu unafikiri ataoa?... hofu na mashaka ya kutafuniwa itamtafuna
3. Kuwa na Matarajio Makubwa
Vijana wengi wanapoingia kwenye mahusiano au ndoa huwa wanakuwa na matarajio makubwa kutoka kwa wenzi wao hii hutokana na ubinafsi, ule umimi, huyu hanifanyii hivi, mbona hafanyi hivi kama fulani, mwisho wa siku humpelekea mtu kutodumu katika mahusiano aliyoyaanzisha ama ndoa husika, inatakiwa ukumbuke wote ni binadamu na hakuna anayeweza kumtimizia mwenzake mahitaji yake kwa 100% hivyo tuwe wenye kutosheka na kuridhika.
4. Harakati za Haki sawa
Hiki ni kirusi kinachotafuna mahusiano na ndoa za wengine, dada yangu nikukumbushe tu kwenye suala la mahusiano hakuna kitu kinaitwa haki sawa, kwenye mahusiano mwanaume ni kiongozi na ili mahusiano yako yadumu lazima uzingatie hili "Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala" (mwanzo 3:15) . utii ndio kitu pekee na cha msingi sana wanawake wa kizazi hiki wamekosa, wanafikiri utii ni manyanyaso, ni ukatili na ndivyo linavyoweka kwa sura hiyo kitu ambacho si kweli.
5. Wanaume kutotaka kuwajibika katika mahusiano
Mahusiano ni zaidi ya tendo la ndoa ambalo wengi ndio hufikri ni mapenzi hayo, na ndio maana utaona wengi wakilalamika oooh mara ananinyima, oooh mara hafanyi sawa sawa, mahusiano ni zaidi ya hilo tendo hapa tukumbushane, baadhi ya wanaume wanasema kuoa mwanamke mwenye mtoto ni risk, ni kweli lakini huyo mtoto mwanamke anamtoa wapi?? usikute mwanaume umezalisha huko halafu unatembea kifua mbele kwamba sioi mwanamke mwenye mtoto, huyo uliyempa mtoto amuoe nani?? hao watoto/mtoto anatengenezewa sai8kolojia ya namna gani? muda mwingine akina dada mnasababisha hili mkihadaika kwamba pengine nikibeba mimba atanioaa, au anakuambia nizalie mtoto sitashindwa kumlea wakati unaona kabisa wewe mwenyewe mahitaji yako hupati sawa sawa, mwisho wa siku tunatengeneza watoto ambao hawana upendo wa kweli, watoto wanakuwa hawajali wala kuheshima
Tusipoliangalia hilop tukalichukulia kawaida basi tunatengeneza kizazi cha ajabu sana hapo baadaye, tutakao kuja kulaumiwa ni sisi, sasa hivi hali sio nzuri huwezi ukapita nyumba mbili tatu ukakosa binti aliyezalia nyumbani, itafika kipindi kumpata mwanamke ambaye hajazaa kabla ya ndoa itakuwa kama kusaka bikira, na litakuwa jambo la kufurahiwa sana kuliko kukutwa na bikra.
Samahani kwakuwachosha kwa thread ndefu najua mnapenda fupi fupi, mniwe radhi kwakweli, na hayo ni kulingana na mtazamo wangu na hali ya mazingira yaliyopo kwa sasa.

KARIBUNI KWA MJADALA