Mapendekezo kuhusu masoko ya Machinga

kipenseli2021

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
831
783
Habari za majukumu ndugu zangu wa JamiiForums kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya nguvu na afya tele na jinsi anavyo zidi kutupigani kwenye kanga hili la Covid 19 au UVIKO 19 wimbi la Tatu

Pili nitoe pongezi kwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia H Suluhu na watendaji wake wote
Wanapendwa kitu kilicho nipelekea kushika karamu na kuandika mambo hayo japo kwa ufupi ni kuhusu Wamachinga/wafanya baishara wadogo

Wamachinga/Mmachinga ni nani?
Mmachinga ni neno japo sio rasmi Ila linatumika kuwatambulisha wafanya biashara wadogo wadogo ambao kwa zamani ilizoelekea kuwa wengi wanatoka Mikoa ya kusini (Lindi na Mtwara)

Chinga ni jina linalo mtambulisha kijana au msichana au mfanya biashara mdogo mdogo anajishughulisha na ununuzi na uuzaji wa bidhaa ndogo ndogo kama viatu, mikoba, nguo nk

Lakini wamachinga wanakumbana na changamoto hasa hasa ya kufanya biashara katika maeneo ambayo yanakuwa sio rasmi hivyo kupata shida ya kufukuzwa na mgambo tangu enzi hizo

Lakini serikali inachukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa wamachinga wanafanya biashara zao kwa amani na upendo pasipo kusumbuliwa na mgambo wa jiji

Swali langu ni moja Je Machinga Complex, Mwanjelwa Complex na Miradi au Masoko mengine yanayo fanana hivyo yalijengwa kwa ajili ya Machinga au. Jibu kama ndiyo Basi nasema hapakufanyika uchambuzi yakinifu hasa hasa kuhusiana na nani anaye kuja kufanya biashara hapo. Siku zote unapofanya mradi ni lazima ulete au uongeze thamani ya biashara au kukidhi mahitaji ya taasisi/watu/mlengwa

PENDEKEZO
Kama hizi complex lengo lake ni kwa ajili ya Machinga /Wafanya biashara wadogo wadogo
Napendekeza yafuatayo:

1: Yasiwe ya Majengo ya ghorofa kama haya yaliyo jengwa
2: Yawe ya chini na yawe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya wateja kuweza kupita bila usumbufu
3: Vibanda viwe vya wazi
4: Vigawanyike kulingana na aina ya bidhaa mfano yawe kwenye mpangilio kufuatana na aina ya bidhaa inayopatikana kama viatu nk
5: Yajengwe kwenye maeneo ambayo yanawapita njia wengi
6: Eneo liwe kubwa na wazi

Mapendekezo haya yanatokana na nature ya wamachinga. Kwa haya majengo ya complex haya yanawafaa wafanyabiashara au mfanyabiashara mkubwa ambaye anaweza kodi lote na kuweka biashara zake

Asante
 
Back
Top Bottom