Kamawewe
JF-Expert Member
- Jan 16, 2013
- 537
- 526
Habari wana JF, ninaomba ufafanuzi au ushauri wa hali ninayokuwa nayo katika maisha yangu ya kimahusiano,kifupi mimi ni Mwanaume mwenye umri wa miaka 30 na nina Mwenza. Kabla ya Mwenza niliyenaye nilikuwa na mpenzi ambaye chanzo kikubwa cha kutengana ni kwamba Mimi nilikuwa mara kwa mara ninamueleza kwamba anafanya mambo ambayo ninaona ni uchafu katika maisha ya kila siku wakati mwingine ninapata hadi kichefuchefu, lakini Yeye amekuwa akinilaumu kuwa ninazingatia usafi kwa kiasi kilichopitiliza hiyo hali ilienda hadi tukatengana.
Kama miaka miwili iliyopita nikawa nimeanzisha uhusiano na Mwanamke Mwingine niliyenaye sasa lakini tatizo lile lile limejitokeza, hapa sasa nikaamua kuwauliza rafiki,ndugu na wafanyakazi wenzangu kujua ukweli juu yangu, nilijisikia vibaya pale karibu wote waliponiambia wanavyoone ni kweli tena wangine wananiogopa katika mazingira fulani kwa kuwa ninawaona hawawezi kufanya usafi na mpangilio wa vitu kikamilifu, hapa ninaongelea zaidi nyumbani au ofisini ndugu au wasaidizi mbalimbali wa nyumbali na ofisini, ata my college mates walinithibitishia hilo.
Wana JF hebu nisaidieni hii hali inasababishwa na nin ina njia gani za kuipunguza? maana kwa study niliyoifanya ni kweli nina tatizo linaloathiri uhusiano wangu na wanajamii hasa kimapenzi.