Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa?

Nimesoma maoni haya ya mhariri wa Citizen nikayapenda nikaona niwashirikishe:

Big and Small Graft All Evil

When people talk about corruption, the common tendency is to focus on the big shots. The emphasis is almost always on those who take advantage of their positions in government or the public sector to enrich themselves.

This tendency has a historical basis. It will be recalled that really serious efforts to combat high-level corruption in this country date back to the formation of the Judge Joseph Warioba Commission in 1996.

The commission's report predictably laid greater emphasis on grand corruption at the national and regional levels, largely ignoring the small-scale graft that is rampant at the grassroots.

The naked truth is that corruption is evil regardless of the magnitude and must be shunned and fought with equal force.

While at the national level, graft diverts public resources from the areas where they are needed into the pockets of a few individuals, at the grassroots, petty corruption leads to denial of public services to deserving cases.

It's for this reason that we wholly welcome Premier Mizengo Pinda's declaration of total war on both the big and small corruption, wherever it may be found.

Despite having the Prevention and Combating of Corruption Bureau, the public body charged with leading the campaign, available evidence indicates that over the past three years, there has been an escalation in cases of corruption and misuse of public resources. The most notorious include the radar deal, Richmond and EPA scandals.

We couldn't agree more with Mr Pinda that as the big graft cases are being dealt with through the judicial process, the focus must now be turned to the small-time village and town operators, whose nefarious activities end up crippling the provision of social services to those who need them most.
 
Invisible,

Mkuu hii ni mbinu ya Kidanganyika.. yaani kutokubali tuna matatizo..

Pinda yeye ni kiongozi hivyo yupo ktk kundi la samaki wakubwa yaani hao wanaweza kufanya Grand corruption. Hivyo lawama zote zinazohusu viongozi zinamhusu yeye na kundi la Mapapa wote ingawaje sii papa wote wanaokula binadamu.

Tatizo la Tanzania linaanza na grand Corruption kwanza. Ikiwa kuna papa anayekula binadamu ni upumbavu mkubwa kuanza kuwinda samaki wadogo wanaokusanyika kula mabaki ya binadamu aliyekwisha uawa na papa..Hivyo msako unaonguanisha samaki wote wanaokula nyama ya binadamu ni kutafuta sababu nje ya ukweli kwamba rushwa zote zinaanza ngazi ya juu.

Ikiwa kutoa container bandari inabidi uwalipe wafanyakazi wahusika ni lazima tukubali kwamba hawa jamaa wamefikia hatua hiyo kutokana na mfumo wa utoaji container hizo. Mara zote fedha unazolipa au wananchi wanazolipa kutoa container hujumuisha na pango la mzee mtoa kibali..
Uzembe wowote wa kazi hutokana na kiongozi wa juu wa shirika au nchi. Na tofauti baina ya nchi mbili ktk rushwa hutokana na mfumo mzima wa uongozi uliopo ktk kutambua na kuziba tobo vinazoweza kukaribisha rushwa. Ukiweza kumzibia mzee (bwana mkubwa) basi wa chini pia hawatapata ulaji..

Mimi nadhani njia bora zaidi ya kukomesha rushwa ni kuweka mfumo bora zaidi wa ukusanyaji fedha za serikali ktk idara zote..ikiwa ni pamoja na kutokubali fedha taslimu (cash) zitumike kulipia malipo yoyote isipokuwa Cheque..

Pili, ikiwa swala la kutotumia cash yaani fedha taslimu litakuwa gumu basi kila ofisi ya serikali iwe na computer kuendesha Account receivable ili kuweka record of every transaction na kutoa receipt badala ya kutumia mkono wa mtu. Hiozi habari za kukadiliwa kodi ndizo chanzo cha matatizo mengi sana nchini..

Tatu, serikali ipunguze mzunguko mkubwa wa ofisi mbali mbali kuomba vibali ktk swala moja. Haya maswala ya kwenda kwa katibu kata, kisha mkuu wa nini sijui kabla hata form za maombi hazijafika ofisi inayotakiwa ni tobo za wazi kabisa kukaribisha rushwa. Ukitaka Passport ni lazima immigration wawe na vigezo vyao. Sio swala la kuambatanisha barua ya katibu kata ambaye sijui anahusiana vipi na uzawa wa mhusika. Unaweza kuwa Unaishi Kariakoo lakini hukuzaliwa Kariakoo, na huyo katibu kata pia anaweza kuwa mhamiaji sasa hii barua ni ktk kuthibitisha kitu gani?.. kwamba wewe ni mkazi wa Kariakoo au raia ulozaliwa nchini kwa sababu unaishi Kariakoo!..sasa vitu kama hivi vinampa sababu katibu kata kuomba kisu kwa sababu hakujui zaidi ya kukuona ukiishi hapo. Wazazi wako wanaweza kuwa wahamiaji baada ya Uhuru lakini yeye hawafahamu kwani yeye pia ni mhamiaji..

Basi ili mradi tu tunajikuna wenyewe kila tunapowashwa..matatizo ya Ufisadi nchini yanaanza na samaki wakubwa mkuu wangu, hizi rushwa ndogo ndogo ni rahisi sana kuzikata ikiwa wakubwa hawana pa kula. trust me, ikiwa Pinda hana Ulaji atahakikisha wa chini yake hawapati kitu..
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Niwe kwanza mletaji wa habari mbaya; hiki kinachoitwa “vita dhidi ya ufisadi” ni vita ambavyo mshindi wake anajulikana mwaka mmoja kabla, mafisadi. Niongeze katika hii habari mbaya; wale wanaojiita wanapigana vita dhidi ya ufisadi wametengeneza mazingira ya kushindwa kwao na hivyo kuwahakikishia mafisadi ushindi rahisi na wa haraka ambao unafanana na ule ushindi wa “chee” wa kwenye mithali. Ni bora tu kama wasingejitokeza kupigana vita hii.

Leo naomba nisiwazungumzie mafisadi moja kwa moja bali wale ambao wanaongoza mapambano dhidi ya ufisadi nchini na maoni yangu ya jumla kuhusu vita hivi na kwanini ninaamini kuwa kama hawatafanya mabadiliko ya haraka ni bora wakae pembeni.

Vita siyo mchezo wa kuigiza na wala si mchezo wa kufuatana mgongoni kama wale wachezao mduara. Anayeingia kwenye vita akifikiria ameingia kwenye mchezo wa “tiari bado” ili kuona ni nani “wa mwisho” ili akamatwe basi hafai vitani. Hakuna mtu wa hatari wakati wa mapambano vitani kama askari ambaye anafanya mzaha kwenye uwanja wa vita. Askari ambaye hajui uzito wa vita anayopigana au kujua uwezo wa adui hafai kunyanyua silaha yake.

Wakati masuala ya EPA yameibuka na kikosi kazi cha kina Mwanyika kilipoanza kazi yake ilisemwa kwamba mafisadi “wameiteka nchi”. Mwanzoni nilichukulia kwa kejeli maneno hayo nikiamini ni msemo tu wa kuelezea ugumu wa kazi iliyopo mbele yao. Karibu mwaka mmoja baadaye na baada ya mimi mwenyewe kufuatilia masuala mbalimbali ambayo yameripotiwa katika ripoti ya kwanza ya Meremeta nimefikia hitimisho kuwa kwamba “wameiteka nchi” haielezei kwa haki kile ambacho mafisadi wamekifanya kwa nchi yetu.

Na hata ulipokuja ugumu wa kuwashtaki wahusika wa Kagoda kuwa ikifanywa hivyo kwa pupa basi “nchi italipuka” nako kunaelezea kwa kiasi tu uzito wa hii vita. Sasa ninaelewa vizuri zaidi kina, upana, uzito, urefu, na kimo cha vita hii. Hii SIYO vita ya watoto kurushiana matope; hii si vita ya watu kugombania ng’ombe au majirani kugombania kuku.

Hii ni vita inayohusu Uhuru wetu. Kilichoko hatarini siyo utajiri wao na tunachogombania siyo kugawana umaskini wetu; ndugu zangu vita hii ni vita ya kuhakikisha tunakuwa huru kutumia nafasi zote halali na za haki kujitengenezea utajiri kila mtu kwa uwezo wake. Ni vita ya kugombania uhuru wetu ambao sasa uko mikononi mwa mafisadi. Siyo tu wameiteka nchi bali mafisadi sasa wanatumiliki; na ushindi wao mwaka 2010 ni kugongelea muhuri tu katika hati ya umiliki wao.

Hiki ndicho kiini cha vita hii; asiyeelewa hili aweke silaha zake chini ajisalimishe kwa adui au arudi nyumbani kulima kama watamuachia arudi. Vinginevyo, kama wale wanaojiita, kujiona au kudhaniwa kuwa ni wa “wapambanaji” wana lengo lolote lile la kushinda vita hii basi wanahitaji kuyapanga majeshi yao upya, kupima uwezo wao, kufikiria mbinu mpya na hatimaye kupigana siyo kupigana ili kutoka sare, wala siyo kupigana ili kutokushindwa; bali kupigana ili KUSHINDA, kwani gharama ya kushindwa ni kukubali kwa taifa zima siyo tu kumilikiwa na mafisadi kama ilivyo sasa bali kuzungushiwa wigo kama wa zizi la mbuzi tukijidhania kuwa tuko huru.

Ndugu zangu, uhuru wa mbuzi ni uhuru kwa kadiri ya kwamba chui hajaamua yupi wa kumla na ni uhuru unaotegemea njaa ya chui. Ukimuona mbuzi anakula majani njiani, na kuacha “karanga” zake barabarani huku akilia “mee mee” usimshangilie kwa kudhania yuko huru.

Bahati mbaya hata hivyo, kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakatiwa ushindi. Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa “mafisadi wanataka kutunyang’anya majimbo” na kuwa “mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu”. Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi.

Ni kwa sababu hiyo naomba niendelee kuwa mletaji wa habari mbaya kwenu. Mafisadi watashinda 2010. Watashinda si kwa sababu wana ujumbe wa uadilifu au wanakubalika zaidi na wananchi, watashinda kwa sababu kwa mtazamo wao vita hii inahusu maisha yao. Wao wanajua vizuri kabisa kuwa endapo watashindwa 2010 hatima yao ni pingu kwenye mikono yao na kuburuzwa kuishia keko; siyo kwa makosa ya kitoto walioshtakiwa kina Mramba, Yona, Mgonja na Liyumba bali kwa makosa makubwa na ya kutisha dhidi ya Jamhuri yetu.

Wanajua wakishindwa 2010 mwisho wao ni Keko au Segerea huku ufunguo wa selo zao ukitupwa katika kichaka cha usahaulifu. Ni kwa sababu hiyo wamejiandaa kushinda na kushinda kwa kishindo cha kutufanya wote wenye kimbelembele cha “ufisadi, ufisadi” kuinamisha vichwa vyetu kwa haya na kurudisha sime zetu alani na kutembea kwa kuchechema kama wafalme walionyang’anywa mataji yao vitani.

Kwanini naamini bila ya mabadiliko ya haraka kwa wapiganaji mafisadi watashinda?

  • Mafisadi wana vipaji. Mojawapo ya mambo ambayo nimegundua katika muda huu wa miaka mitatu ya kufuatilia suala hili ninaweza kusema kwa uhakika mkubwa kabisa kuwa wale watu tunaowataja kuwa ni wanahusika na ufisadi na wale ambao majina yao hatujaanza kuyataja kwa wana vipaji vikubwa vya ushawishi na uwezo wa ajabu wa kufanikisha malengo yao.

Ninapozungumzia vipaji sizungumzii karama zao wenyewe tu bali nazungumzia mkusanyiko wa watu wanaowakubali, kuwaamini na kuwaitikia kila wanapoita. Ni kwa sababu hiyo wamejipanga katika nafasi mbalimbali za serikali, vyombo vya usalama, vyombo vya habari, taasisi za kidini na kama vinyonga vikaragosi vyao vinapita katikati yetu na kujionesha kwa rangi ya upambanaji. Ugumu wake ni kujua yupi ni kinyonga na yupi ni mpambanaji wa kweli. Si wote wapigao kelele za “vita ya ufisadi” ni wapiganaji wa vita hivyo; wengine wanalazimishwa na wake zao!

  • Mafisadi wana raslimali: Katika hili wala kusiwe na utata; mafisadi wamekusanya raslimali zao na wakiunganisha na vipaji vyao kikomo chao ni mbingu tu. Kimsingi wanachofanya kama mtu mmoja alivyoangaliza siku chache zilizopita ni kuwa wanatumia utajiri waliounyonya toka migongoni mwetu kuhakikisha tunabakia chini ya miguu yao. Yaani, wamepanga kutukaanga kwa mafuta yetu wenyewe huku sisi wenyewe tukichekelea chekelea.

  • Mafisadi hawaogopi vyombo vya sheria au usalama. Hili linaweza lisiwe dhahiri kwa mtu mwingine lakini kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia suala la ufisadi tangu kuanza kwake kwa mtindo wa kuuza raslimali zetu wakati wa Loliondo hadi leo Meremeta mafisadi wamejifunza kujiamini kiasi kwamba sheria zinazotufunga sisi wengine wao wamejipa udhuru.

Asikudanganye mwanasiasa yoyote, mafisadi, makuwadi wao, vikaragosi na wapambe wao hawamuogopi Mwema wala shemeji yake Mwema; hawamuogopi Othmani wala Feleshi na kwa hakika hawana hofu ya kitu kinachoitwa “utawala wa sheria”. Katika fikra zao wao NDIO sheria. Walitengeneza mfumo huo wa wao kuwa juu ya sheria tangu walipoanza kuvunja vunja sheria zetu mwaka 1995, 1996, 1997, 1998, 1999, na 2000. Kuanzia 2000 ilikuwa ni wakati wa mavuno. Mafisadi wamezuiliwa kidogo tu kati ya 2005 na sasa lakini wameshajifunza somo moja hawawezi tena kukaa nje ya madaraka ifikapo 2010.

  • Mafisadi hawamuogopi Rais Kikwete. Kuna watu wanafikiri kuwa Kikwete ni tishio la mafisadi nchini; kwamba kwa namna moja au nyingine mafisadi wanatetemeka mbele yake. Naomba niendelee kuwa mjumbe wa habari mbaya kwenu; mafisadi hawamuogopi Kikwete, cheo chake wala jina lake.

Laiti wangekuwa na chembe ya woga wasingethubutu au kuwa na ujasiri wa kuendelea kutenda wayatendayo. Wakiangalia mashtaka mbalimbali dhidi ya wenzao wanajua kwa uhakika kuwa hakuna jambo lolote ambalo linaweza kuwakuta ambalo ni kali kuliko haya mengine.

Na hii ndiyo sababu hadi hivi sasa kwenye suala la Richmond kwa mfano, hadi hivi sasa hakuna hata mmoja wao aliyesimama na kusema “tulifanya makosa” na kukubali kuwajibika. Ninashangazwa na jinsi gani Richmond inaonekana kama vile ililetwa na mizimu kwani hakuna mtu ambaye anakubali moja kwa moja kuhusika. Kikwete anakana, Rostam hawajui, Lowassa ndio kabisa.

Sasa imebakia kutoa matamko kwenye vyombo vya habari. Inapofikia Ikulu wanajiuma uma maneno kuwachukulia hatua wahusika wa Richmond na Kagoda ujue mafisadi hawana hofu.

Hata hivyo siyo yale tu ambayo wanafanya mafisadi ndiyo yatawahakikishia ushindi 2010. Ninaamini na ndio sababu pia ya kuandika hili kuwa yale wayafanyayo wapambanaji ndiyo yanawatengenezea ushindi mafisadi na makuwadi wao. Miongoni mwa mambo ambayo wapambanaji wanayafanya na ambayo hayamfai mpiganaji yeyote vitani ni haya:

  • Wamegawanyika: Hivi sasa ukiangalia kwa karibu utaona kuna makundi ya wapambanaji. Wapo walioko ndani ya CCM na wapo walioko kwenye upinzani. Kwenye CCM wapo watu kama kina Ole Sendeka, Mpendazoe, Kilango, Mwakyembe n.k na kwa upande wa upinzani wapo kina Dr. Slaa, Zitto, Ahmed Rashid n.k Ukiangalia kwa karibu utafikiri kuwa wote wanapigana vita moja.

Bahati mbaya kama ilivyoonekana Busanda wapiganaji hawa wanasema wanapigana vita ile ile na adui yule yule lakini wao wenyewe wanapigana vile vile. Haya ni maajabu vitani. Kwenye uwanja wa vita askari akigeuza silaha yake na kuanza kuwarushia risasi wapiganaji wenzake askari huyo ni msaliti wa vita na ni kinyume na mwelekeo wa ushindi.

Hivyo, ninapoona na kusikia wabunge wapambanaji wa upinzani wakirusha maneno dhidi ya wale wa CCM au kinyume chake nina uhakika wapiganaji wa upande wa ufisadi wanachekelea tu kwani wanajua kuwa wapiganaji dhidi yao hawajaungana (united front). Hakuna jeshi rahisi kulishinda kama jeshi lililogawanyika.

  • Hawana ujumbe mmoja: Mojawapo ya vitu ambavyo vinanishangaza ni kuona jinsi gani wapiganao vita dhidi ya ufisadi walivyokosa ujumbe mmoja. Hivi ukiwauliza wanapigana vita hii wakiwa na ujumbe gani watasema nini? Kusema “kuna ufisadi” siyo ujumbe wa matumaini; kusema “mafisadi wameiteka nchi” siyo ujumbe wa faraja; kusema kuwa “tuwapinge mafisadi” haitusaidii.

Matokeo yake utaona kuwa kila mpambanaji akianza kuzungumza anazungumzia maslahi yake. Jinsi gani mafisadi hawamtakii mema, wanapanga njama za kumuangusha n.k Hadi hivi sasa Watanzania wanajua kile ambacho mafisadi wamekifanya kwa nchi yetu. Lakini Watanzania hawahitaji ujumbe wa kuwaelewa mafisadi au ubaya wake kwani hilo limeandikwa vya kutosha.

Watanzania wanataka kujua hawa wapambanaji wakipewa nafasi ya ushindi 2010 watafanya nini na mafisadi? Leo hii, wote wanaogopa kusema watakachofanya kuwashughulikia mafisadi na kurudisha uwajibikaji katika ulingo wa siasa. Wapiganaji wanahitaji ujumbe mpya wa matumaini ambao ndani yake utashughulikia mambo makubwa mawili; kwanza, utaeleza hatua za kumaliza kashfa hizi zote za kifisadi (msamaha si mojawapo) na pili, utaelezea ni jinsi gani wataleta mabadiliko ambayo hayatafungua mlango wa ufisadi mpya na hivyo kutuelekeza katika ujenzi wa taifa la kisasa.

Vinginevyo hii ni vita ambavyo mwisho wake tutagundua kuwa ina chuki za ndani, visasi, wivu, n.k na haihusiaji hata kidogo na maslahi ya taifa letu.

  • Hawajaunganisha raslimali zao na vipaji: Mojawapo ya mambo ambayo ninaweza kuona tofauti kubwa kati ya kambi ya mafisadi na kambi ya wapambanaji ni kuwa wapambanajij wanategemea kudra na imani kuwa wananchi wanawaunga mkono. Wanaombea kuwa hatimaye mafisadi watashindwa. Hiyo siyo vita.

Vita ni mbinu na ni mikakati. Na unapoingia vitani usisite kuchukua mateka na ukirusha makombora yako hakikisha unalenga kwenye kuangamiza siyo kuchekelea. Kama kweli hii ni vita ya uhuru wetu basi ningetarajia wapambanaji na wenyewe wangeonesha kuwa wanaweza kupigana.

Juzi nimesoma mmoja wao akilalamika kuwa kuna vipeperushi vimeangushwa kwenye jimbo lake na mwingine alilalamika kuwa mafisadi wanapeleka misaada na fedha kwenye jimbo lake. Nikajiuliza, wao wanafanya nini kujibu mashambulizi?

Nimechoka na sauti zao za kulia lia na kulalamika kama watoto walionyang’anywa pipi. Nimeshasema hapo juu kuwa mafisadi hawafanyi utani kwani katika vita hii wao wanapigania maisha yao. Nilitarajia wapiganaji wetu na wenyewe wangeacha utani. Moto kwa moto na kombola kwa kombola. Haya mambo ya “acheni malumbano” ni mambo ya kitoto. Ni lazima mgongano wa kifikra utokee na uendelee na wapiganaji wasiombe radhi kwa kuchukua msimamo huo.

Wakifanya hivyo nao wajue kuwa watashambuliwa. Hiyo ndiyo maana ya vita. Haiwezekani wao warushe makombora halafu watarajie mashada ya maua toka kwa maadui. Mafisadi nao watarusha makombora yao na kama wale wapiganaji wa waasi kule Iraq na Afghanistani mafisadi hawafuati sheria za vita hivyo watakuja hata na mbinu chafu. Mpiganaji ambaye hajatarajia hilo au hajajiandaa kwa hilo ni bora akae pembeni kwani huko tunakokwenda siyo mishale na mikuki itatumika bali hadi makombora ya masafa marefo ya bara na bara (Inter-Continental Ballistic Missiles -ICBMs).

Nina uhakika hata mimi niliye kijijini huku sitoachiliwa makombora hayo. Bahati nzuri miye na kikosi changu tunasubiri kwa hamu kwani tayari makombora yetu ya “Patriots” (mzalendo) yako tayari kujibu mashambulizi.

Hivyo, kama hawawezi kukaa chini na kuangalia ni raslimali gani walizonazo, ni vipaji gani walivyonazo na wakajipanga kuelekea ushindi basi wajue mafisadi watauelekea ushindi kwa raha yao wenyewe.

Ninachosema ni kuwa mapambano haya yataendelea. Hata hivyo, mafisadi ndio wamejipanga vizuri zaidi wakijua wanachopigania na wakiwa tayari na ujasiri wa kufanya lolote ili kurudi madarakani 2010. Na kama mwendo utaendelea hivi hivi basi nitakuwa mtu wa mwisho kushangaa nikisikia “wapiganaji” wakianguka mwakani. Msije mkasema hamkuweza kuona hilo likija. Mmeonywa mwaka mmoja na zaidi kabla. Mafisadi wakishinda msiwalaumu; mmewatengenezea njia na kuipalilia.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Post ya MKJJ imeniacha na woga usio kifani!..KUNA MATUMAINI YOYOTE YA KUSHINDA HII VITA KAMA MAMBO NI HAYA?..

Kwa wapambanaji, kuna haja ya ku retreat..na kujipanga upya.Vita haipiganwi mfululizo..inabidi kuvuta pumzi wakati mwingine.
 
Companero watu wetu hawajui tunachopigania na wengine wanafikiri ni kama utani wa aina fulani hivi. Unajua watoto wakienda baharani wana michezo mbalimbali, kurushiana maji, kucheza kidali po..na siku hizi hadi beach volleybal na basketball.. what is at stake ni furaha yao na heshima yao. Ni michezo tu.

Ninaposikia watu wanasema "vita dhidi ya ufisadi" sasa hivi nabakia kucheka tu kwani kama vita ndiyo inapiganwa hivi.. kwanini adui asishinde?
 
Mkuu majuzi niliangalia mkanda murua wa TBC1 kuhusu Vita dhidi ya Nduli Amin. Nilimsikiliza sana Mboma na Msuguri ambao walionyesha kuwa hakika wao na Marwa pamoja na Kiwelu walikuwa vinara (masterminds) wa vita hiyo. Mboma alielezea kwa undani mbinu za hali ya juu zilizotumika kuipiga mabomu kwa ndege Kampala. Kuna Fizikia ya hali ya juu ilitumika kupitisha ndege chinichini bila kuonwa na rada za adui tena kwa kwa kasi ya sauti (speed of sound) na hivyo kusababisha kelele nzito kama zile za mabomu ya Mbagala. Hakika nia ya kumpiga tulikuwa nayo, sababu ya kumpiga tulikuwa nayo na uwezo wa kumpiga tulikuwa nao!

Lakini je, kila mwananchi na askari alikuwa na nia moja, sababu moja na uwezo wa aina moja? La hasha! Kwenye kila vita kuna makomandoo na makuruta. Hata kwenye vita hii ya ufisadi ni hivyo hivyo. Tuna ma-field masharl, kina Silaha. Lakini pia tuna makuruta, kina Kompanero. Ni jukumu la ma-field masharl ambao ndio masterminds wa vita hii kutuonesha njia. Pia ni jukumu lao kutuhamasisha kwa propaganda za hali ya juu kama alivyotuhamasisha Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Nyerere!

Aluta Continua! La Hasta Victoria Siempre! Vinceremos!
 
Komredi.. baada ya suala la Meremeta na mambo yaliyofuatia baadaye (ambayo sasa yanabakia kifuani) nimeweza kuelewa vizuri zaidi ugumu wa vita hii. Ninamuelewa vizuri adui sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote ule.

Mojawapo ya shows zangu ninazozipenda sana ni ile ya Star Trek ya "The Next Generation" na kapteni Jean Luc Piccard (Patrick Stewart - wengi wanamfahamu kutoka na na filamu za X-Men). Mojawapo ya episodes ni pale ma Borgs walipoweza kumteka na kujaribu kumassimilate na kuanza kumtumia dhidi ya federation. Walijua wakimkamata kapteni basi ni rahisi kuweza kuinfiltrate taarifa nyingi za kimkakati na usalama.

Ilibidi wale maofisa waliochwa kwenye meli wafikirie ni jinsi gani wanaweza kumnusuru kapteni wao na hatimaye kuwazidi maarifa my cyborgs.
 
Mkuu mbona unanena kwa mifano (parables)! Hapo awali si umesema hawamwogopi Nahodha (Captain)! Au ni kwa sababu wamemzoesha (assimilate) na kuanza kumtumia dhidi ya muungano wa wapinga ufisadi? Kama ni hivyo, je anaweza kunusurika (rescued) huyu?
 
mzee huyu wa sasa sidhani kama ameshakuwa assimilated fully.. yule wa 1995-2005 ndiyo walimuingiza katika himaya yao na kumtumia dhidi yetu. Siyo yeye tu bali pia mwanasheria wetu Mkuu, wakuu wetu wa Usalama, magavana wetu wa Benki Kuu n.k Sasa sasa hivi tumenasa kama yule sungura alivyonaswa kwenye ile sanamu!
 
Samaki mmoja akioza? Naona huyu bado una imani naye! Yeye sio sehemu ya hiyo "n.k" yako hapo juu? Kumbe Synovate wako sahihi! Je, yeye ndiye au tumtegemee mwingine atuongoze kwenye vita hii dhidi ya ufisadi?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Niwe kwanza mletaji wa habari mbaya; hiki kinachoitwa "vita dhidi ya ufisadi" ni vita ambavyo mshindi wake anajulikana mwaka mmoja kabla, mafisadi. Niongeze katika hii habari mbaya; wale wanaojiita wanapigana vita dhidi ya ufisadi wametengeneza mazingira ya kushindwa kwao na hivyo kuwahakikishia mafisadi ushindi rahisi na wa haraka ambao unafanana na ule ushindi wa "chee" wa kwenye mithali. Ni bora tu kama wasingejitokeza kupigana vita hii.

Leo naomba nisiwazungumzie mafisadi moja kwa moja bali wale ambao wanaongoza mapambano dhidi ya ufisadi nchini na maoni yangu ya jumla kuhusu vita hivi na kwanini ninaamini kuwa kama hawatafanya mabadiliko ya haraka ni bora wakae pembeni.

Vita siyo mchezo wa kuigiza na wala si mchezo wa kufuatana mgongoni kama wale wachezao mduara. Anayeingia kwenye vita akifikiria ameingia kwenye mchezo wa "tiari bado" ili kuona ni nani "wa mwisho" ili akamatwe basi hafai vitani. Hakuna mtu wa hatari wakati wa mapambano vitani kama askari ambaye anafanya mzaha kwenye uwanja wa vita. Askari ambaye hajui uzito wa vita anayopigana au kujua uwezo wa adui hafai kunyanyua silaha yake.

Wakati masuala ya EPA yameibuka na kikosi kazi cha kina Mwanyika kilipoanza kazi yake ilisemwa kwamba mafisadi "wameiteka nchi". Mwanzoni nilichukulia kwa kejeli maneno hayo nikiamini ni msemo tu wa kuelezea ugumu wa kazi iliyopo mbele yao. Karibu mwaka mmoja baadaye na baada ya mimi mwenyewe kufuatilia masuala mbalimbali ambayo yameripotiwa katika ripoti ya kwanza ya Meremeta nimefikia hitimisho kuwa kwamba "wameiteka nchi" haielezei kwa haki kile ambacho mafisadi wamekifanya kwa nchi yetu.

Na hata ulipokuja ugumu wa kuwashtaki wahusika wa Kagoda kuwa ikifanywa hivyo kwa pupa basi "nchi italipuka" nako kunaelezea kwa kiasi tu uzito wa hii vita. Sasa ninaelewa vizuri zaidi kina, upana, uzito, urefu, na kimo cha vita hii. Hii SIYO vita ya watoto kurushiana matope; hii si vita ya watu kugombania ng'ombe au majirani kugombania kuku.

Hii ni vita inayohusu Uhuru wetu. Kilichoko hatarini siyo utajiri wao na tunachogombania siyo kugawana umaskini wetu; ndugu zangu vita hii ni vita ya kuhakikisha tunakuwa huru kutumia nafasi zote halali na za haki kujitengenezea utajiri kila mtu kwa uwezo wake. Ni vita ya kugombania uhuru wetu ambao sasa uko mikononi mwa mafisadi. Siyo tu wameiteka nchi bali mafisadi sasa wanatumiliki; na ushindi wao mwaka 2010 ni kugongelea muhuri tu katika hati ya umiliki wao.

Hiki ndicho kiini cha vita hii; asiyeelewa hili aweke silaha zake chini ajisalimishe kwa adui au arudi nyumbani kulima kama watamuachia arudi. Vinginevyo, kama wale wanaojiita, kujiona au kudhaniwa kuwa ni wa "wapambanaji" wana lengo lolote lile la kushinda vita hii basi wanahitaji kuyapanga majeshi yao upya, kupima uwezo wao, kufikiria mbinu mpya na hatimaye kupigana siyo kupigana ili kutoka sare, wala siyo kupigana ili kutokushindwa; bali kupigana ili KUSHINDA, kwani gharama ya kushindwa ni kukubali kwa taifa zima siyo tu kumilikiwa na mafisadi kama ilivyo sasa bali kuzungushiwa wigo kama wa zizi la mbuzi tukijidhania kuwa tuko huru.

Ndugu zangu, uhuru wa mbuzi ni uhuru kwa kadiri ya kwamba chui hajaamua yupi wa kumla na ni uhuru unaotegemea njaa ya chui. Ukimuona mbuzi anakula majani njiani, na kuacha "karanga" zake barabarani huku akilia "mee mee" usimshangilie kwa kudhania yuko huru.

Bahati mbaya hata hivyo, kwa mwendo wa sasa wa wapiganaji wetu na nikiangalia mwelekeo wa harakati za mabadiliko nashawishika kuamini kuwa vita hii ni vita ya maneno na siyo ya yenye mkakatiwa ushindi. Ni vita ya mbele ya vyombo vya habari na kwenye majukwaa ya siasa. Ni vita ya wanaharakati kulalamika kuwa "mafisadi wanataka kutunyang'anya majimbo" na kuwa "mafisadi wanamwaga fedha kwenye majimbo yetu". Sisikii kauli za wapiganaji wenye fikra za ushindi.

Ni kwa sababu hiyo naomba niendelee kuwa mletaji wa habari mbaya kwenu. Mafisadi watashinda 2010. Watashinda si kwa sababu wana ujumbe wa uadilifu au wanakubalika zaidi na wananchi, watashinda kwa sababu kwa mtazamo wao vita hii inahusu maisha yao. Wao wanajua vizuri kabisa kuwa endapo watashindwa 2010 hatima yao ni pingu kwenye mikono yao na kuburuzwa kuishia keko; siyo kwa makosa ya kitoto walioshtakiwa kina Mramba, Yona, Mgonja na Liyumba bali kwa makosa makubwa na ya kutisha dhidi ya Jamhuri yetu.

Wanajua wakishindwa 2010 mwisho wao ni Keko au Segerea huku ufunguo wa selo zao ukitupwa katika kichaka cha usahaulifu. Ni kwa sababu hiyo wamejiandaa kushinda na kushinda kwa kishindo cha kutufanya wote wenye kimbelembele cha "ufisadi, ufisadi" kuinamisha vichwa vyetu kwa haya na kurudisha sime zetu alani na kutembea kwa kuchechema kama wafalme walionyang'anywa mataji yao vitani.

Kwanini naamini bila ya mabadiliko ya haraka kwa wapiganaji mafisadi watashinda?

  • Mafisadi wana vipaji. Mojawapo ya mambo ambayo nimegundua katika muda huu wa miaka mitatu ya kufuatilia suala hili ninaweza kusema kwa uhakika mkubwa kabisa kuwa wale watu tunaowataja kuwa ni wanahusika na ufisadi na wale ambao majina yao hatujaanza kuyataja kwa wana vipaji vikubwa vya ushawishi na uwezo wa ajabu wa kufanikisha malengo yao.

Ninapozungumzia vipaji sizungumzii karama zao wenyewe tu bali nazungumzia mkusanyiko wa watu wanaowakubali, kuwaamini na kuwaitikia kila wanapoita. Ni kwa sababu hiyo wamejipanga katika nafasi mbalimbali za serikali, vyombo vya usalama, vyombo vya habari, taasisi za kidini na kama vinyonga vikaragosi vyao vinapita katikati yetu na kujionesha kwa rangi ya upambanaji. Ugumu wake ni kujua yupi ni kinyonga na yupi ni mpambanaji wa kweli. Si wote wapigao kelele za "vita ya ufisadi" ni wapiganaji wa vita hivyo; wengine wanalazimishwa na wake zao!

  • Mafisadi wana raslimali: Katika hili wala kusiwe na utata; mafisadi wamekusanya raslimali zao na wakiunganisha na vipaji vyao kikomo chao ni mbingu tu. Kimsingi wanachofanya kama mtu mmoja alivyoangaliza siku chache zilizopita ni kuwa wanatumia utajiri waliounyonya toka migongoni mwetu kuhakikisha tunabakia chini ya miguu yao. Yaani, wamepanga kutukaanga kwa mafuta yetu wenyewe huku sisi wenyewe tukichekelea chekelea.

  • Mafisadi hawaogopi vyombo vya sheria au usalama. Hili linaweza lisiwe dhahiri kwa mtu mwingine lakini kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia suala la ufisadi tangu kuanza kwake kwa mtindo wa kuuza raslimali zetu wakati wa Loliondo hadi leo Meremeta mafisadi wamejifunza kujiamini kiasi kwamba sheria zinazotufunga sisi wengine wao wamejipa udhuru.

Asikudanganye mwanasiasa yoyote, mafisadi, makuwadi wao, vikaragosi na wapambe wao hawamuogopi Mwema wala shemeji yake Mwema; hawamuogopi Othmani wala Feleshi na kwa hakika hawana hofu ya kitu kinachoitwa "utawala wa sheria". Katika fikra zao wao NDIO sheria. Walitengeneza mfumo huo wa wao kuwa juu ya sheria tangu walipoanza kuvunja vunja sheria zetu mwaka 1995, 1996, 1997, 1998, 1999, na 2000. Kuanzia 2000 ilikuwa ni wakati wa mavuno. Mafisadi wamezuiliwa kidogo tu kati ya 2005 na sasa lakini wameshajifunza somo moja hawawezi tena kukaa nje ya madaraka ifikapo 2010.

  • Mafisadi hawamuogopi Rais Kikwete. Kuna watu wanafikiri kuwa Kikwete ni tishio la mafisadi nchini; kwamba kwa namna moja au nyingine mafisadi wanatetemeka mbele yake. Naomba niendelee kuwa mjumbe wa habari mbaya kwenu; mafisadi hawamuogopi Kikwete, cheo chake wala jina lake.

Laiti wangekuwa na chembe ya woga wasingethubutu au kuwa na ujasiri wa kuendelea kutenda wayatendayo. Wakiangalia mashtaka mbalimbali dhidi ya wenzao wanajua kwa uhakika kuwa hakuna jambo lolote ambalo linaweza kuwakuta ambalo ni kali kuliko haya mengine.

Na hii ndiyo sababu hadi hivi sasa kwenye suala la Richmond kwa mfano, hadi hivi sasa hakuna hata mmoja wao aliyesimama na kusema "tulifanya makosa" na kukubali kuwajibika. Ninashangazwa na jinsi gani Richmond inaonekana kama vile ililetwa na mizimu kwani hakuna mtu ambaye anakubali moja kwa moja kuhusika. Kikwete anakana, Rostam hawajui, Lowassa ndio kabisa.

Sasa imebakia kutoa matamko kwenye vyombo vya habari. Inapofikia Ikulu wanajiuma uma maneno kuwachukulia hatua wahusika wa Richmond na Kagoda ujue mafisadi hawana hofu.

Hata hivyo siyo yale tu ambayo wanafanya mafisadi ndiyo yatawahakikishia ushindi 2010. Ninaamini na ndio sababu pia ya kuandika hili kuwa yale wayafanyayo wapambanaji ndiyo yanawatengenezea ushindi mafisadi na makuwadi wao. Miongoni mwa mambo ambayo wapambanaji wanayafanya na ambayo hayamfai mpiganaji yeyote vitani ni haya:

  • Wamegawanyika: Hivi sasa ukiangalia kwa karibu utaona kuna makundi ya wapambanaji. Wapo walioko ndani ya CCM na wapo walioko kwenye upinzani. Kwenye CCM wapo watu kama kina Ole Sendeka, Mpendazoe, Kilango, Mwakyembe n.k na kwa upande wa upinzani wapo kina Dr. Slaa, Zitto, Ahmed Rashid n.k Ukiangalia kwa karibu utafikiri kuwa wote wanapigana vita moja.

Bahati mbaya kama ilivyoonekana Busanda wapiganaji hawa wanasema wanapigana vita ile ile na adui yule yule lakini wao wenyewe wanapigana vile vile. Haya ni maajabu vitani. Kwenye uwanja wa vita askari akigeuza silaha yake na kuanza kuwarushia risasi wapiganaji wenzake askari huyo ni msaliti wa vita na ni kinyume na mwelekeo wa ushindi.

Hivyo, ninapoona na kusikia wabunge wapambanaji wa upinzani wakirusha maneno dhidi ya wale wa CCM au kinyume chake nina uhakika wapiganaji wa upande wa ufisadi wanachekelea tu kwani wanajua kuwa wapiganaji dhidi yao hawajaungana (united front). Hakuna jeshi rahisi kulishinda kama jeshi lililogawanyika.

  • Hawana ujumbe mmoja: Mojawapo ya vitu ambavyo vinanishangaza ni kuona jinsi gani wapiganao vita dhidi ya ufisadi walivyokosa ujumbe mmoja. Hivi ukiwauliza wanapigana vita hii wakiwa na ujumbe gani watasema nini? Kusema "kuna ufisadi" siyo ujumbe wa matumaini; kusema "mafisadi wameiteka nchi" siyo ujumbe wa faraja; kusema kuwa "tuwapinge mafisadi" haitusaidii.

Matokeo yake utaona kuwa kila mpambanaji akianza kuzungumza anazungumzia maslahi yake. Jinsi gani mafisadi hawamtakii mema, wanapanga njama za kumuangusha n.k Hadi hivi sasa Watanzania wanajua kile ambacho mafisadi wamekifanya kwa nchi yetu. Lakini Watanzania hawahitaji ujumbe wa kuwaelewa mafisadi au ubaya wake kwani hilo limeandikwa vya kutosha.

Watanzania wanataka kujua hawa wapambanaji wakipewa nafasi ya ushindi 2010 watafanya nini na mafisadi? Leo hii, wote wanaogopa kusema watakachofanya kuwashughulikia mafisadi na kurudisha uwajibikaji katika ulingo wa siasa. Wapiganaji wanahitaji ujumbe mpya wa matumaini ambao ndani yake utashughulikia mambo makubwa mawili; kwanza, utaeleza hatua za kumaliza kashfa hizi zote za kifisadi (msamaha si mojawapo) na pili, utaelezea ni jinsi gani wataleta mabadiliko ambayo hayatafungua mlango wa ufisadi mpya na hivyo kutuelekeza katika ujenzi wa taifa la kisasa.

Vinginevyo hii ni vita ambavyo mwisho wake tutagundua kuwa ina chuki za ndani, visasi, wivu, n.k na haihusiaji hata kidogo na maslahi ya taifa letu.

  • Hawajaunganisha raslimali zao na vipaji: Mojawapo ya mambo ambayo ninaweza kuona tofauti kubwa kati ya kambi ya mafisadi na kambi ya wapambanaji ni kuwa wapambanajij wanategemea kudra na imani kuwa wananchi wanawaunga mkono. Wanaombea kuwa hatimaye mafisadi watashindwa. Hiyo siyo vita.

Vita ni mbinu na ni mikakati. Na unapoingia vitani usisite kuchukua mateka na ukirusha makombora yako hakikisha unalenga kwenye kuangamiza siyo kuchekelea. Kama kweli hii ni vita ya uhuru wetu basi ningetarajia wapambanaji na wenyewe wangeonesha kuwa wanaweza kupigana.

Juzi nimesoma mmoja wao akilalamika kuwa kuna vipeperushi vimeangushwa kwenye jimbo lake na mwingine alilalamika kuwa mafisadi wanapeleka misaada na fedha kwenye jimbo lake. Nikajiuliza, wao wanafanya nini kujibu mashambulizi?

Nimechoka na sauti zao za kulia lia na kulalamika kama watoto walionyang'anywa pipi. Nimeshasema hapo juu kuwa mafisadi hawafanyi utani kwani katika vita hii wao wanapigania maisha yao. Nilitarajia wapiganaji wetu na wenyewe wangeacha utani. Moto kwa moto na kombola kwa kombola. Haya mambo ya "acheni malumbano" ni mambo ya kitoto. Ni lazima mgongano wa kifikra utokee na uendelee na wapiganaji wasiombe radhi kwa kuchukua msimamo huo.

Wakifanya hivyo nao wajue kuwa watashambuliwa. Hiyo ndiyo maana ya vita. Haiwezekani wao warushe makombora halafu watarajie mashada ya maua toka kwa maadui. Mafisadi nao watarusha makombora yao na kama wale wapiganaji wa waasi kule Iraq na Afghanistani mafisadi hawafuati sheria za vita hivyo watakuja hata na mbinu chafu. Mpiganaji ambaye hajatarajia hilo au hajajiandaa kwa hilo ni bora akae pembeni kwani huko tunakokwenda siyo mishale na mikuki itatumika bali hadi makombora ya masafa marefo ya bara na bara (Inter-Continental Ballistic Missiles -ICBMs).

Nina uhakika hata mimi niliye kijijini huku sitoachiliwa makombora hayo. Bahati nzuri miye na kikosi changu tunasubiri kwa hamu kwani tayari makombora yetu ya "Patriots" (mzalendo) yako tayari kujibu mashambulizi.

Hivyo, kama hawawezi kukaa chini na kuangalia ni raslimali gani walizonazo, ni vipaji gani walivyonazo na wakajipanga kuelekea ushindi basi wajue mafisadi watauelekea ushindi kwa raha yao wenyewe.

Ninachosema ni kuwa mapambano haya yataendelea. Hata hivyo, mafisadi ndio wamejipanga vizuri zaidi wakijua wanachopigania na wakiwa tayari na ujasiri wa kufanya lolote ili kurudi madarakani 2010. Na kama mwendo utaendelea hivi hivi basi nitakuwa mtu wa mwisho kushangaa nikisikia "wapiganaji" wakianguka mwakani. Msije mkasema hamkuweza kuona hilo likija. Mmeonywa mwaka mmoja na zaidi kabla. Mafisadi wakishinda msiwalaumu; mmewatengenezea njia na kuipalilia.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

MWKJJ, ukiwa kwenye vita huwapi sifa adui. Hata kama unajua wamewazidi ujanja kwa sasa, hali hiyo ni temporary tu. Muda si mrefu tunawabwanga. Hiyo ndo mentality inayotakiwa kwenye vita. Point 7 ulizotoa zina ukweli, na unge-concentrate na hizo badala ya ku-demolorise the troops. Vita hii sio ndogo, ni kubwa. Na sio rahisi iishe mwaka huu au hata ujao. Lakini tujipange na kuimaliza. Maybe hata itabidi tu-defend kwa damu...but free we shall be.
 
Nitaendelea kuwaletea mengine zaidi ila hadi wakati huo..tuchangie katika yafuatayo?
Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.

Hebu tuangalie uzoefu wa wenzetu:

UGANDA
The struggle against corruption has evolved significantly since the President first identified corruption as a priority issue requiring top-level Government attention. Initially, an Anticorruption Unit was created in the Office of the Vice-President to coordinate the anticorruption activities of the agencies, the Inspectorate of Government (“IGG”), the Criminal Investigations Department of the Police (“CID”), the Auditor General (“AG”), the Ministry of Finance, Planning and Economic Development (“MFPED”) and the Ministry of Public Service (“MPS”). Because some of these agencies did not have a voice in Cabinet, the Vice-President was made the spokesperson.

But Government soon realised that tackling corruption required long-term attention, not only to investigation and prosecution, but also to the prevention of corruption and to its root causes. The section grew to a Directorate headed by a full Cabinet Minister, lodged in the Presidency. Its name was changed to “Directorate of Ethics and Integrity” to reflect its wider mandate.

In December 1998, the Government of Uganda advanced its first comprehensive anticorruption Plan of Action, “Government Policy and Plan of Action to Fight Corruption” (“Plan of Action” or “Plan”). The Plan was the outcome of the first joint planning for anticorruption. It embraced the activities of a number of different government structures, and to address the specific concerns that had been voiced by civil society, donor partners, and government actors themselves. This plan was discussed and approved by Cabinet. To date the plan has been prioritised operationalised and costed. The plan is now entitled “Government Strategy and Plan of Action to Fight Corruption and Build Ethics and Integrity in Public Office 2000/1 – 2002/3.”

The Government’s political will to fight corruption has been demonstrated by its identification of corruption as a priority action, by the heading of the Directorate of Ethics and Integrity by a full Cabinet Minister, by Cabinet’s approval of a comprehensive anticorruption Plan of Action, by the establishment of an Inter-Agency Forum to oversee the development and implementation of the anticorruption Plan of Action, and by the censuring of Ministers and the prosecution of Accounting Officers for corrupt acts.

In February-March, 2000, the Government conducted an assessment of progress on implementation of the Plan of Action, based on document reviews and interviews with government stakeholders.
The progress made so far should be considered in light of the considerable constraints with which the various agencies grapple. These include:
Constraints
Lack of human resources. There is a general lack of human resources both in quality and quantity. Most agencies continue to be short of needed staff even as they find that they must cover wider areas because of decentralisation. The agencies have difficulty attracting and retaining skilled personnel because of low pay, particularly for the professionals. In some cases, the lack of trained staff has created serious bottlenecks for government response to corruption cases. For example, there is only one documents expert in the country, and the wait for his services can be as long as a year or a year and a half, delaying completion of investigations. Other skills shortages that impede investigations are the lack of accounting and computer expertise (particularly relevant to white collar crime), and forensics and ballistics expertise. The shortage of trained prosecutors has put most of the burden of prosecuting cases on untrained police prosecutors. This not only effectively reduces the amount of time the CID has for its primary responsibility of investigating crime, but also contributes to the dismissal of cases for failure to prosecute or lack of evidence. Magistrates also lack training in economic crimes. The Auditor General’s office has a shortage of trained auditors, with consequences for the depth and quality of audits. While anticorruption agencies suffer these shortages, it should also be noted that skills shortages among those responsible for financial management, particularly at the district level, contribute to problems of corruption.

Lack of funds. Resource shortages have been felt across the board, even as anticorruption agencies are being asked to extend coverage because of decentralisation. They result in an inability to conduct in-house training, lack of vehicles, computers, and per diem money for staff that must travel. For example the CID has about Ug. Shs. 400,000 a month for each regional office to conduct investigations. The Inspectorate of the Judiciary consists of two persons with one vehicle who must cover the entire country.

Low salaries and uneven remuneration. Despite some salary increases as a result of public service reform, most government actors receive less than a living wage. There are substantial differences in salary for government actors attached to different services who have the same qualifications and performed the same tasks (e.g., prosecutors with the DPP, the IGG, and the CID; differences among judges). The need to assure basic needs is an important driving force for corrupt actions among the most poorly paid, while more generally, poor pay and pay differentials have been widely cited as demotivating staff and contributing to poor job performance.

Weak information management. The agencies require assistance in strengthening systems for records management and information sharing, in order to facilitate investigation, to assist in case tracking, and to maintain baseline performance statistics. For example, the CID, which has not benefited from donor support, lacks a single computer to help them track 50,000 annual complaints

Non-institutional factors. The struggle against corruption takes place against a background of a number of important social, historic, and cultural factors. Acute poverty means that underpaid civil servants are nevertheless responsible for numerous dependants. Uganda’s violent upheavals have promoted a culture of survival, and its history has not been conducive to the fostering of a sense of national ownership of the government and its resources. Uganda’s formal government institutions, including its 1995 Constitution, are new and their operation is not yet generally understood by the poorly educated population. Formal rules and institutions continue to be subordinated to family and social obligations. The fight against corruption requires not only institutional change, but also social and cultural change.

Kutokana na hayo hapo juu ni dhahiri kwamba hali ya Uganda kwa maana ya mikakati ya serikali kupambana na Rushwa haitofautiani sana na hii ya Tanzania kwa maana ya taasisi na hata mifumo na taratibu.
Labda tuangalie hizo changamoto zinazofanya vita dhidi ya Rushwa iwe ngumu.Mimi naona kama changamoto walizo nazo na sisi tunazo pia.
 
Back
Top Bottom