Yohana Kilimba
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 8,105
- 5,635
Tunasubiria Ripoti ya Mapato ya Mwezi Juni
Ripoti ya mwezi wa sita imetoka vipi umeshaipata? AhahahaTunasubiria Ripoti ya Mapato ya Mwezi Juni
MALENGO YAPI KAKA WAKATI TAKWIMU HAZIJWAHI KUSIMAMA SAWA..! MAANA KILA MWEXI KUNA KUNA KUWA NA MABADILIKO..! LAKN PIA KUMBUKA LENGO LIKIWEKWA HATUAMBIWI NI ASILIMIA NGAPI HAYA MANENO YA TUMEVUKA LENGO HUJA BAADA HAPA KUNA SIASA..! WATANGAZE MALENGO YAO HATA YA MWAKA WATU TUWE NA TAKWIMU ALAFU TUWE TUNALINGANISHA KILA MWEZI CO WATU WANAJIFUNGIA NDANI ALAFU WAKITOKA WANAANZA KUIMBA "TUMEVUKA LENGO" HAPA KUNA KITU GANI KINAWEZA KUWA KIELELEZO CHA WATU KUAMINI..???Mkuu, hizo ni hisia zako tu ila ukweli unabaki kwamba TRA wanakusanya mapato kwa kuvuka malengo yao
TUNASUGUA NA KUISOMA WOTE MBONA MKUU..!Endeleeni kujiaminisha hilo. Mtasugua sana maana Magufuli ni Rais hadi 2025
Roho mbaya zenu hizi ni laana ya kubadili gia angani inawatafuna.TUNASUGUA NA KUISOMA WOTE MBONA MKUU..!
Kumekuwa na maporomoko makubwa ya mapato ya TRA kutoka trilioni moja na bilioni mia nne Mwaka Jana wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mpaka trilioni moja mwezi wa tano.Ni wazi mwezi wa sita TRA watatangaza mapato ya bilioni 900. Tunarudi kulekule kwa JK.
Ni ishara kwamba JK hakuwa mzembe bali mapato yalienda na upepo wa biashara,mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna wizi sijui wapi,sasa mbona na udhibiti wote ndani ya miezi sita mapato yameshuka kwa bilion 400? Zinakwenda wapi?zimepotelea wapi?
Kuna mtu Mwenye ubavu wa kuzikosoa jitihada za Kikwete kwenye kukusanya mapato na aamke nimuone.
Kumekuwa na maporomoko makubwa ya mapato ya TRA kutoka trilioni moja na bilioni mia nne Mwaka Jana wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mpaka trilioni moja mwezi wa tano.Ni wazi mwezi wa sita TRA watatangaza mapato ya bilioni 900. Tunarudi kulekule kwa JK.
Ni ishara kwamba JK hakuwa mzembe bali mapato yalienda na upepo wa biashara,mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna wizi sijui wapi,sasa mbona na udhibiti wote ndani ya miezi sita mapato yameshuka kwa bilion 400? Zinakwenda wapi?zimepotelea wapi?
Kuna mtu Mwenye ubavu wa kuzikosoa jitihada za Kikwete kwenye kukusanya mapato na aamke nimuone.
Mkuu sasa ndiyo tunaona na kuamini kuwa ilikuwa ni nguvu ya sodaKumekuwa na maporomoko makubwa ya mapato ya TRA kutoka trilioni moja na bilioni mia nne Mwaka Jana wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mpaka trilioni moja mwezi wa tano.Ni wazi mwezi wa sita TRA watatangaza mapato ya bilioni 900. Tunarudi kulekule kwa JK.
Ni ishara kwamba JK hakuwa mzembe bali mapato yalienda na upepo wa biashara,mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna wizi sijui wapi,sasa mbona na udhibiti wote ndani ya miezi sita mapato yameshuka kwa bilion 400? Zinakwenda wapi?zimepotelea wapi?
Kuna mtu Mwenye ubavu wa kuzikosoa jitihada za Kikwete kwenye kukusanya mapato na aamke nimuone.
Mwezi wa sita chaaliiiiiiMkuu, hizo ni hisia zako tu ila ukweli unabaki kwamba TRA wanakusanya mapato kwa kuvuka malengo yao
ya kupikwa. reality will catch up with you people soon!Mkuu, mapato yamefikia 1.4 trilion kwa mwezi June 2016. Vipi yameongezeka au yamepungua.
Kipi ni kizuri kwako, yashuke au yakipanda.
Kuna akili zingine za ajabu sana, inaelekea unafurahi sana ukiona yanshuka.
Tunasugua wote bila kujali rangi za chama, na walio wengi ni kijani jembe na nyundo ndio wanaipataEndeleeni kujiaminisha hilo. Mtasugua sana maana Magufuli ni Rais hadi 2025
Hiyo haipo mbali na usishangae watakwambia kuwa ukawa ndio wameombea mapato kushukaSasa waje watwambie bilioni 400 zimekwenda wapiii?? Na kwa jinsi mambo yalivyo tutafika hata makusanyo ya bilioni 800,biashara zinakufa sana
Asante sana mkuuHaaa. Lumumba moja iyoo. Hta kama akiwa raic milele kama mseven hakuna shida. Naomba turudi kwenye point ya mapato TRA.
Mapato ya june 1.4trl Leta jingine au uufyate.Mbona ttz inaongeza idadi ya mataila wengi kama nyie? Kisa kikwete alikaa had 2015 so ni haki magu akae 2025? Wewe unajua hta maana ya "haki" kweli????
Kwanza hoja apa ni mapato kushuka msianze kupotezea mada husika.
Jipya unalo wewe, nimwendo wa kushuka tu au kuporomoka, nimeamini kikwete aliweza sanaHuna jipya
Tunataka makusanyo ya mwrzi wa sita na siyo ngonjeraTRA YAVUKA LENGO LA MAKUSANYO YA KODI KWA MWEZI MEI 2016
![]()
MKamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata akitilia mkazo jambo wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwezi Mei 2016,kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe.
*******************
MAMLAKA ya Mapato Tanzania imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.032 katika mwezi Mei ambayo ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.025 katika mwezi huo.
Makusanyo ya kipindi cha miezi kumi na moja (Julai 2015 hadi Mei 2016) ni jumla ya shilingi trilioni 11.956 sawa na asilimia 99.2 ya lengo la shilingi trilioni 12.054 katika lengo la kipindi hicho kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata amesema TRA inaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha inafikia na kuvuka lengo la makusanyo iliyopangiwa na serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka katika ukusanyaji wa mapato.
“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha, ambapo kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo hususani katika pwani ya bahari ya Hindi na mipaka yote, kupambana na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi na wanaokiuka kutumia mashine za kodi za keielektroniki , kuwawajibisha wafanyakazi wasio waadilifu pamoja na kuhakikisha inaboresha zaidi mifumo itakayompa urahisi mlipakodi katika zoezi zima la ulipaji kodi wa hiari, alisema Kamishna Mkuu.
Bw. Kidata ameendelea kusisitiza wananchi na wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kutoa na kudai risiti za EFD pindi wanaponunua au kuuza bidhaa pamoja na huduma ili kuongeza mapato ya nchi.
Katika kutekeleza agizo la Mh. Rais na kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa ushirikiano katika matumizi ya mashine za EFD Mamlaka imeanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wadogo kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
TRA imeanza ugawaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara wapatao 5,703 wenye mauzo ghafi kati ya Shilingi milioni 14 na milioni ishirini (20) kwa mwaka, wafanyabiashara hao wanatakiwa wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato za Mikoa wanayolipia kodi ya Ilala, Kinondoni na Temeke ili waweze kuhakiki usajili wao wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) na kupewa kibali cha kupewa Mashine ya EFD zoezi lililoanza Juni Mosi alisisitiza Kamishana Mkuu.
Aidha, Bw. Kidata alifafanua kuwa zoezi hili litaendelea katika Mikoa yote Tanzania kwa awamu kwa utaratibu utakaotangazwa mara kwa mara na hivyo kutoa wito kwa wafanyabiashara wenye mauzo tajwa wote nchini kutoa ushirikiano pindi inapofika zamu yao katika Mikoa yao.
Zoezi hili litasaidia kuongezaka kwa Mapato ya nchi endapo wafanyabiashara na wananchi watakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha wanatumia mashine hizo na kutoa taarifa kwa Mamlaka kuhusu wafanyabiashara wote watakao kiuka kutumia mashine hizo za EFD.
Kwa upande wa wananchi, kamshna mkuu amewaasa kuadai risiti kila wanunuwapo bidhaa au kupata huduma na kuhakikisha usahihi wa kiwango walicholipia sambamba na risiti walizopewa
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu"
Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Nimwendo wa kurudi chini tuSasa kuna hoja gani hapo? Hata kama tutakusanya bilioni 200 si ndiyo mapato ya mwezi? Kikubwa zaidi ni namna fedha hizo zitakavyotumika
Reality ipi tena? Reality si ndio hiyo mapato ta june 1.4 trl?ya kupikwa. reality will catch up with you people soon!
I worriedly smell our own "Nkurunziza" in the making.