Mapato ya TRA mwezi Juni yatashuka

Mapato ya TRA mwezi Juni yatashuka

Bajeti tuliyonayo ni ya Kikwete. Ya Magufuli itaanza tarehe 1 july 2016. Ukitaka kumpima Magufuli mpime kwenye makusanyo ya July mwaka huu.
Bajeti tuliyonayo ni ya Kikwete. Ya Magufuli itaanza tarehe 1 july 2016. Ukitaka kumpima Magufuli mpime kwenye makusanyo ya July mwaka huu.
Siongelei bajeti....naongelea revenue collection..makusanyo,soma vizuri wewe killa.za
 
Si swala la lumumba. Kikwete alikaa vipindi viwili. Ni haki Magufuli akae mpaka 2025 amalize majipu.
Mbona ttz inaongeza idadi ya mataila wengi kama nyie? Kisa kikwete alikaa had 2015 so ni haki magu akae 2025? Wewe unajua hta maana ya "haki" kweli????

Kwanza hoja apa ni mapato kushuka msianze kupotezea mada husika.
 
TRA ni wajanja wanaweka makadirio madogo ili waweze kuvuka makadirio yao.Ni kwanini makusanyo yanazidi kupungua mwezi baada ya mwezi? kama awatuhadai wangetakiwa waweke malengo makubwa kuliko mwezi wa mwisho kukusanya mapato.Mfano Mei wamekusanya trillion 1.02 malengo ya mwezi june yanatakiwa yazidi mapato ya mwezi may.
Lakini wanatuhadaa kwa kupunguza kiwango.
Makusanyo yatapandaje wakati uchumi unashuka.TRA wapo sawa maana wanapanga kulingana na hali halisi ya uchumi inavyoenda.Uchumi unazidi kudoda kwa hiyo lazima na makadirio yawe yanashuka chini.Hiyo ni direct proportion sion inversely proportion
 
Kumekuwa na maporomoko makubwa ya mapato ya TRA kutoka trilioni moja na bilioni mia nne Mwaka Jana wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mpaka trilioni moja mwezi wa tano.Ni wazi mwezi wa sita TRA watatangaza mapato ya bilioni 900. Tunarudi kulekule kwa JK.

Ni ishara kwamba JK hakuwa mzembe bali mapato yalienda na upepo wa biashara,mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna wizi sijui wapi,sasa mbona na udhibiti wote ndani ya miezi sita mapato yameshuka kwa bilion 400? Zinakwenda wapi?zimepotelea wapi?

Kuna mtu Mwenye ubavu wa kuzikosoa jitihada za Kikwete kwenye kukusanya mapato na aamke nimuone.
Wewe unaombea/unalazimisha mapato yashuke
Mwezi wa sita pia ni mwisho wa mwaka kodi nyingi zinakusanywa,labda maombi yako yatafanikiwa mwezi wa nane inshaallah
 
Mkuu, hizo ni hisia zako tu ila ukweli unabaki kwamba TRA wanakusanya mapato kwa kuvuka malengo yao
Saa nyingine huwa nashindwa hata kukuelewa mkuu. Mtu kaja na mchanganuo wa jinsi mapato yanavyopungua we unajibu kirahis rahis tu. Njaa ikizid sana utafikiria kwa Tumbo mkuu badala ya kichwa
 
Nilishasema hapa serikali ilifikia kukusanya 1t mwezi Dec na January tu, miezi mingine ni maigizo tu makusanyo yanapikwa kumfurahisha mfalme, biashara zimeshuka mno matajiri wamepaki magari kabisa, bandarini kweupee hizo kodi zinakusanywa toka wapi?
Subiri mpaka bajeti ijayo kodi ya kichwa inarudi mtaona
 
Makusanyo yatapandaje wakati uchumi unashuka.TRA wapo sawa maana wanapanga kulingana na hali halisi ya uchumi inavyoenda.Uchumi unazidi kudoda kwa hiyo lazima na makadirio yawe yanashuka chini.Hiyo ni direct proportion sion inversely proportion
Ndio maana nimesema wanatudanganya wakisema wanavuka lengo.Wanatakiwa kutumia makusanyo ya mwezi uliopita kama kiwango chao cha chini.
Na bado awatoi mchanganuo wa mwezi uliopita kwa kusema mwezi uliopita tulikusanya kiasi ichi na mwezi huu tumekusanya kiasi ichi, na tofauti ni kiasi flani.Na waseme makusanyo yamepungua au yameongezeka.
 
Umejuaje kuwa yatakuwa bilioni 900? Unalinganisha na kipindi cha jk kwa upeo upi sasa ulionao? Ila kuna watu mnapiga sala mioyoni mwenu ili magufuli ashindwe katika uongozi wake, mmesahau kuwa nanyi ni watanzania
Hayo makadirio yako hayaainishi sababu za kushuka kwa mapato hayo!!
 
Natofautiana na JPM kwa vitu vingi sana na sipendi kabisa alivyolitendea bunge.
Natofautiana na Dr. Waziri wa fedha kwa kutuleta namba ambazo sijui hata alikozipata huku akitaka tuziamini.
Cha msingi ni kwamba hata walioendelea iliwachukua zaidi ya kizazi kimoja kufanikisha kitu, mfano ukisema elimu ya Scandinavia ni nzuri inabidi kujua kuwa hawakufanikisha hilo kwa kufanya BRN ya kupeleka watoto wa form IV kusomea degree za ualimu bali huenda ilikuwa ni mipango iliyogharimu kizazi kizima au viwili. Nchi zilizoendelea na kufanikisha mambo hawakutumia mipango kama ya ccm ya 'barabara za disposable' ili kuonyesha wananchi wao mafanikio ya 'Big Results NOW' kama mleta mada anavyotaka tuamini.
Watanzania tuanze kujifunza uhalisia wa mambo, mfano ukipanda viazi uvunaji ni miezi sita na ukipanda viazi vikuu vinakomaa vizuri baada ya mwaka japo vyote vinaotea ardhini. Hivyo tujaribu pamoja na kutumia parameters za kupima ufanisi wa JPM pia kuwa na realistic time frame ya kupima hayo matokeo. Mbali na hapo itakuwa ngumu kuniaminisha kuwa tugemee maofisa waliokuwa wakifaidika na wafanyakazi hewazaidi ya 11,000, wezi wa makontena bila kulipa ushuru, wajenzi wa barabara hewa watakuwa na subira ya mazuri ya JPM. JK kama binadamu mwingine alijaribu lakini alishindwa kwa kiasi kikubwa.
 
Mkuu, hizo ni hisia zako tu ila ukweli unabaki kwamba TRA wanakusanya mapato kwa kuvuka malengo yao

Mkuu Lizaboni:
Ni TRA wenyewe ndio wanao jiwekea hayo malengo na hakuna anae wahakiki, sidhanì kama hilo ni sawa.
Lakini mwelekeo unaonyesha ya kwamba makusanyo ya kila mwezi yanapungua, ni wazi mtu yeyote ataanza kujiuliza na kutafuta sababu...kulikoni?
 
Katika nchi yoyote ile, makusanyo hayawezi kuwa sawa kwa miezi yote.
Kuna miezi yanapanda sana kwa sababu maalum na kuna wakati wa ukame pia.
Kuna watu walisema baada ya miezi miwili yatashuka lakini so far bado ni zaidi ya trillion kila mwezi. Hata yatashuka hayawezi kuwa below average ya Mkwere!
 
Kumekuwa na maporomoko makubwa ya mapato ya TRA kutoka trilioni moja na bilioni mia nne Mwaka Jana wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani mpaka trilioni moja mwezi wa tano.Ni wazi mwezi wa sita TRA watatangaza mapato ya bilioni 900. Tunarudi kulekule kwa JK.

Ni ishara kwamba JK hakuwa mzembe bali mapato yalienda na upepo wa biashara,mwanzoni tuliaminishwa kwamba kuna wizi sijui wapi,sasa mbona na udhibiti wote ndani ya miezi sita mapato yameshuka kwa bilion 400? Zinakwenda wapi?zimepotelea wapi?

Kuna mtu Mwenye ubavu wa kuzikosoa jitihada za Kikwete kwenye kukusanya mapato na aamke nimuone.
Ili mapato yaongezeke itabidi watoe EFD kwa machinga na maa nitilie.
 
Makusanyo yatapandaje wakati uchumi unashuka.TRA wapo sawa maana wanapanga kulingana na hali halisi ya uchumi inavyoenda.Uchumi unazidi kudoda kwa hiyo lazima na makadirio yawe yanashuka chini.Hiyo ni direct proportion sion inversely proportion
 
Mkuu Lizaboni:
Ni TRA wenyewe ndio wanao jiwekea hayo malengo na hakuna anae wahakiki, sidhanì kama hilo ni sawa.
Lakini mwelekeo unaonyesha ya kwamba makusanyo ya kila mwezi yanapungua, ni wazi mtu yeyote ataanza kujiuliza na kutafuta sababu...kulikoni?
Tatizo lako elimu elimu elimu..

Ujuaji ndio shida yenu ufipa hadi mnafanya utabili mambo ya uchumi bila kutoa data za kiuchumi...

Malengo ya ukusanyaji yanawekwa kwa kufuata vigezo vya kitaalam vya kiuchumi na sio kuwa wanaamka asubuhi wanasema mwezi huu tukusanye trilion 1.
 
Back
Top Bottom