Mapendekezo ya CCM Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani

Mapendekezo ya CCM Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani

Binafsi nilipata taarifa kama miezi 6 iliyopita kutoka kwa mmoja wa viongozi wakubwa serikalini, ambaye alidai kwamba kulikuwa mkakati batili wa kuarisha uchaguzi wa serikali za mitaa/vijji mwaka 2014 kwa hoja kuwa serikali haina fedha za kutosha za kuuendesha uchaguzi huo. Lengo likiwa ni kuepusha aibu ya ccm kushindwa vijiji vingi na hivyo, kusababisha athari kubwa na mbaya kwenye uchaguzi wa 2015 kwa upande wa CCM.
kwa mujibu wa mtonyaji wangu,tatizo kubwa la mpango huo ni kama serikali itaeleweka kwa wananchi huku wakitarajia vyama vya upinzani kuupinga mpanga huo kwa kusema kuwa ccm wameogopa uchaguzi, kitu ambacho mtoa taarifa wangu anasema kingewaathiri zaidi badala ya kuwasaidia.

Hata hivyo, taarifa ziliandikwa ktk gazeti maarufu kufichua habari nzito nzito la mawio la Kila wiki (kila alhamisi) inayoonesha kuwa, mkakati wa kuahirisha uchaguzi unawatatiza na badala yake gazeti limefichua mikakati kadhaa batili yenye lengo kuhakikisha ccm inashinda uchaguzi huo kwa gharama yo yote. Gazeti lilimuuliza Tundu Lissu kuhusu Mikakati hiyo, naye akakiri kuifahamu vizuri.

Mikakati hiyo ya ccm ni pamoja viongozi wake kuandika kimya kimya barua (waraka?) yenye kumb No CMM/OND/626/VOL.111/44 kwenda ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI wakipendekeza mambo kadhaa ambayo ni dhahiri yanalenga kuhujumu uchaguzi huo. Mapendekezo hayo batili ni kama yafuatavyo;
A) CCM wamependekeza waalimu wasisimamie uchaguzi wa vitongoji na serikali za mitaa/vjiji kwa madai kwamba walimu wana mgogoro na serikali kuhusu maslahi yao.
B) Wamependekeza wananchi waombe nafasi hiyo ya kusimamia uchaguzi kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ( yaani mkuu wa wilaya/mkoa) ambaye pia mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm ya wilaya/mkoa?
C) CCM wamependekeza udhamini wa wagombea utolewe na viongozi wa ngazi husika – mgombea kitongoji au mtaa/kijiji adhamiwe na viongozi wa chama chake wa ngazi hiyo.
D) CCM pia wamependekeza wasimamizi hao wa uchaguzi wasiwasaidie watu wasiojua kusoma na kuandika badala yake mawakala wa vyama watumike kuwasaidia.
E) CCM wamependekeza muda wa kujiandikisha uwe siku 14 ( siyo 7) na mpiga kura awe amekaa ktk eneo husika kwa muda usiopungua miezi 3.

Gazeti gazeti lilitaka maoni ya CHADEMA kwa Tundu Lissu ambaye alimshauri mwandishi kumtafuta katibu mkuu Dr Slaa kujua msimamo wa CHADEMA. Hata hivyo, Tundu Lissu alipoulizwa kama anajua waraka huo alijibu, tulipokamata nyaraka za akina Asha Rose Migiro, Nape Nnauye, Mwigulu za kuchakachua mchakato wa katiba mpya, vile vile tulikamata mkakati wao wa kuchakachua uchaguzi wa 2014. Tundu Lissu aliendelea kusema, tunajua mipango ya CCM kuhakikisha inashinda uchaguzi wa 2014 hata ikibidi kuchakachua kura. Akaendelea, CHADEMA ni chama kikubwa kaka, tunajua wanchokifanya hatua kwa hatua, wenzetu wamejiandaa kuvuruga uchaguzi wa vitongoji na vijijj.
Kwa mujibu wa gazeti hilo,Tayari katibu mkuu wa TAMISEMI ameshawaandikia barua makatibu wakuu wa vyama vyote akitaka watoe maoni ya kuboresha uchaguzi wa 2014. Hata hivyo, kuombwa kwa maoni hayo, ni mkakati wa maandalizi ya kuchomeka mapendekezo hayo ya ccm kwenye mchakato wa uchaguzi ujao wa serikali vitongoji na mitaa/vijiji.


Maswali ninayojiuliza;
Kitendo cha kutaka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali wateuliwe na kada wa ccm kwa jina la mkuu wa wilaya siyo juhudi za wazi wazi za kuhujumu uchaguzi huo? Je, mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm wilaya yenye jukumu la kuhakikisha usalama wa ccm kisiasa ataacha kupendelea ccm kwa vile ni mkuu wailaya?

Pili, Kitendo cha ccm kutaka wagombea wadhaminiwe na ngazi husika, siyo kwamba ccm wanatarajia kuwa vyama vya upinzani havina uongozi ktk ngazi ya vijiji na vitongoji? Je huu siyo mkakati wa ccm kutaka kupita bila kupingwa kwa wagombea wa vyama vingine kukosa udhamini? Nadhani wamesahau kuwa CHADEMA iko mpaka ngazi ya vitongoji.

Tatu, Kwa nini ccm wanawakimbia walimu? Je, siyo kwamba CCM inataka uchaguzi huo usimamiwe na wananchi wa kawaida wakati lengo lao ni kuchomeka wanaccm kusimamia uchaguzi huo kupitia kwa kada wa ccm au mkuu wa wilaya ili waipendelee CCM?
Je CHADEMA tunapaswa kufanya nini kama jambo hili litatokea?


Nawasilisha.

Asante kwa maelezo yako ya kina.
 
Basi ccm iwalipe walimu madai yao ili warudishe mapenzi yaliyopotea.
Yani haya maccm yanafikiria madaraka bila kujali njia ama mbinu wanayotumia hata iwe haramu ya kuua watu watafanya hivyo ilimradi yabaki madarakani.

Shame on you gambaz.
 
Haa kumbe!! Naacha ualimu nakujiunga na ccm ili nishiriki uchaguzi, nape naomba kadi ya kuambatanisha kivuli chake kwny barua yangu ya kuomba kusimamia.
 
hii ni hofu ya chadea baada ya kuona wanazidiwa siasa sasa wanaendelea ku pre empty mambo...kesi ya ugaidi na ulishaji watu sumu na utekaji inawatafuna
mara zote ccm hawawezi kutoa pendekezo la kulisaidia taifa kama taifa kiujumla wake, wao kazi kutoa mapendekezo yatakayoibeba ccm tu na si taifa, chukulia mfano suala la katiba mpya, ccm wameiteka tume ya warioba ili itengeneze mfumo wa mabaraza ya katiba kwa kuingiza Wdc, ili waingie wanaccm peke yao, binafsi sina imani kama ccm wanalipenda taifa letu kwa moyo wa dhati kabisa!
 
WaTZ sisi nyenzo ni UCHAGUZI taratibu zake zikibakwa hivyo inavyoandaliwa watatujua! Tuko kimya kwa vile muda wa kuchinja umewadia. Other wise...or!!!
 
Huu ni ujinga mwingine unaosambazwa na wapenda sifa za kijinga

Ungeeleweka kama ungetoa ushahidi kuthibitisha huo "ujinga" wao kama mtoa maada alivyofanya hadi akatoa reference ya barua husika.
 
Back
Top Bottom