Aiseee! umeamka asubuhi hii ukaona leo usipoandika kitu JF siku kwako haitaisha! Please rethink harafu urudi tena kutetea hoja yako.
Ni ukweli mtupu..................
Kwa wale wanaomfahamu Pinda walishtushwa sana pale ambapo aliteuliwa kuwa PM baada ya E.L kubwaga manyanga........wengi wetu wa ambao tunamfahamu vizuri tulimwona ni kiongozi dhaifu ambaye ni bendera fuata upepo. Tulipojaribu kuhoji sifa za Pinda lakini tukanyamazishwa ya kuwa apewe muda wa kutosha kabla ya kuhukumiwa..................ninaamini muda kapewa wa karibu miaka 4 hivi na utendaji wake una walakini mkubwa..........
Kwanza hana maamuzi thabiti.
a) Kwenye swala la mahakama za kadhi, yeye akiwa mwanasheria- pamoja hajawahi kukanyaga mahakamani na kumtetea mtu yoyote yule- i.e he lacks judicial experience..... alilipotosha bunge ya kuwa hilo linawezekana ndani ya katiba yetu jambo ambalo ulikuwa ni upotoshaji. Mhe. Samweli Sitta ndiye aliyeokoa jahazi pale alipotoa ufafanuzi sahihi kuwa katiba yetu inakataza upendeleo wowote ule wa kidini!!!!!!!!!
b) Kwenye suala la mauaji ya kikatili dhidi ya malbino majawabu yake yalikuwa kutoa machozi ya mamba na kujaribu kuturubuni kwa kusaka huruma zetu ambazo nazo si haba.............na haba haba hujaza kibaba. Hadi leo hajaweka mikakati yoyote zaidi ya kuwadhulumu waganga asilia haki yao ya kujitafutia kipato kwa kuwatupia lawama ambazo hazina ushahidi. Na ana bahati sana ya kuwa waganga tajwa hawakwenda mahakamani kumshtaki kwa kuwachafua majina yao na kuwazuia kujipatia kipato khalali.........
c) Kwenye suala la uwajibikaji wa watendaji serikalini baada ya kashfa ya Dowans/Richmond wakiwemo kibosile wa Takukuru; Dr. Hosea, Pinda amekuwa mstari wa mbele kukwamisha jitihada za bunge kuwawajibisha wakorofi tajwa hususani kibosile wa Takukuru ambaye bila ya aibu alilidanganya bunge na taifa kwa ujumla ya kuwa hakuna ufisadi kwenye richmond jambo ambalo Bunge kupitia kamati yake teule iliyoongozwa na Mwakyembe ilibaini vinginevyo. La ajabu hadi alipostaafu mwishoni mwa mwaka jana, Dr. Hosea aliendelea kutesa pale takukuru na hii inathibitisha Pinda si kiongozi mwenye dhamira ya kutoa maamuzi imara wakati yanapohitajika.
d) Kwenye sakata la katibu mkuu pale Wizara ya Nishati Pinda alitoa majibu yenye utata. Kwanza akiunga mkono hoja za wabunge kuwa mhusika alipaswa kuachia ngazi halafu baadaye akidai yeye siye mteuzi wa nyadhifa husika. Yeye mweyewe kwenye nafasi ya U-PM huhusika katika uteuzi wa nyadhifa zote serikalini lakini kwa sababu hana ushawishi wa kisiasa wa kutosha basi amekuwa akiegemea upepo kadri unavyomsukuma!!!!!!!!!!!
e) kushindwa kumshauri Raisi ya kuwa malalamiko ya wafanyakazi wote wa umma hususani ndani ya serikali kuu na serikali za mitaa yanatokana na kuwepo mihimili mingi ya kupanga masilahi ya wafanyakazi na Hazina kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria ya kuratibu mahitaji hayo. Katika khali hii taifa linaendelea kuyumba kutokana na kuwa na waziri mkuu asiye na uwezo kwa majukumu aliyopewa na JK kwa sababu za kujilinda nafsi yake. JK kama walivyo maraisi waliomtangulia hupendelea kuteua PM dhaifu ili kujilinda wao wenyewe wasifunikwe na PM chapakazi endapo angeliteuliwa.
Unafiki wa wazi.
Kama nilivyobaini hapo awali ni dhahiri Pinda ni mtaalamu wa unafiki na hutumia kauli za upole kuhadaa watu kuwa ni kiongozi mwaminifu na ambaye anajali masilahi ya taifa lakini ukweli lazima tuufichue ya kuwa Pinda ni mtaalamu wa kujali masilahi yake binafsi na ndiyo maana hawezi kushauri maamuzi ambayo yanatofautiana na bosi wake au ya wale anaowaona wako karibu na bosi wake.
Mapendekezo.
Wakati sasa umefika kujiuliza hivi JK na Pinda ni viongozi sahihi katika safu ya uongozi wa juu wa taifa hili? Nionavyo Pinda aonyeshe njia kwa kujitoa kafara khalafu JK aamue kusuka au kunyoa........................kwani hiki kitanzi cha kushindwa kurekebisha uchumi hakitamwacha salama...................utashangaa hivi sasa BOT wanazungumzia kuanzisha noti za 50,000/= na laki moja................................na huku baadhi ya watendaji waandamizi ndani ya BOT wanafikiria kupika muswada wa kufuta sifuri tatu kwenye sarafu yetu kama Zimbabwe walivyofanya na bila ya mafanikio zaidi ya kuitelekeza sarafu yao sasa wao ni US dola mtindo mmoja........................
Bye-bye Pinda & na JK wake...........................uchumi dororo ndiyo utawauumbua......
Point yako ni nini hasa? Ruta amekosea wapi? Nina mashaka hata topic yenyewe hukuisoma zaidi ya kusoma heading tu.Aiseee! umeamka asubuhi hii ukaona leo usipoandika kitu JF siku kwako haitaisha! Please rethink harafu urudi tena kutetea hoja yako.
Kikwete badala ya kushughulikia matatizo yanayoikabili nchi pamoja na matatizo ya migomo ya madaktari yeye anajishughulisha na misafara ya kutalii duniani, ni rais wa watanzania au ni waziri wa mambo ya nchi za nje?