Mapenzi na Pesa: Utata wa Uaminifu

Mapenzi na Pesa: Utata wa Uaminifu

Mwl.RCT

Platinum Member
Joined
Apr 5, 2009
Posts
15,595
Reaction score
22,334
Audio:

Chanzo:
Nilimsajilia line kwa jina langu, sasa nimegundua ananificha mwanaume mwingine... je, msamaha wake ni wa kweli?
Mwili wa Uzi:



Naomba msaada wa mawazo ya kweli kutoka kwa watu waliotulia na waliowahi kupitia maisha haya.

Niko kwenye mahusiano na dada mmoja ambaye nimekuwa naye kwa muda sasa. Kipindi fulani aliniomba nimsajilie line ya simu kwa jina langu kwa ajili ya kuhifadhi pesa lakini moyo ukawa unasita ni kama miaka 2 hv sasa week zilizo pita nikawa nime sajili ni ka mwambia line iko tayal lakin alikua bado ajaichukua , kwa sababu alisema anapata changamoto kwenye line zake. Nilimwamini, nikamsajilia line hiyo — na akaiweka pesa zaidi ya laki sita nk .Tsh 600,000.

Mpaka sasa line hiyo bado ipo kwenye simu yangu kwa sababu baada ya kutofautiana sikuweza kumpa. Sijaitumia hata shilingi, ila sasa najikuta nashindwa kuelewa kama niitumie, nimpatie au niifungie kwa usalama wangu wa kisheria na heshima yangu binafsi.

Leo amenitembelea nyumbani. Akiwa ananionyesha meseji kwenye simu yake, niliona jina la mwanaume mmoja kwenye inbox. Sikutilia maanani sana hadi aliponiomba simu yake, nikamkabidhi. Cha kushangaza, akaifuta haraka meseji ile ile niliyoiona.

Nilipomuuliza, mwanzo alikanusha. Baadaye akasema huyo jamaa ni mteja anayeleta pesa nyingi dukani kwao. Kwakua ananunua vitu vya paka hadi laki tatu 3 paka laki 4 Akasema jamaa huyo alikuwa anamfuata kimapenzi, lakini alikataa mara nyingi hadi akamkubalia ili amkamue hela— lakini anadai walikuwa hawapo kwenye mahusiano ya kweli

Nikaomba namba ya huyo mwanaume ili nijiridhishe lakini akakataa akisema ataniharibia biashara ya nyumbani kwao.

Kinachonisumbua zaidi ni kwamba:

✅ Mimi ndiye mwanaume wa kwanza kwake kimapenzi na kihisia.
✅ Nilimheshimu, nikampa nafasi ya maisha yenye heshima — hadi nikamfungulia line ya pesa kwa jina langu mwenyewe.
❌ Lakini sasa uaminifu umeanza kuwa na doa, na moyo wangu umechanganyikiwa.

Baada ya haya, alianza kupiga simu zaidi ya mara tano. Nilipopokea, akaanza kuniomba msamaha kwa uchungu. Anasema hajawahi kunichezea, ila alijikuta kwenye presha ya huyo mwanaume.

Lakini akili yangu inanieleza: msamaha wake ni wa kweli au ni wa kuokoa sura tu?
Na kuhusu hiyo line — je, nimuachie au nibaki nayo kwa usalama wangu?

Naomba mawazo ya wakuu — ya ukweli kabisa.
Nimejitahidi kuwa mkweli kwa upande wangu, bila kuongeza wala kupunguza.

Ahsanteni sana kwa ushauri wenu.
Naomba michango yenye tija na sio kubeza ilo tukio tu na solve vipi maana ana piga simu sikupokea baada ya apo anaomba msamah
 
Sheria ya wanaume kamili inakataza kuendelea na mahusiano na mwanamke ambaye tayari kaonesha hisia kwa mwanaume mwingine.Ikiwa wewe ni mwanaume kamili piga chini huyo malaya mpya.
Usimpe laini yako,toa pesa zilizopo kwenye line mkabidhi.
Ukiwa una akili timamu mueleze kuwa mahusiano yenu yameisha.
Endelea na maisha mengine.
Ukiwa bwege msamehe endelea kutunza na kuwekeza kwa malaya.
 
Back
Top Bottom