DRC: Yalipuka mapigano makali kati ya waasi wa M23 dhidi ya Wazalendo

nyabhera

JF-Expert Member
Nov 25, 2011
660
729
Tangu tarehe 01.10.2023 kumekuwapo na vuguvugu la muungano wa vijana wapiganaji kuvamia ngome za waasi wa M23.

Vijana hawa wanaojiita wazalendo ni mchanganyiko wa vikundi vidogo vidogo vya waasi na wanamgambo nje jeshi la nchi. Wengi ni vikundi maarufu kama Mayi Mayi na Nyatura.

Wazalendo wameanza mapigano kama utani kushambulia M23. Cha ajabu ni hawa vijana wamewaelemea vikali waasi wa M23.

Kwa siku sita tu wameza kukomboa maeneo ya vijiji 21.
Ikumbukwe M23 wamekua na wapiganaji wenye rekodi kubwa na kudhaminia na jeshi la Rwanda

Mara nyingi jeshi la DRC limekua halifui dafu mbele ya hawa M23.

Mapambano yanaendelea huko. Tuwaombe rai wema wasidhurike.

Picha 1 ni orodha ya vijiji na miji iliyokombolewa na wazalendo.

Tazama video hii uone jinsi raia wa mji wa Kitchanga uliokuwa umetekwa na M23 walivyowapokea kwa shangwe wapiganaji wa Wazalendo.
View: https://twitter.com/michombero/status/1710261210103292129?t=GxgPzEyaSS4YN5iRVEyK6Q&s=19

Picha 2 ni wapiganaji Wazalendo baada ya kukomboa mji wa Kitchanga.
1335562513.jpg
1858231261.jpg


Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kuta wanajeshi wa Congo hata mishahara hawalipwi AU wanalipwa nusunusu kama wanajeshi wa Putin.Sasa kwanini ujitoe kwa nguvu zote kwa kazi ambayo haulipwi?Hao wazalendo,mayimayi,hawana cha kupoteza.Mishahara wanajilipa wao wenyewe.Kile wanachokiteka ni mali yao.Ikumbukwe maeneo wanayoyapenda waasi ni yale yenye utajiri mkubwa wa madini kama dhahabu🤔
 
Unaweza kuta wanajeshi wa Congo hata mishahara hawalipwi AU wanalipwa nusunusu kama wanajeshi wa Putin.Sasa kwanini ujitoe kwa nguvu zote kwa kazi ambayo haulipwi?Hao wazalendo,mayimayi,hawana cha kupoteza.Mishahara wanajilipa wao wenyewe.Kile wanachokiteka ni mali yao.Ikumbukwe maeneo wanayoyapenda waasi ni yale yenye utajiri mkubwa wa madini kama dhahabu🤔
Ni kwel kbs askari mdogo anapewa chini ya Dola 50 na anaweza kosa,huku mbunge anapata milioni 54 kwa thamani ya kitanzania kwa mwz.wakongo Wana asili ya usaliti sn
 
Dunia ya sasa ni vita tu sababu ni unafiki wanao tawala Dunia,ikivamiwa Ukreine au Israeli wanachukua hatua ila ikivamiwa Congo au Colombia aiwahusu.
 
Bamutu wamevurugwa balaaa huko wamechafukwa roho vibaya mno unaambiwa huo morali wao haujawahi kuonekana tangu miaka 700 iliyopita tall anaharisha huko mana hata maiti bacongolee wanazitia moto kabisaa za mishnatatu
 
Hii ilikiwa ni wiki ya wanyonge duniani kutakata, huku Hamas kuipa noma the might Israel wakati huohuo hapo jirani Congo anampa kipigo sio cha nchi hii M27.
Congo Anamuunganiko wa vikosi kadhaa vinavyoenda kwa jina la wazalendo.
Watutsi kila saa wanapoteza wapiganaji wao na position.
Wacongo Wamesema dharau sasa mwisho
Slim anasemaje
 
Wanajeshi wa DRC utadhani walichukuliwa kutoka Dar,...

Hawana tofauti na Wanaume wa Dar, wanaokimbia panya road
 
Back
Top Bottom