Mapendekezo! Vyama vya siasa vifutwe vyote vinaliangamiza Taifa

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,314
10,017
Wanabodi,

Katika nchi yetu tumekuwa na mfumo wa kupata viongozi vya kisiasa kupitia mfumo wa vyama vya siasa na katiba yetu hairuhusu wala kutambua mgombea asiye na chama cha siasa.

Nimekuja hapa nikiwa na mawazo tofauti ambapo nimeweka katika mizania faida na hasara ya uwepo wa vyama vya siasa nimegundua hasara ni nyingi zaidi kuliko faida.

Tumekuwa tukipata viongozi wetu kutoka ndani ya vyama vya siasa hali hii imetuletea matabaka katika vyombo vya maamuzi kuanzia serikali za mitaa mpaka bungeni. Viongozi wanaotokea chama fulani wamekuwa na maelewano na kushirikiana na viongozi wenzao kutoka chama kimoja jambo ambalo si afya kwa maendeleo ya taifa.

Kumekuwa na tabia ya hawa viongozi tunaowapata kutoka vyama vya siasa kutanguliza maslahi ya vyama vyao kuliko maslahi ya taifa. Aghalabu tumeshuhudia wabunge wa CCM wakiitetea serikali katika mambo ambayo yanastahili kukemewa hii ni kwa vile tu serikali ni ya chama chao. Hii ni hasara kubwa kwa taifa na inapunguza uwajibikaji wa serikali.

Vyama vya siasa havina msaada katika kukemea mwenendo mbaya na maadil ya kiutumishi wa makada wao ambao ni viongozi wa umma. Wabunge na hata madiwani wengi utendaji wao wa kazi umekuwa wa kusikitisha na mara nyingine wanatelekeza majimbo yao na kuonekana kwa nadra hadi uchaguzi ukikaribia lakini vyama vya siasa hivi vimekuwa hutaona chama kikimuonya au kumuwajibisha mwanachama wao ambaye ni kiongozi kwa kutotimiza wajibu wake kwa wananchi. Unaweza kusema kazi ya kuwawajibisha wawakilishi wa wananchi ni ya wananchi wenyewe kupitia sanduku la kura lakini je vyama vya siasa vina kaz gani baada ya uchaguzi? Mbona vinaendelea kupokea ruzuku?

Uwepo wa vyama vya siasa unavuruga umoja na mshikamano wa wananchi. Wananchi wanagawanyika kutokana na itikadi hizi za uCCM na UCDM hali hii hailisaidii taifa bali inaliangamiza. Tumesikia mara nyingi watu wakiumizana hadi kuuwana kwa sababu itikadi za kisiasa.

JE VYAMA VYA KISIASA VIKIFUTWA TUTAPATAJE VIONGOZI?
Napendekeza mfumo wa kura za maoni utumike kupata wagombea binafsi katika chaguzi katika ngazi zote.

Mathalani katika ngazi ya mtaa wananchi watapendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kugombea uenyekiti wa kijiji. Baada ya kupatikana majina kadhaa basi waliopendekezwa watapewa muda wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea. Wao wenyewe watatafuta wadhamini .

Lakini kwa mtu ambaye ana nia ya kugombea uchaguzi na jina lake halijatwa na wananchi atakuwa na haki ya kugombea lakini itabidi awe na wadhamini mathalani kwa mwenyekiti wa kijiji wadhamini 10. Wagombea waliopendekezwa na wanachi watachukua fom za kugombea bure lakini wagombea ambao hawakupendekezwa watachukua fom kwa malipo.

Ngazi ya Udiwani uwe huo huo wa wananchi kupendekeza majina ya watu wanaoona wanafaa kugombea na mtu mwenye nia ya kugombea na hajapendekezwa achukue fom kwa malipo.

Ngazi ya ubunge wanyeviti wa vitongoj ndio watapendekeza majina ya wanaoona wanafaa kugombea. Watapendekea mtu yeyote yule mwenye sifa zinazotajwa na katiba isipokuwa sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa itaondolewa. Mtu binafsi ataruhusiwa kugombea kwa utaratibu uliotajwa juu.

Ngazi ya Urais. Wabunge watapendekeza majina na mtu mwenye nia ya kugombea na hajapendekezwa (mgombea binafsi) utaratibu utakuwa huo huo uliotajwa juu.

Kwa namna hii tutapata viongozi bora zaidi , tutaondokana na mipasho bungeni, mambo ya uchama hayatakuwepo bungeni na masuala ya ruzuku kwa vyama vya siasa yataondoka na vile vile tume ya uchaguzi na polisi wataondolewa majaribuni.

NAWASILISHA.
 
Upuuzi mtupu kutoka kwa mpuuzi wa kawaida. Kutetea serikali ndiyo kutetea taifa?
Serikali iliyotetewa kipindi kile ilikuwa ni Chama gani? Na iliteteqa na wabunge wa Chsma gani? Serikali ya Kipindi hiki inayojaribu kila siku kuinyesha serikali iliyopita ilikuwa failed na corruote ni ya Chama gani na inatetewa na wabunge wa Chama gani?
 
Hilo wazo lako mtu akikulupuka kulisoma juujuu atamwaga povu lakutosha.ila kiundani na kiuhalisia linamaana.hoja zimejijenga.
Atakaye kuja kuupinga huu uzi aje na hoja za maana, maana hoja hupingwa kwa hoja.
 
CCM kimelitafuna taifa hili, wakati tunajichukulia Uhuru nchi hii ilikuwa na uchumi wa kati

CCM ikatupeleka kwenye uchumi wa kugombania kilo ya sukari ndani ya miaka michache tu

Sasa hivi ati wanajifanya wanataka kutupeleka kwenye uchumi wa kati hahaha!!

Mleta mada amekatishwa tamaa na siasa za vyama kutokana alichokiona

Ukweli ni kwamba tubadilishe Vyama CCM imeshindwa

Chadema kiko serious tukipe japo Awamu ya tano
 
Hivyo vyama vililetwa na wazungu kuja kutuvuruga tu na kura kodi zetu,kiukweli havifai ,jiulize kila hao mabeberu wanapojifanya kuingilia mataifa kutetea demokrasia ndio wanaangamiza kabisa hayo Mataifa
Waafrika watuache na tamaduni.zetu tu
 
Mleta mada una hamu ya kuona mabadiliko kwa kuondoa vyama vya siasa lakini umeshindwa kuonesha hao wapiga kura watakuwa-organized vipi. Unasema tu wanapendekeza majina. Vyama vya kijamii ndio mfumo pekee (katika kujaza nafasi za umma kupitia uchaguzi) ambao unaruhusu wananchi kuwa organized na kushindana. Bila vyama vya kijamii katika siasa ndio vyama vya siasa.

Ungeshauri tuwe na mfumo wa kuchagua unaoganya tuchague mkuu wa wilaya, na mbunge kama muwakilishi wa wilaya (sio jimbo) ingeleta maana sana!! Nchi ingekuwa katika mazingira ambayo ingewezekana mkuu wa wilaya ni wa chama A na mbunge ni wa chama B. Ni katika mazingira hayo tungejali maswala ya wananchi badala ya vyama.

Katika hali ya sasa, siasa zinafanywa ktk ngazi ya kitaifa na kuathiri utendaji wa halmashauri na kuathiri maendelea ya wananchi huku umuhimu wa vyama ukitamalaki. Sera ya serikali za majimbo ilikuwa sahihi!! Serikali kuu ingeshughulika na mambo ya kitaifa wakati maswala ya wananchi yangeshughulikiwa ngazi ya jimbo. Ni aibu Rais kuambiwa habari za matundu ya choo ya shule iliyo chini ya halmashauri.
 
Upuuzi mtupu kutoka kwa mpuuzi wa kawaida. Kutetea serikali ndiyo kutetea taifa?
Serikali iliyotetewa kipindi kile ilikuwa ni Chama gani? Na iliteteqa na wabunge wa Chsma gani? Serikali ya Kipindi hiki inayojaribu kila siku kuinyesha serikali iliyopita ilikuwa failed na corruote ni ya Chama gani na inatetewa na wabunge wa Chama gani?

Sijajua umetoa wapi hayo uyasemayo maana hayapo kwenye thread content
 
Hivyo vyama vililetwa na wazungu kuja kutuvuruga tu na kura kodi zetu,kiukweli havifai ,jiulize kila hao mabeberu wanapojifanya kuingilia mataifa kutetea demokrasia ndio wanaangamiza kabisa hayo Mataifa
Waafrika watuache na tamaduni.zetu tu
Mleta mada anasema hadi CCM kifutwe,naona umekurupuka!Mleta mada katia mchanga ugali wako!
 
Ni sawa,lakini pia mali zilizopatikana chini ya mfumo wa chama kimoja zirudishwe serikalini!
Yes hili naliunga mkono na niliwahi kushauri
Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa!

Nilisema
Wanabodi,
Ili Tanzania Ibarikiwe, Magufuli Asiishie Kwenye Shule Tuu, Arejeshe Mali Zote Za Umma Zilizoporwa, kuibiwa na kuhodhiwa na Yeyote!.

Rais Magufuli amejipambua kuwa ni mkweli na ni mtenda haki, kwa wema huu tuu alioshalitetea taiFa hili tangu ashike madaraka, kiukweli tayari Mungu ameisha mbariki na anaendelea kumbariki, na ili kuongeza nguvu za neema kutiririka, tunamuomba afanye tathmini ya kina, ni mali gani ambazo CCM inazimiliki kihalali, na ni mali gani CCM inazimiliki isivyo halali, zile za halali zibaki CCM na zile ambazo sio halali zirudishwe serikalini.

Nikimaanisha ni mali za wizi, ambazo CCM ili zi loot kutoka kwa Watanzania, then kwa zile mali zake halali, CCM iendelee kuzimiliki, na zile mali za jasho la Watanzania, zikiwemo mashule, viwanja mbalimbali, majengo na maeneo ya wazi ambayo CCM imepora virudishwe serikalini kuwa mali ya umma wa Watanzania, kwa kufanya hivyo, Magufuli, ataendelea kubarikiwa sana na sana, CCM nayo itabarikiwa na Tanzania kwa ujumla Itabarikiwa.

P
 
Back
Top Bottom