Mapenzi ya Kikwete kwa Haji Mponda na Lucy Nkya, Mauti kwa Watanzania Masikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi ya Kikwete kwa Haji Mponda na Lucy Nkya, Mauti kwa Watanzania Masikini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Mar 6, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ni dhahiri kwamba Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr. Haji Mponda na naibu wake Dk. Lucy Nkya hawako tayari kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi zao za uongozi katika Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.

  Ni dhahiri kuwa Dr. Mponda na Dk. Nkya wako tayari kuona watanzania wakiendelea kupoteza maisha ilimradi tu wao hawaachii ngazi katika wizara ya afya na hivyo kupoteza ulaji.

  Ni dhahiri kwamba Raisi Kikwete anawapenda sana hawa wateule wake na angependa kuona bado wanaendelea kuisimamia wizara ya afya kadri anavyoona inafaa.

  Ni dhahiri kuwa kuendelea kuwepo wizara ya Afya kwa Dr. Mponda na Dk. Nkya kutasababisha madaktari waendelee na mgomo na hivyo kusababisha vifo vingi kwa watanzania masikini wasiokuwa na hatia na ambao wanahitaji huduma za afya katika hospitali zetu za umma na hawana uwezo wa kwenda kutibiwa hospitali za binafsi, za hapa nchini ama kwenda nchini India.

  Katika hali hii ningemuomba Raisi kikwete awahamishie wizara nyengine hawa wapenzi wake ili kuokoa maisha ya watanzania wengi watakaoathirika kutokana na mgomo wa madaktari kufuatia 'kiburi' cha hao wateule wake.
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tatizo si Mawaziri bali ni Pesa. Kama mtataka madaktari na walimu mishahara ipande ni lazima Watanzania wafanye yafuatayo

  (1) Punguzeni ukubwa wa serikali- Pesa hizo hizo ambazo zingetumika kuongeza mishahara zinalipa mkataba wa ndege mbovu ya ATC. Hivyo Punguzeni serikali kwani inafanya vitu vingi sana
  (2) Kipato-Serikali ni lazima iongeze kipato haiwezi kuchukuwa mishahara ya polisi au walimu na kulipa madaktari! ni pwagu na pwaguzi ni lazima tuongeze kipato cha kodi.
  (a) Wasaidie Bank kuu kuanzisha credit system, angalia rate za T- Bills ili upunguze gharama za mikopo
  (b) Weka Technologia wizara ya ardhi ili vibali vya viwanja visichukue miaka mitatu au mi nne.
  (3) Rushwa- Kuna watu wengi wanafaidika na matatatizo ya Tanzania tuweke sheria ngumu za rushwa.
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sidhani!
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Walau wewe umemuomba.... Bi Bisimba kumuamuru mukulu kwa "kumtaka" awawajibishe....lol (Sorry) ila nimeshindwa kuto cmment hilo
   
 5. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja kwanza serikali iendelee kupima kima cha mto kwa mguu!!
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kamundu,
  Mawazo yako ni mazuri sana kama yatafanyiwa kazi kikamilifu na kama tutakuwa na serikali isiyotafuta kulipa fadhila bali kuwatumikia wananchi. Ingawa pia mpango kama huo ili utekelezwe unahitaji muda mrefu, for instance hadi bajeti ya mwaka ujao.

  Lakini kwakuwa tuko katika hali ya dharura (state of emergency) basi tunahitaji maamuzi ya haraka sana kiasi kwamba uamuzi rahisi na wa busara ni kuwahamisha hao wateule wake ili kuwanusuru wananchi watakaoumia kutokana na mgomo wa madaktari.
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Inavyoonekana Mponda na Nkya wana Umuhimu sana Kuliko Maisha ya Watanzania
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  AshaDii,
  Dr. Kijobi Simba ameongea kisheria kwa ku refer vifungu vya katiba. Lakini wote tuna lengo moja tu, kuepusha vifo vinavyoepukika!

  Btw, hongera kwa kazi nzuri MMU 2011.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Na Madaktari kuacha Watanzania wafe kwa sababu eti Mawaziri hawakujiuzulu ni haki au Mauti ya aina hiyo siyo mabaya? Watanzania bwana wa ajabu kweli. Madaktari mtambue kwamba inaweza kuwa kosa mawaziri kutojiuzulu lakni kugoma kwa sababau waziri hakujiuzulu siyo tu ni kosa bali pia ni Dhambi. Binafsi siwezi kuunda mkono dhambi hiyo.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Albedo,
  Hiyo ndiyo imenifanya nijiulize mara mbilimbili juu ya kiwango busara ya hawa mawaziri, kwamba hawathamini kabisa maisha ya watanzania wenzao.

  Inakuwaje uwaziri wa Dr. Mponda na Dk. Nkya unakuwa muhimu zaidi ya maisha ya watu?
   
 11. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumuomba na kumtaka yote yana lengo moja tofauti ni lahaja tu!
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kma madaktari wanavyoona umuhimu wa Mawaziri kujiuzulu kuliko kutibu wagonjwa. Si wakasimamie Dispenzsari zao walizofungua kwa dawa za Serikali. Serikali sijui kama inajua vifaa vinavyotumiwa katika Dispensari zao ni vya Hospitali za walipa kodi?. Tunaomba sasa Sheria zifuate mkondo manake ndizo zinazowapa kiburi. Watanzania ifike mahali tuhoji Dispensari hizi za hawa Madaktari wanaojifanya wanasiasa
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Thatha,
  Kwakuwa madaktari wanahitaji kuendelea kuongea na serikali ili kutatua kero zao, na kikwazo kimojawapo cha wao kumaliza matatizo yaliyopo baina yao ni Mponda na Nkya. Kwahiyo busara inanituma kumshauri raisi awahamishe hao mawaziri katika wizara nyengine kwakuwa haiwezekani kuwahamisha madaktari ili kutatua mgogoro uliopo.
  Kwa kufanya hivyo atakuwa amenusuru maisha ya watu na kuruhusu mazungumzo yaendelee.
   
 14. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Style ya Jk inanikumbusha wakati tukiwa sekondari tunakataka kuwa viranja wa shule.kwa kuwa wagombea ni wengi ilitulazimu kumhonga Discipline master ili jina lako lipitishwe kwenye mchujo. Sasa ukishaukwaa ukiranja hata kukutimua ukikosea inakuwa ngumu maana alishameza ndoano.
  Sasa nahisi kusudi upate uwaziri kwa JK kuna masharti wanapeana ndo maana inakuwa ngumu kujiuzulu au Jk kuwafukuza kazi.
   
 15. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama kweli vifaa tiba vinatolewa na serikali katika hospitali zake vinachukuliwa na hawa madaktari na kupelekwa katika dispensari zao, basi kiwango cha uzembe na kutojali kwa serikali ya kikwete ni cha kutisha na hakuna kiongozi wa afya anayefanya wajibu wake sawa sawa.
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inawezekana Dr. Mponda na Dk. Nkya wamo kwenye kundi la mtandao?!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kukumbatia watu wawili ni bora kuliko maelfu?
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji,
  Hilo ndio swali linalonitatiza, na wengine nao bila shaka wanatatizwa na swali hilo.
  Natamani kujua rais Kikwete anawaza nini juu ya hili sakata.
   
 19. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa raisi wangu ana nini jamani? Whats so special kwa hawa watu wawili mpaka aruhusu serekali yake iingie kwenye mgogoro hivi? Kama aliruhusu na kuridhia kuondoka kwa waziri mkuu anashindwa nini kwa hawa? Najua humu ndani wapo watu wake wa karibu, mshaurini hata kama anadhani ni watu wa muhimu kwake na serekali yake, basi awabadilishe wizara kutuepushia dhahma itakayotokea!
   
 20. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sioni sababu ya Serikali kuamrishwa na wanaharakati namna y akuendesha cabinet.Leo hii ukiacha madaktari wakuchagulie nani awe waziri na nani asiwe ujue hapo hamna serikali. Nkya na Mponda nyie komaeni tu kwenye nafasi zenu. Mpaka sasa hamna yeyote mwenye sababu zinazoingia akilini juu ya kujiuzulu, si Dr Ulimboka wala Bisimba
   
Loading...