Mapenzi ya Kikwete kwa Haji Mponda na Lucy Nkya, Mauti kwa Watanzania Masikini

Sitashangaa nkisikia wanasema CDM wako nyuma ya haya yote manake kila anayedai haki yake, badala ya wakuu kutatua tatizo wanasema "CDM ndo wamesababisha"
 
Hii awamu ya pili ya mkweree ni lala salama yake ya kuiba hivyo sio rahisi yeye kuwafukuza kazi Mponda na Nkya wizara ya Afya wakati huo huo akawaacha Ngeleja na Malima wizara ya nishati na madini!! Huku kwenye nishati na madini ndiko alikoegemea katika wizi wake wa lala salama.He does not want to create a precedent ya kuwafukuza hawa wa afya; wadanganyika mpo hapo, hivyo atawaacha watu wafe halafu aende kwenye mazishi kama desturi yake ya unafiki.
 
ngoja tusubiri kujua nani anayetishika.
nimemsikia akisema kama habari za polisi kula rushwa ni kweli,yaani anazungumza kama raia wa kawaida.
intelejensia yake anaipatia kwenye magazeti?

Fanya kazi zako utunze familia, hayo mambo ya kusubiri uone anayetishiwa nyau hayakuongei kitu. Usitegemee kuona busara aliyoitumia Pinda wakati ule...this time atatekeleza kauli yake ya awali...nadhani unaikumbuka.
 
Wana JF,

Rais Kikwete kwa mara nyingine tena amedhihirisha kwamba yeye ndiye chanzo kikuu cha mgogoro na mgomo wa Madaktari. Inasikitisha kuona kwamba pamoja na mamia kama siyo makumi kadhaa ya Watanzania kupoteza maisha yao mwezi uliopita kutokana na mgomo wa Madaktari Kikwete wala hajali!

Nchi za wenzetu ambako uhai wa kila Mwananchi unathaminiwa kifo cha Raia mmoja tu kinaweza kumfanya Rais wa nchi akajiuzulu lakini siyo Tanzania. Rais gani asiyejali uhai wa watu waliompa ridhaa ya kuwaongoza hata kama aliingia kwa kura za wizi?

Kitendo cha Rais Kiwete kuendelea kuwakumbatia Waziri wa Afya Haji Mponda na Naibu wake Lucy Nkya kimeonyesha kuwa Kiwete hathamini uhai wa mamilioni ya Watanzania wanaopatiwa huduma na madaktari wetu. Inawezekanaje UTHAMINI AJIRA YA WATU 2 ULIOWATEUA KUSHIKA NAFASI YA UWAZIRI na UNAIBU WAZIRI lakini USHINDWE KUTHAMINI UHAI WA MAISHA YA WATANZANIA ZAIDI YA MILIONI 40???

Hivi Rais Kiwete akiwaachisha Uwaziri na Unaibu Waziri hawa watu 2 atakuwa amepoteza nini hasa???Sielewi kama Rais Kiwete huwa anakaa na kufiri juu ya matukio kama haya au huwa anategemea ushauri kutoka kwa wasaidizi wake kwa kila kitu.

Sasa naamini kuwa Kiwete hayuko makini hata kidogo. Inanikumbusha utani mmoja niliousikia kuwa kuna siku moja WATU WATATU WALIKUTANA. Mjerumani mmoja,Mmarekani mmoja na Mtanzania mmoja na wakawa na mazungumzo kama ifuatavyo:

  • Mjerumani akaanza,''Sisi kule Ujerumani kuna mtoto alizaliwa hana miguu.Basi akawekewa miguu ya bandia na kwa sasa huyo jamaa ni Bingwa wa mbio za Marathoni za Olympic.
  • Mmarekani akasema,''Sisi bwana kule Marekani kuna mtoto alizaliwa akiwa hana mikono basi akawekewa mikono ya bandia na kwa sasa huyo jamaa ni Bingwa Ndondi ulimwenguni.
  • Mtanzania alikuwa wa mwisho kuzungumza,akasema,"Nyie mbona mnaleta utani,hizo za kwenu ni cha mtoto bwana. Sisi Tanzania kuna mtoto alizaliwa hana kichwa,basi tukamwekea kichwa cha nazi na sasa ni Rais wa Tanzania!

Huu utani unachekesha lakini kuna ukweli ndani yake. Fikiria juu ya Nchi inayoongozwa na Rais mwenye kichwa cha nazi! Tanzania ndipo tulipo, kuwa Rais wetu hawezi kufikiri vya kutosha kuhusu maswala mazito ya kitaifa na kuyatolea maamuzi magumu kwa interest ya Nchi.Kiwete amethibitisha kuwa ni kiongozi mwoga,dhaifu na mnafiki wa hali ya juu. Hilo limeonekana kwenye speech yake ya mwisho wa Mwezi aliposema, ATI ALISAINI MSWADA WA KATIBA MPYA KWA KUOGOPA HASIRA ZA WABUNGE WA CCM!

Ebo,unaogopa hasira za Wabunge wa CCM ina maana Wabunge wa CCM ndio waliokupa Urais? Hii ni mawazo ya kichwa cha nazi. Kushindwa kuwafukuza Dk.Haji Mponda na Lucy Nkya ili Watanzania waendelea kufa ni uthibitisho wa kichwa cha Nazi.

Maandishi mekundu, haina mvuto tena hiyo imepitwa na wakati. Ndiyo kwanza unaingia JF nini? ya tangu 2006. Tafuta nyingine.
Hivi Mponda na Nkya kweli kujiuzulu ndiyo suluhisho la matatizo ya Madaktari? nadhani Watanzania kuna kitu tunakosa vichwani mwetu. Tunasema kwa sababu wanaharakati na Madaktari wamesema au tunasema tunachokijua? Wakishajiuzulu itabidi madaktari warudi kazini kwa furaha na kusahau madai yao. Halafu watakapokuja awamu nyingine watakuja na lipi? Nakua na wasiwasi na Taaluma zao. Sidhani kama walikula viapo vya kazi.
 
Jk huwa anahudhuria clinic ya wagonjwa wa akili huko nje kwa hiyo ni sawa anavyofanya. Kama tunachagua taahira kuwa raisi mnashangaa nini. Acha tukome !
 
Sitashangaa nkisikia wanasema CDM wako nyuma ya haya yote manake kila anayedai haki yake, badala ya wakuu kutatua tatizo wanasema "CDM ndo wamesababisha"

Kama wewe ndiye mwenye fikra hizo kwa nini unasema kwa kuogopa?
 
Aiseee! umeamka asubuhi hii ukaona leo usipoandika kitu JF siku kwako haitaisha! Please rethink harafu urudi tena kutetea hoja yako.

kwa kisa kipi? ukweli; always , unauma...................
 
hivi huyu haji mponda na lucy nkya ni madaktari kweli ama ndio ule wakwetu wakupewa, na je wanaroho ya kibinadamu kweli ama kishetani??? pili kwani walzaliwa wakiwa mawaziri??? kama suala la pesa si wamesha zipata zakutosha ama hawajui hiyo pesa wanayo ingangania ilimsaliti bwana yesu.
tena kipindi hiki cha kwaresma hivihuyu mama anakwenda kanisani kweli na anashiriki sakramenti ya meza ya bwana na anajua maana yake ama anakula ilimradi aonekane naye amepata sakramenti???

damu inayomwagika (wagonjwa wanaokufa) sababu ya kiburi chao itawahukumu siku ya mwisho wakae walielewe hilo!!
 
kwa heshima ya raisi wetu na kwaheshima ya watanzani pamoja naheshima yenu dr. mponda na nkya tunawaomba MJIUZULU kwani mtapungukiwa nanini????????????? natoka nitarudi baadae:flypig:
 
Kwa kuwa jk amedhamiria tufe kwa kukosa huduma za tiba sahihi, tumsubiri si anapenda sana kuongoza mazishi, ikitokea kadhia hii muhanga nikawa mimi au wewe, akifika tu eneo la kaburi asukumizwe kaburini, wenye machepe mfukieni fasta, atakayekuwa maiti kwa wakati huo amng'ang'anie huko chini hakuna kumuachia. Utakuwa mwisho wa upumbavu wa aina hii. Lijitu halijui limeajiriwa na nani!
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Kikwete si rais wa nchi hi mana Ikulu hakuingia kihalali aliiba kura,uwezo wa kuongoza hana mana hakuchaguliwa na wananchi,wala uchungu wa watanzania hana mana hakuchaguliwa nao,kila siku safari za nje hazimuishi kwenda kutalii,ni heri atuachie nchi yetu kama kuiharibu ameshaiharibu vya kutosha wakishirikianana chama chake legelege cha CCM.
 
yaani tunakufa kwa sababu ya watu wa wili tu?....je katibu mkuu wa wizara ya afya ni nani?..hakuna anaweza kuteuliwa hiyo nafasi hata kwa kukaimu>..vipi nafasi ya mganga mkuu?,,,je matataizo ya madaktari ni nani anayashughulikia kwa sasa?...
 
Kwa wale wanaomfahamu Pinda walishtushwa sana pale ambapo aliteuliwa kuwa PM baada ya E.L kubwaga manyanga........wengi wetu wa ambao tunamfahamu vizuri tulimwona ni kiongozi dhaifu ambaye ni bendera fuata upepo. Tulipojaribu kuhoji sifa za Pinda lakini tukanyamazishwa ya kuwa apewe muda wa kutosha kabla ya kuhukumiwa..................ninaamini muda kapewa wa karibu miaka 4 hivi na utendaji wake una walakini mkubwa..........

Kwanza hana maamuzi thabiti.

a) Kwenye swala la mahakama za kadhi, yeye akiwa mwanasheria- pamoja hajawahi kukanyaga mahakamani na kumtetea mtu yoyote yule- i.e he lacks judicial experience..... alilipotosha bunge ya kuwa hilo linawezekana ndani ya katiba yetu jambo ambalo ulikuwa ni upotoshaji. Mhe. Samweli Sitta ndiye aliyeokoa jahazi pale alipotoa ufafanuzi sahihi kuwa katiba yetu inakataza upendeleo wowote ule wa kidini!!!!!!!!!

b) Kwenye suala la mauaji ya kikatili dhidi ya malbino majawabu yake yalikuwa kutoa machozi ya mamba na kujaribu kuturubuni kwa kusaka huruma zetu ambazo nazo si haba.............na haba haba hujaza kibaba. Hadi leo hajaweka mikakati yoyote zaidi ya kuwadhulumu waganga asilia haki yao ya kujitafutia kipato kwa kuwatupia lawama ambazo hazina ushahidi. Na ana bahati sana ya kuwa waganga tajwa hawakwenda mahakamani kumshtaki kwa kuwachafua majina yao na kuwazuia kujipatia kipato khalali.........

c) Kwenye suala la uwajibikaji wa watendaji serikalini baada ya kashfa ya Dowans/Richmond wakiwemo kibosile wa Takukuru; Dr. Hosea, Pinda amekuwa mstari wa mbele kukwamisha jitihada za bunge kuwawajibisha wakorofi tajwa hususani kibosile wa Takukuru ambaye bila ya aibu alilidanganya bunge na taifa kwa ujumla ya kuwa hakuna ufisadi kwenye richmond jambo ambalo Bunge kupitia kamati yake teule iliyoongozwa na Mwakyembe ilibaini vinginevyo. La ajabu hadi alipostaafu mwishoni mwa mwaka jana, Dr. Hosea aliendelea kutesa pale takukuru na hii inathibitisha Pinda si kiongozi mwenye dhamira ya kutoa maamuzi imara wakati yanapohitajika.

d) Kwenye sakata la katibu mkuu pale Wizara ya Nishati Pinda alitoa majibu yenye utata. Kwanza akiunga mkono hoja za wabunge kuwa mhusika alipaswa kuachia ngazi halafu baadaye akidai yeye siye mteuzi wa nyadhifa husika. Yeye mweyewe kwenye nafasi ya U-PM huhusika katika uteuzi wa nyadhifa zote serikalini lakini kwa sababu hana ushawishi wa kisiasa wa kutosha basi amekuwa akiegemea upepo kadri unavyomsukuma!!!!!!!!!!!

e) kushindwa kumshauri Raisi ya kuwa malalamiko ya wafanyakazi wote wa umma hususani ndani ya serikali kuu na serikali za mitaa yanatokana na kuwepo mihimili mingi ya kupanga masilahi ya wafanyakazi na Hazina kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria ya kuratibu mahitaji hayo. Katika khali hii taifa linaendelea kuyumba kutokana na kuwa na waziri mkuu asiye na uwezo kwa majukumu aliyopewa na JK kwa sababu za kujilinda nafsi yake. JK kama walivyo maraisi waliomtangulia hupendelea kuteua PM dhaifu ili kujilinda wao wenyewe wasifunikwe na PM chapakazi endapo angeliteuliwa.

Unafiki wa wazi.

Kama nilivyobaini hapo awali ni dhahiri Pinda ni mtaalamu wa unafiki na hutumia kauli za upole kuhadaa watu kuwa ni kiongozi mwaminifu na ambaye anajali masilahi ya taifa lakini ukweli lazima tuufichue ya kuwa Pinda ni mtaalamu wa kujali masilahi yake binafsi na ndiyo maana hawezi kushauri maamuzi ambayo yanatofautiana na bosi wake au ya wale anaowaona wako karibu na bosi wake.

Mapendekezo.

Wakati sasa umefika kujiuliza hivi JK na Pinda ni viongozi sahihi katika safu ya uongozi wa juu wa taifa hili? Nionavyo Pinda aonyeshe njia kwa kujitoa kafara khalafu JK aamue kusuka au kunyoa........................kwani hiki kitanzi cha kushindwa kurekebisha uchumi hakitamwacha salama...................utashangaa hivi sasa BOT wanazungumzia kuanzisha noti za 50,000/= na laki moja................................na huku baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya BOT wanafikiria kupika muswada wa kufuta sifuri tatu kwenye sarafu yetu kama Zimbabwe walivyofanya na bila ya mafanikio zaidi ya kuitelekeza sarafu yao sasa wao ni US dola mtindo mmoja........................

Bye-bye Pinda & na JK wake...........................uchumi dororo ndiyo utawauumbua......
Naunga mkono hoja!:
 
Hii awamu ya pili ya mkweree ni lala salama yake ya kuiba hivyo sio rahisi yeye kuwafukuza kazi Mponda na Nkya wizara ya Afya wakati huo huo akawaacha Ngeleja na Malima wizara ya nishati na madini!! Huku kwenye nishati na madini ndiko alikoegemea katika wizi wake wa lala salama; wadanganyika mpo hapo, hivyo atawaacha watu wafe halafu aende kwenye mazishi kama desturi yake ya unafiki.
Hivi wagonjwa wakifa kwa sababu eti Madaktari wamegoma na Madaktari nao watakwenda kwenye misiba hiyo? kama ni ndugu yangu ndiye amefariki itabidi nicheke badala ya kulia kwa sababu hii itakuwa kama sinema vile. Lakini Mungu mkubwa anaweza kuanza na watoto wa madaktari kwanza then wakaanza wagonjwa wengine, tusicheze na maombi. Tunajidanganya kwamba Mungu anamuona Rais, Waziri Mkuu , Mponda na LUCY Nkya kwamba ndiyo wenye makosa. ANANILEA, BISIMBA,NAMALA, SLAA na wengine wote watafanyiwa uchambuzi na hapo pumba na Mchele vitatenganishwa.
 
Jk huwa anahudhuria clinic ya wagonjwa wa akili huko nje kwa hiyo ni sawa anavyofanya. Kama tunachagua taahira kuwa raisi mnashangaa nini. Acha tukome !

Tunateseka kwa sababu Rais aliye madarakani hakuchaguliwa na watanzania, alitumia pesa yake kupata madaraka, viashiria ndio kama hivi, jifunzeni kwa mfano wa nabii suleiman alipoletewa kesi mbele yake kuwahusu wamama wawili wakivutania kitoto kichanga ki-hai na mwili wa kitoto kichanga kana kwamba mtoto yupi ni wa nani huku kila mmama akidai aliye hai ndiye wake! (mmama mmoja wao alifanya hila, alimlalia mwanae usiku akafa, akamchukua wa mwenzie na kumuweka wake aliyekufa ubavuni pa mwenzie. walipoamka tazama mwenzie alipomtazama kwa makini aligundua kitoto kilichokufa si chake mzozo ukaanzia hapo) mfalme suleiman alipoona kila mmoja anang'ang'ania kuwa mtoto mzima ndiye wake, aliamua aletewe shoka ili amcharange vipande viwili awagawanyishe wale wamama. yule mwenye mtoto hai aliposikia hivyo akamwambia mfalme akasema mpatie huyu mama mtoto huyu hai usimcharange! lakini yule aliyemlalia kichanga wake akamwambia mfalme akasema "bora umcharange tukose wote!!!" ndiposa mfalme suleiman alipotambua ya kuwa kichanga hai kilikuwa cha yule mama aliyebambikiwa na mwenziwe, na akaamuru akichukue kichanga chake. AMINI NAWAAMBIENI kikwete hakuchaguliwa na watanzania. Ni baba gani watoto wake wakimuomba samaki akawapa nyokaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom