Mapenzi yanauma sana

Mapenzi yanauma sana

Habari zenu, Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu, jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe muda ili atafute pesa zaidi, nilikubali lakin ilivofikia mwaka huu mwezi wa saba akasema tuachane , hivyo nilimkubalia maana mahusiano hayalazimishwi.
Shida ya dada zetu ukiwa mpole wanakuona kama bwege hyo inaitwa away team won both halves

Nothing can surprise me any more!
 
Jua litazama ma mdogo.. atakuja kutafuta mume yoyote huyu
Kitakachomsababishia hayo ni kutokujitambua kwake tu!!
Kwanza anavyosema mapenzi yanauma hivi alishawahi kubanwa na mlango kile kidole cha mwisho (kidogo) cha mguu akasikilizia maumivu yake???
 
Miaka 23,Mahusiano ya miaka 5 23-5=18

Halafu unataka kumsahau.

Iko hivi mrembo.Wewe ni mdogo na mzuri sana na unavutia wanaume wengi sana hasa kwa sababu ya umri wako na uzuri wako.Hata hivo suala la ndoa na kuolewa ni majaliwa.Kuhusu kumsahamu uliyemuacha ni swala la muda na wewe utakavoamua.Mapenzi yanauma na yasipouma sio mapenzi ni kupoteza muda wako.


Ushauri wangu.

Kunywa maji mengi,Cheka,jichanganye na watu na zaidi hakikisha kwamba haufikiri kwamba wewe ndo umepoteza kwa kuachwa kwani kwa uzoefu wangu yule ambaye anamuacha mwenzake hasa bila sababu ya msingi huwa ndo anapata hasara.Hii ni kwa sababu yeye atakuwa anabeba majuto hasa kama mambo yake yakienda hovyo katika mapenzi.

So ukiachwa umepewa nafasi ya kutafuta mtu bora zaid na kuwa mtu bora zaidi.
 
Polee mdogo wangu, pia Hongera kwa kuwa muaminifu Kwa jamaa kwa hiyo miaka yote mitano.

Lakini tambua kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako hakukupi guarantee ya wewe kutokuachwa, cha msingi soma alama za nyakati ukishaona mwenzio haeleweki Anza kujiweka mbali naye usije enda extra miles zaidi kufanya come back huwa inakuwa ngumu kidogo.

I hope utapata mwenye kujua thamani yako

Ila kwanini akafikia hiyo hatua, je kuna kitu aliomba ukamnyima au ulibadili baadhi ya tabia zako za awali may be ndo zilimfanya avutiwe nawe au kuna mengine hutaki kuyasema????
 
Habari zenu, Mimi binti wa miaka23, naomba mnipe ABC ndg zangu, jinsi ya kumsahau mtu aliye kuacha.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mkaka kwa zaidi ya miaka 5 , ikafika muda akataka aende home kupeleka mahari lakini baadae alisema kuwa nimpe muda ili atafute pesa zaidi, nilikubali lakin ilivofikia mwaka huu mwezi wa saba akasema tuachane , hivyo nilimkubalia maana mahusiano hayalazimishwi.

Ikumbukwe huyo kaka wakati nipo nae nilikuwa nikikataa wanaume wengine waliokuwa wakinifuata , baada ya kumuona yupo serious, niliamua kufanya nae malengo,Mimi ninapenda biashara japo elimu yangu chuo sikusomea mambo ya biashara, nilimshauri pamoja na kufanya nae mambo mengi sana, taratibu akaanza kutoka hatuwa aliyokuwa nayo na kwenda hatua ya juu zaidi ya kimaendeleo.

Baada ya kuona nimeshampenda ilifika hatua hadi alihama alipoishi bila kuniambia,lakini mim naishi na wazazi , baada ya Mimi kupafahamu kwake matokeo yake alinitambulisha kuwa mim n mdogo wake niliumia sana na ndy mwanzo wa kunifanya visa hadi tukaachana niliumia sana maana nilimpenda mno.

Sikutaka kupoteza muda pia kuna kaka alikuwa akinitaka niliamua kumkubalia ili nizidi kupoteza mawazo na kumsahau haraka yule wa mwanzo ,tulianza vizuri lakini na yeye yapita wiki moja Sasa tumesha achana, nilichokigundua kwake hakuwa serious na hatahivyo alitaka nimpende kwa pesa zake hivyo alitumia nguvu nyingi kunionesha alivyonavyo, baada ya Mimi kuona nimempima kwa vipimo vyangu ndipo aligundua kuwa nimejua anacho hitaji na kukndoka mwenyewe.

Ndg zangu yote haya yaliyo nikuta , kusema Ukweli ninahitaji faraja ya moyo saana ,maana ninatamani kuwa na mahusiano serious lakini wanaume kwa Sasa hawaeleweki, hata wawe wachaMungu ,hakuna lolote, inshot mi napenda kusali(mkristu) lakini mkaka akishajua jinsi ulivyo nae anakuja kwa style hiyo hiyo Ninahisi kwa Sasa hakuna waoaji maana nimekata tamaa kabisa.

Natamani sana kuwa hata na mpenzi anayejitambua , anayejua kutafuta pesa ,ambaye hajaoa wala Hana mtoto ,maana Mimi pia Sina mtoto, awe mtumishi , zaidi ya yote awe mchamungu .
Hata wanawake wa kuoa hakuna....karibu wote ni wadangaji kwa 99%.......we endelea kuliwa kimasihara hivyo hivyo
 
Mtumishi, Mcha Mungu, Asiye na Mtoto, hahaha...ngoja afike 38 ndio atajua nini maana ya vigezo...23 si yuko shule?
bado miaka 7 atataka yeyote anae pumua angalau.....sasa hivi mwache asugue bench kwanza
 
My wangu usisumbuke hata....jiweke busy kua busy tafuta issue za kufanya fanya.......maisha yatasonga....wanaume wengi sa hv ni waongo sana wengi ni matapeli tu
Tatizo wanawake mnapiga virungu mno....ndiyo maana vijana wa kiume wanawayeyusha
 
Pole sana. Ni kweli siku hizi kuna shida kila upande. Endelea kumwomba Mungu na kusahau yaliyopita. Wakati ukuta. Mungu atakuletea wa moyo wako. kumbuka hao wote walikuwa hawajapangiwa kwako ndiyo maana wameondoka bila kukuachia majeraha ya kudumu.
 
Back
Top Bottom