Mapendekezo ya CCM Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani

Mapendekezo ya CCM Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ameandika barua kwa Katibu Mkuu TAMISEMI ya tarehe 12 April 2013 ya kutaka waalimu wote wa sekondari na shule za msingi wazuiwe kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani.

Lengo kubwa la CCM kuamuru wazuiwe ni kwamba waalimu wana mgogoro na serikali hivyo kuna hofu ya kusaidia CHADEMA kwenye uchaguzi huo.

Badala yake CCM inapendekeza uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi huo ufanywe na Kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa. Kamati hizo za ulinzi na usalama zinaongozwa na wakuu wa wilaya na mikoa ambao kimsingi ni wajumbe wa kamati za siasa za CCM za wilaya na mikoa.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema endapo serikali itakubali pendekezo hilo la CCM basi itakuwa ni kitanzi kwa CHADEMA katika uchaguzi huo.

Source: Mawio
 
Binafsi nilipata taarifa kama miezi 6 iliyopita kutoka kwa mmoja wa viongozi wakubwa serikalini, ambaye alidai kwamba kulikuwa mkakati batili wa kuarisha uchaguzi wa serikali za mitaa/vijji mwaka 2014 kwa hoja kuwa serikali haina fedha za kutosha za kuuendesha uchaguzi huo. Lengo likiwa ni kuepusha aibu ya ccm kushindwa vijiji vingi na hivyo, kusababisha athari kubwa na mbaya kwenye uchaguzi wa 2015 kwa upande wa CCM.
kwa mujibu wa mtonyaji wangu,tatizo kubwa la mpango huo ni kama serikali itaeleweka kwa wananchi huku wakitarajia vyama vya upinzani kuupinga mpanga huo kwa kusema kuwa ccm wameogopa uchaguzi, kitu ambacho mtoa taarifa wangu anasema kingewaathiri zaidi badala ya kuwasaidia.

Hata hivyo, taarifa ziliandikwa ktk gazeti maarufu kufichua habari nzito nzito la mawio la Kila wiki (kila alhamisi) inayoonesha kuwa, mkakati wa kuahirisha uchaguzi unawatatiza na badala yake gazeti limefichua mikakati kadhaa batili yenye lengo kuhakikisha ccm inashinda uchaguzi huo kwa gharama yo yote. Gazeti lilimuuliza Tundu Lissu kuhusu Mikakati hiyo, naye akakiri kuifahamu vizuri.

Mikakati hiyo ya ccm ni pamoja viongozi wake kuandika kimya kimya barua (waraka?) yenye kumb No CMM/OND/626/VOL.111/44 kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI wakipendekeza mambo kadhaa ambayo ni dhahiri yanalenga kuhujumu uchaguzi huo. Mapendekezo hayo batili ni kama yafuatavyo;
A) CCM wamependekeza waalimu wasisimamie uchaguzi wa vitongoji na serikali za mitaa/vjiji kwa madai kwamba walimu wana mgogoro na serikali kuhusu maslahi yao.
B) Wamependekeza wananchi waombe nafasi hiyo ya kusimamia uchaguzi kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ( yaani mkuu wa wilaya/mkoa) ambaye pia mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm ya wilaya/mkoa?
C) CCM wamependekeza udhamini wa wagombea utolewe na viongozi wa ngazi husika – mgombea kitongoji au mtaa/kijiji adhamiwe na viongozi wa chama chake wa ngazi hiyo.
D) CCM pia wamependekeza wasimamizi hao wa uchaguzi wasiwasaidie watu wasiojua kusoma na kuandika badala yake mawakala wa vyama watumike kuwasaidia.
E) CCM wamependekeza muda wa kujiandikisha uwe siku 14 ( siyo 7) na mpiga kura awe amekaa ktk eneo husika kwa muda usiopungua miezi 3.

Gazeti gazeti lilitaka maoni ya CHADEMA kwa Tundu Lissu ambaye alimshauri mwandishi kumtafuta katibu mkuu Dr Slaa kujua msimamo wa CHADEMA. Hata hivyo, Tundu Lissu alipoulizwa kama anajua waraka huo alijibu, tulipokamata nyaraka za akina Asha Rose Migiro, Nape Nnauye, Mwigulu za kuchakachua mchakato wa katiba mpya, vile vile tulikamata mkakati wao wa kuchakachua uchaguzi wa 2014. Tundu Lissu aliendelea kusema, tunajua mipango ya CCM kuhakikisha inashinda uchaguzi wa 2014 hata ikibidi kuchakachua kura. Akaendelea, CHADEMA ni chama kikubwa kaka, tunajua wanchokifanya hatua kwa hatua, wenzetu wamejiandaa kuvuruga uchaguzi wa vitongoji na vijijj.
Kwa mujibu wa gazeti hilo,Tayari katibu mkuu wa TAMISEMI ameshawaandikia barua makatibu wakuu wa vyama vyote akitaka watoe maoni ya kuboresha uchaguzi wa 2014. Hata hivyo, kuombwa kwa maoni hayo, ni mkakati wa maandalizi ya kuchomeka mapendekezo hayo ya ccm kwenye mchakato wa uchaguzi ujao wa serikali vitongoji na mitaa/vijiji.


Maswali ninayojiuliza;
Kitendo cha kutaka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali wateuliwe na kada wa ccm kwa jina la mkuu wa wilaya siyo juhudi za wazi wazi za kuhujumu uchaguzi huo? Je, mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya yenye jukumu la kuhakikisha usalama wa ccm kisiasa ataacha kupendelea ccm kwa vile ni mkuu wailaya?

Pili, Kitendo cha ccm kutaka wagombea wadhaminiwe na ngazi husika, siyo kwamba ccm wanatarajia kuwa vyama vya upinzani havina uongozi ktk ngazi ya vijiji na vitongoji? Je huu siyo mkakati wa ccm kutaka kupita bila kupingwa kwa wagombea wa vyama vingine kukosa udhamini? Nadhani wamesahau kuwa CHADEMA iko mpaka ngazi ya vitongoji.

Tatu, Kwa nini ccm wanawakimbia walimu? Je, siyo kwamba CCM inataka uchaguzi huo usimamiwe na wananchi wa kawaida wakati lengo lao ni kuchomeka wanaccm kusimamia uchaguzi huo kupitia kwa kada wa ccm au mkuu wa wilaya ili waipendelee CCM?
Je CHADEMA tunapaswa kufanya nini kama jambo hili litatokea?


Nawasilisha.
 
Huu ni ujinga mwingine unaosambazwa na wapenda sifa za kijinga
 
Wao wazidi kuwakataa walimu tu, lakini wajue hata hao wanao itwa makada wao wengine sio wao, itafika wakati hawataamini macho yao, watajikimbia hata wao wenyewe, mwisho wao umefika, wawe wapole ili waondoke salama wakajipange vizuri kwa kizazi kijacho sio sasa.
 
Waache warukeruke tu na taulo kiunoni... Mwisho wake huwa ni aibu.....[ sasa nyie mtalaumu mpaka lini? Swali la msingi chadema wafanye ili kuepuka kuchakachuliwa? Badala ya kutoa pendekezo au kuonyesha njia unaanza kulalamika kwa kusema yana mwisho! Ni kweli yana mwisho lakini si hivi hivi lazima wananchi wafanye kitu,
 
Binafsi naona ni mkakati hatari lakini bahati nzuri umeshaangukia mikononi mwa makachero wetu! Ni wakati muhimu zaidi kwa chetu kuongeza nguvu za katika Idara ya usalama kuliko wakati mwingine wowote. Ccm hawawezi kushinda ujao hata ukimleta kipofu ataliona hilo lakini vile vile hawataondoka madarakani kirahisi tujiandae kwa mapambano! Kuikomboa nchi yetu kunahitaji kujitoa hata kama ni uhai wetu, mababu zetu wangekuwa waoga tungekuwa bado tuanatwaliwa na wakoloni. Walijitoa wakafa wakitetea nchi yao, sisi lazima tufuate nyayo kwa ajiri ya watoto na wajukuu zetu.
 
Maongezi yenu ya matukio ya kufikirika ambayo mmnayafanya kwenye vijiwe na vilabu vya pombe, msiyalete hapa na kutaka kutuaminisha kama ndiyo mkakati kitaifa.

Mkakati wa kuhujumu uko wapi hapo zaidi ya mapendekezo ya CCM yaliyopelekwa kwenye wizara inayohusika na usimamizi wa serikali za mitaa.MiCHADEMA niya ajabu kweli. Badala ya kupeleka mapendekezo yao, badala yake inaanza kulia lia na kulalamika.

Hizi preemptive reasoning zenu za kujiandaa baada ya kunyolewa kwenye sanduku la kura hata hazitosaidia.

Kuwapa watu muda wa 14 days kujiandikisha badala ya 7 days kwenu ni mkakati wa kuhujumu uchaguzi?. My foot.
 
Je huu siyo mkakati wa ccm kutaka kupita bila kupingwa kwa wagombea wa vyama vingine kukosa udhamini? Nadhani wamesahau kuwa CHADEMA iko mpaka ngazi ya vitongoji.

NA HAPA NDIPO NILIPO NA MASHAKA NAPO.....Ni kweli ipo hadi ngazi hii kwa kiasi hicho?
 
nakumbuka kauli ya mkuu kwa walimu :-
nione mtu ananyanyua pua yake kugoma walimu wakasema hatugomi ila tutagoma indirect way
 
Binafsi nilipata taarifa kama miezi 6 iliyopita kutoka kwa mmoja wa viongozi wakubwa serikalini, ambaye alidai kwamba kulikuwa mkakati batili wa kuarisha uchaguzi wa serikali za mitaa/vijji mwaka 2014 kwa hoja kuwa serikali haina fedha za kutosha za kuuendesha uchaguzi huo. Lengo likiwa ni kuepusha aibu ya ccm kushindwa vijiji vingi na hivyo, kusababisha athari kubwa na mbaya kwenye uchaguzi wa 2015 kwa upande wa CCM.

Narudia tena na tena kusema, hujawahi hata siku moja kuleta kitu cha maana humu jamvini, zaidi ya uzushi na maneno yakusadikika kuliko ukweli halisi. Nawasilisha.
 
Wanachosahau ccm ni kwamba ndani ya systeam tayari kuna watu wameshawachoka na upuuzi wao wanachofanya kila wakipambanga mbinu zao watu wanazidaka wanazipeperusha hewani..Muhimu ccm watekeleze ahadi zao tu kwa wananchi tu na si ujanja ujanja wao!
 
Back
Top Bottom