Mapambano makali kati ya jeshi la DRC dhidi ya kundi la M23 yaanza tena

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Msemaji wa FARDC Kanali Ndjike Kaiko amesema mapambano makali kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kundi la waasi lijulikanalo kama “The March 23 Movement” (M23) yameanza tena mapema jana huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kanali Kaiko amesema FARC ilianza kufanya mashambulizi dhidi ya Kundi la M23 kuanzia Jumapili asubuhi katika eneo la Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini, ambapo Jeshi la DRC linaendelea kuongoza dhidi ya maadui wao.

Jeshi la taifa linataka kumaliza unafiki wa waasi wa M23 kwa njia timilifu, kwasababu waasi hao hawataki kutimiza amani kwa dhati. Kutokana na kurejeshwa kwa operesheni hizi, jeshi la taifa litadhibiti tena vilima vinavyotumiwa na waasi kama kituo chao, na kuwaletea tena wananchi amani.
 
Waafrika badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma, hii inachangiwa na uuzaji wa silaha kiholela, waafrika hatustahili kupigana hapo tulipopigana panatosha, watu wapepigana juzi tu hali zao ziko hoi huko kwenye nchi tajiri, sisi kuna kitu gani ambacho kinatufanya kupigana kila siku
 
Msemaji wa FARDC Kanali Ndjike Kaiko amesema mapambano makali kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kundi la waasi lijulikanalo kama “The March 23 Movement” (M23) yameanza tena mapema jana huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kanali Kaiko amesema FARC ilianza kufanya mashambulizi dhidi ya Kundi la M23 kuanzia Jumapili asubuhi katika eneo la Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini, ambapo Jeshi la DRC linaendelea kuongoza dhidi ya maadui wao.

Jeshi la taifa linataka kumaliza unafiki wa waasi wa M23 kwa njia timilifu, kwasababu waasi hao hawataki kutimiza amani kwa dhati. Kutokana na kurejeshwa kwa operesheni hizi, jeshi la taifa litadhibiti tena vilima vinavyotumiwa na waasi kama kituo chao, na kuwaletea tena wananchi amani.
vip Bosco Ntaganda anaendeleaje cijapata habari zake kitambo
 
This time JWTZ wasiende kuwasaidia FARDC, waawaache wacongoman wapambane na hali yao kwa maana last time tuliwasaidia kuwafurusha hao 'wahuni' mwishowe wakatu geuzia kibao, tena kibao chenyewe cha uongo….
Tulivamiwa na ADF sio wacongoman. Kidogo ungesema Uganda/Rwanda kahusika ila sio Kinshasa.
 
This time JWTZ wasiende kuwasaidia FARDC, waawaache wacongoman wapambane na hali yao kwa maana last time tuliwasaidia kuwafurusha hao 'wahuni' mwishowe wakatu geuzia kibao, tena kibao chenyewe cha uongo….
kuna jeshi la sadc,na pia kn majeshi ya eac yataenda. Kn mazoezi ya pamoja yanakaribia kuanza yote ni kupeleka aman congo mashariki
 
Back
Top Bottom