Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Jul 29, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ni maneno, malalamiko, manung'uniko, shutuma tu kila kukicha kulikoni? Tanzania haijawahi kupungukiwa na taasisi za kupambana na Rushwa. Wakati wa uhuru, Tanzania ilirithi Sheria ya wakoloni ya kupambana na Rushwa ya 1958, hadi 1971 wakati sheria ya Anti-corruption ilipopitishwa. Pia Permanent Commission of Enquiry ilianzishwa 1966 kuchunguza mienendo ya Rushwa iliyokuwa inafanywa na Viongozi wa juu wa Serikali na Siasa na kulalamikiwa na wananchi.Kutokana na kukuwa kwa tatizo la rushwa, mwaka 1975 serikali ikaanzisha kikosi cha kupambana na rushwa (Anti-Corruption Squad). Katikati ya miaka ya 1980, kikosi hiki kilionekana dhahiri kuwa hakifanyi kazi yake kikamilifu na hata watu kukibatiza “Corruption Squad”.

  1983 jitihada nyingine zilifanyika – Mahakama ya wahujumu Uchumi ilianzishwa (National Anti-Economic Sabotage Tribunal) ili kushughulikia washtakiwa waliokuwa wanatuhumiwa kuhujumu uchumi. Mwaka wa kwanza tu, kati ya watuhumiwa 4,216 waliofikishwa kwenye tribunal hiyo iliyoongozwa na Jaji Mrosso, washtakiwa 424 walionekana na hatia, 2,155 wakaachiwa baada ya kuonekana hawana hatia. Hata hivyo ilikuja kudhihirika kuwa wengi wa waliokamatwa kwa uhujumu walikuwa ni watu wa kawaida mno na hakukuwemo na watu wazito au mapapa na manyangumi wa Ufisadi kama wanavyojulikana leo.

  Miaka ya 1990 ilishuhudia hatua zaidi zikichukuliwa ambapo mwaka 1991 yakafanyika mabadiliko ya Kikatiba, na kubadilisha Anti-Corruption Squad kuwa the Prevention of Corruption Bureau (PCB). Mwaka 1995, ikaundwa Sheria ya maadili ya viongozi- the Public Leadership Code of Ethics kuwamulika viongozi wenye kutumia vibaya madaraka. Pia Sheria hii ikaunda Sekretariat iliyoongozwa na Commisioner wa Maadili.

  Pamoja na kuundwa kwa utitiri huu wa taasisi na Sheria, hadi kufikia katikati ya miaka ya 1990, hali ya Rushwa ilionekana kutisha – ikiwa imeingia kila nyanja ya maisha ya Mtanzania. Ndipo Rais wa awamu ya Tatu Bwana William Mkapa alipotangaza kupambana na rushwa kuwa ni kipaumbele katika utawala wake. Alianza kwa kuunda Tume iliyojulikana kama Tume ya Warioba (the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption) mwaka 1996. Mwenyekiti akiwa ni Jaji Joseph Warioba. Tume hii ilifanya kazi yake kwa kuchambua na kutafiti tatizo la rushwa nchini na kuandika taarifa iliyojulikana kama Warioba Report.Humo walionyesha visababishi vya rushwa kwa kirefu sana, na kupendekeza nini kifanyike. Aidha ilibainisha kuwa rushwa imeenea kila mahali na imesababishwa na uzembe na kukosekana kwa uwajibikaji katika taasisi za umma, ukosefu wa huduma muhimu, mishahara midogo kwa watumishi wa umma ukilinganisha na hali ya maisha inavyozidi kupanda siku hadi siku, mmomonyoko wa maadili/uadilifu kwa

  Ripoti ya Warioba ilipendekeza mambo kadhaa ambayo utekelezaji wake ulizaa urekebishwaji wa taasisi na mifumo mbalimbali ndani ya Serikali.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kusafisha safu ya juu ya uongozi na kuweka watu waadilifu, Rais kutoa Maagizo kwa viongozi wote kupambana na rushwa maeneo wanayoongoza, elimu kwa umma kufahamisha kuhusu haki zao, kuwaadhibu vikali wale wote walioonekana na makosa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao kisheria.

  Serikali ilichukua hatua kadhaa kama utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo hayo kama kuweka mpango mkakati wa kupambana na Rushwa (Nation Anti-Corruption Strategic Action Plan (NACSAP) wa mwaka 1999. Hii ilifuatiwa na kuanzishwa kwa Kitengo cha kuratibu Utawala bora - Good Governance Coordinating Unit mwaka 2000 ili kiwe kinasimamia utekelezwaji wa NACSAP pamoja na mambo mengine.Sanjari na hili pia ikaanzishwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - the Commission for Human Rights and Good Governance mnamo mwaka 2001. Kulifuatiwa na maboresho mengine kadhaa pamoja na kupitishwa kwa Sheria kadhaa ikiwa ni pamoja na Finance Act na Public Procurement Act (2001) iliyorekebishwa 2004, sheria iliyolenga kuongeza uwazi na uwajibikaji (transparency and accountability). Hii ni kwa uchache tu.Sheria hii imeshafanyiwa marekebisho zaidi.

  Nitaendelea kuwaletea mengine zaidi ila hadi wakati huo..tuchangie katika yafuatayo?
  Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.

   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tunafanya makosa tukidhania kuwa watu wale wale wale, wenye fikra zile zile, na malengo yale yale wanaweza kubadilika wasiwe watu wale wale!
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  naomba ianze hivi "Tunafanya makosa tukidhania kuwa chama kile kile cha watu wale wale ........
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tuache ulimbukeni wa kukimbilia kuilaumu CCM, hili suala halihusu siasa wala chama fulani. Ni suala la kitaifa linalomuhusu kila Mtanzania.

  Rushwa: wananchi hawako tayari kupambana na rushwa.!! Why? kwa sababu sheria zilizopo zinatosha kuwapa shida wala rushwa wachache hazitumiwi na wananchi. Wananchi wanakata tamaa badala ya kulalamika na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria wanaona hakuna la kufanya, wanaona ni afadhali na wao wale rushwa kuliko kuhangaika kupambana na rushwa.

  Wananchi wanatakiwa kubadilika (kama ni kwa kuelimishwa au kwa wao wenyewe kuchoka) wawe wakali dhidi ya wala rushwa popote pale walipo. Rushwa isionewe aibu kuanzia majumbani hadi maofisini ndipo Taifa litafanikiwa kupambana na Rushwa. Vita ya rushwa inafaa ipiganwe kama au sambamba na AIDS, kila mmoja ajione ana jukumu la kupambana na rushwa pale alipo kwa vitendo na sio kulaumu kwa maneno matupu.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na kosa kubwa ni kuwa tumewaruhusu watufanye sisi tudhani hivyo
   
 6. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #6
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  1.Wala rushwa, mafisidi wahujumu uchumi hawa wajibishwi ipasavyo. wananchi tunakata tamaa.
  2. Tunapenda sana shortcuts mf hatulipi kodi, bills za maji, umeme. Tunatafuta mtu atufanyie 'proposa' ili tukwepe kulipa. This fuels rushwa.
  3. ....
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hawajibishwi ipasavyo -huenda hapo ndio tatizo ila labda uende hatua zaidi - ungeshauri wawajibishwe vipi?
  Mlolongo wa kutumia Sheria na ustaarabu ndio unafanya hakuna mabadiliko katika miendo y aRushwa.Angalia mchakato wa upelelezi, na kushtakiwa watu wa EPA hadi leo..nini kinaendelea?
   
 8. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Wananchi hawajachukia rushwa ipasavyo. Wengi wao hawawezi kuishi bila kutoa/kupokea rushwa. Rushwa ni rafiki yetu watanzania.
  Lakini nafikiri Obama alisema vizuri zaidi huko Ghana kwamba inabidi tuwekeze kwenye taasisi na siyo miungu watu "we need strong institutions".Tunaogopa sana watu na siyo sheria.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Rushwa imeshageuka utamaduni..njia ya maisha kwa watanzania.Pamoja na kuwa watu "wanachukia" rushwa, bado wanaiendekeza.....wanashiriki..kutoa na kupokea..kuanzia wasio na kitu hadi wenye vitu.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,490
  Likes Received: 81,808
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kuna ulimbukeni kuilaumu CCM chama ambacho kimekuwa madarakani tangu tupate uhuru miaka 48 iliyopita. Bunge kama watunga sheria zetu na Serikali kama waangalizi wa kuhakikisha sheria zetu zinafuatwa wote wamezembea na matokeo yake sasa hivi nchi inaendeshwa kama haina sheria.

  Pamoja na kuwa hili swala linamuhusu kila Mtanzania lakini wa kulaumiwa ni wale ambao tumewapa dhamana ya kuhakikisha sheria za nchi yetu ili kuhakikisha utawala bora zinafuatwa bila upendeleo wowote na Watanzania wote. Na hawa si wengine bali ni CCM ambao ndiyo wameunda Serikali iliyo madarakani.

  Angalia jinsi tume zinavyoundwa kila kukicha kuchunguza ufisadi mbali mbali ndani ya chama na serikali. Tume hizo zinapomaliza kazi zao na kutoa recommendations zao Serikali ya chama tawala inakuja na maamuzi yao ya kuendelea kukingia kifua wahusika mbali mbali ndani ya chama na serikali.

  Angalia akina Rostam, Mkapa, Karamagi, Lowassa, Mramba, Msabaha, Chenge na wengineo wengi ambao kwa maoni yangu walistahili kufukuzwa CCM kutokana na madhambi yao makubwa waliyoyafanya ndani ya nchi yetu lakini hadi hii leo bado CCM imewakumbatia na hata kuwapigia debe kwamba watu hawa ni safi kabisa. Sasa hapa wa kulaumu ni nani kama si chama tawala!? ambacho kinaendekeza kulea maovu mbali mbali yanayofanywa na wanachama na viongozi mbali mbali hata wale ambao wamewahi kuwa na nyadhifa za juu katika chama hicho au serikali.

  Wananchi wanajitahidi kadri ya uwezo wao tumeona wananchi wakianza kuwazomea viongozi mbali mbali wa CCM katika baadhi ya mikoa yetu lakini CCM kwa kutumia tume ya uchaguzi bado wananunua kura, kuwahonga wananchi mashati, fulana, vyakula, magodoro ili kuhakikisha wanaendelea kushinda kila chaguzi. Tume ya uchaguzi inaona uozo wote unaofanywa na CCM lakini inafumba macho na kuwaruhusu CCM wafanye watakavyo bila tume hiyo kutoa sauti ili kukemea ukiukwaji wa sheria za uchaguzi unaofanywa na CCM ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa.

  Kwa hiyo kwa maoni yangu ushahidi chungu nzima uliokuwepo unaonyesha dhahiri kwamba CCM haioni umuhimu wowote wa kupambana na ufisadi ndiyo maana mafisadi chungu nzima ndani ya chama na serikali hadi hii leo hawajashughulikwa na baada ya uchaguzi wa 2010 wote hawa wataachiwa huru kwa kukosekana 'ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani'

  Hivyo kwa serikali ya CCM kutoona umuhimu wa kuwaadhibu pamoja na kuwafilisi mafisadi wote ndani ya chama chao na Serikali iliyoundwa na chama chao kwa kutumia sheria zetu tulizonazo wanastahili kabisa kulaumiwa kwa kuendelea kuwakumbatia mafisadi na hivyo kushindwa kupambana na mafisadi maana wanajua mafisadi na ufisadi ndiyo vitu viwili vinavyoendelea kuiweka CCM madarakani na kamwe hawatafanya lolote lile ili kuhakikisha sheria kali za nchi zinatumika dhidi ya mafisadi.

  Tumeona majirani zetu, Zambia na Malawi wameweza kuwapandisha kizimbani Marais wastaafu wao kwa kutumia madaraka yao vibaya ili kujitajirisha lakini kamwe hili halitatokea ndani ya Tanzania kwa kuwa CCM ni chama kilichoshikwa na mafisadi si chama cha Wakulima na Wafanyakazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
   
  Last edited: Jul 30, 2009
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  - Kwanza kujibu swali la WOS, ni kwamba kauli wapi tunafanya makosa by itself ni makosa pia kwa sababu ili binadamu ufanye makosa, maana yake ni kwamba at onetime uliwahi kutofanya makosa, something Tanzania hatujawahi kufanya toka tupate uhuru kila tunachofanya imekua ni makosa tu, labda swali lingekua ni lini tuta get things right? Maana hatujawahi!

  - Mkulu BAK, ni kweli kosa ni la bunge la jamhuri ambalo lina CUF, CCM, Chadema na TLP, yaani wananchi wote tunawakilishwa humo, kwa maneno mengine ni sisi wananchi ndio tunapenda ufisadi na rushwa hawa viongozi si ni reflection yetu wananchi wa Tanzania ndio maana kila uchaguzi tunawachagua hao hao.

  Mpaka wananchi tutakapokuwa tayari kubeba responsibility kwamba viongozi wanatufanyia tunayoyapenda tu na sio anything else, tutaendelea kutafutana uchawi bila kupiga hatua yoyote mbele, kwenye hivi vyama vya siasa hakuna alternative yoyote ni wale wale tu, almost wote zamani walikuwa viongozi wa CCM, wakahamia Upinzani, hakuna jipya mpaka kina the kitilas watakaposhika ngazi.

  - Sasa hivi the dataz ni kwamba Lowassa atarudi tena kwa kishindo cha ajabu na sasa ninaziamini sana hizi habari kuliko huko nyuma, kwa sababu ni hivi karibuni sana one on one, alimwambia Lukaza asijali sana na ile kesi ya EPA maana haipo tena na akamtaka aendelee na biashara zake bila uoga wowote na kwamba soon mambo yatakuwa mazuri sana, sasa hivi Lukaza yuko on top of his form tena kama zamani, sasa eti hii nguvu Lowassa anaipata wapi kama hapewi na sisi wananchi? Nasikia baadhi ya viongozi waliomuandama huko nyuma sasa wanajipanga kwake kwa siri siri saa za usiku! Tanzania tuna laana flani hivi tumuombe Mungu aiondoe kabla hatujaenda mbali! maana tufwile mwee!  Respect.

  Field Marshall Emergency System.
   
 12. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni azma thabiti ya kupambana na rushwa, viongozi wetu hawana nia thabiti ya kupambana na rushwa. Lao ni Usanii mtupu! Tulipoona Tanzania imedorora katika soka tulikwenda Brazil nchi mahiri kisoka kutafuta kocha mtaalamu katika soka-Maximo. Leo sisi si kichwa cha mwenda wazimu... Katika Ufisadi kama tumeshwindwa kwanini tunaona aibu kwenda Cuba au China kutafuta mtaalamu atakae chukua nafasi ya kikargosi cha mafisadi Bw. Hosea wa kuongoza mbinu mpya za kupambana na ufisadi? Naamini watanzania wapo tayari kuwalipa wataalumu wa nje kupambana na ufisadi zaidi ya fedha anazolipwa Maximo kocha wa soka toka Brazil
   
 13. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mi nadhani sasa tuhamishe vita kutoka mhimili wa executive hadi wa sheria tuwachambue hawa maofisa(majaji na mahakimu) mmoja hadi mwingine tuwasukume nao wawajibike katika eneo lao kuliko kuendelea kuishutumu serikali ambayo kwa kiasi fulani imewezesha hata hao wachache kufika kizimbani.hawa waheshimiwa wanakula kiulaini kwa vile wao hawana upinzani wa CUF wala chadema!!!!
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0

  - Mkulu Zed, chonde chonde kaka, sisi wananchi wa taifa hili ni watu wa ajabu sana na hatuna mfano dunia nzima, hili la kocha wa mpira bado kumbe hujaelewa kwamba ni changa la macho, hivi unajua kuwa political base ya Muungwana ni wananchi flani hivi wasioelewa anything, zaidi ya kupenda penda mipira mipira ndio maana akaletwa kocha kwa amri ya rais wetu mwenye nguvu za ajabu sana maana hata King George hakuwa nazo, hawa wananchi as long as kuna habari za rais kujali mipira mipira ya Yanga na Simba kama anavyofanya, they could careless na ishus za ufisadi na rushwa, sasa the bad news ni kwamba hawa ndio wapiga kura mazee sasa unaona haya ya mipira yalivyo changa la macho!

  - Sisi ni wananchi wa ajabu sana duniani mkuu, wewe hata Iran sasa wananchi hawataki mambo yasiyoeleweka, sisi ndio kwanza tunalilia mahakama ya kadhi, sheria za jamhuri zimetushinda sio tu kuzisimamia bali hata kudai zitumike, matokeo yake Mtikila alipotaka kumfungulia mashitaka Marehemu Ditopile, ili arudi rumande anakostahili kisheria baada ya kuua mwananchi malalahoi tena helpless na bastola, wakatokea wananchi flani wa dini ya Ditopile na kumtaka Mtikila aache mara moja kuingilia dini ya Ditopile, juzi nimeona kichwa cha habari ya media "Shehe Yahaya amjia juu Pinda", yaani we are so empty hata hawa watabiri viganja yaani kwa jina lingine wachawi au magicians wana ujiko politically mbele ya hii jamiii, sasa masikini ya Mungu tunajiuliza eti tulikosea wapi as if kuna wakati tuliwahi kuwa on the right track, Mungu alibariki tu hili taifa lakini hakuna hope na hii generation, tumedai hatutaki viongozi wazee, haya sasa tuna viongozi vijana kina Masha na Nchimbi, kumbe chupa ni ile ile ya zamani ila tumebadili mvinyo tu ndani yake!

  Tuendelee tu kuwapigia kelele hapa JF, kuliko kuwaacha kabisa wakajisahau!

  Field Marshall Es!
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kifupi chake - NDIVYO TULIVYO.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Field Marshall Es,
  Mkuu, kwa mtu mwenye kufahamu unazungumzia upande mmoja tu, ama kweli nyani huwa haoini kundule...Hii ikiwa na maana wewe unawaona watu kama Waislaam tu kuwa wao ndio wenye makosa, inawezekana kabisa ktk fikra zako hata Kikwete unafikiria makosa yake yanatokana na kuwa Muislaam...Ya Ufisadi yameshakuwa ya Waislaam, duh! nina hakika hizi ndizo mbinu za kanisa tunazishtukia tayari mkuu wangu tunajua kinachoendelea...
  Now, vita imegeuka sio against mafisadi tena ila waislaam - heeee!...mkuu, hatutafika mkuu wangu, ya Nigeria yatakuja wala sii muda, kwani waislaam sii watu wa kutiwa vidole vya macho wakanyamaza..Diversity ni pamoja na wewe kukubali ya wengine sio sisi tukubali na kuvumilia yako tu.
  Kaazi kweli kweli ..ndio Maana nakubali kabisa maneno ya Nyani Ngabu - NDIVYO TULIVYO..
   
  Last edited: Jul 30, 2009
 17. S

  Shamu JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni Ujamaa ndiyo uliosababisha hayo matatizo ya Ufisadi. Sasa hivi afadhali tuna Freedom, na technology mambo yanaweza kubadilika.
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Bob Mkandara, Katika hoja yote ya FMES ni hiyo mifano ya kidini tu ndio umeiona.??!!
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ni muhimu sana kuhakikisha tunadumisha 'separation of powers'. Yani bunge liweze kukaa na kujadili serikali kwa uwazi bila kuhofia chochote au affiliation za chama, mahakama kuwa wazi zaidi na serikali kujisafisha. Tatizo nionalo ni hivyo vyombo vyote vya kusimamia rushwa kama PCB, NACSAP viko chini ya serikali. Kama ingewezekana na kwa kusudi la kuvifanya viwe huru zaidi vingewekwa chini ya Bunge, yani vinajibu directly kwa bunge na sio Serikali.
   
 20. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  FMES

  Mtazamo wako ni uko on the spot. Wananchi wengi wanakimbia ukweli huo kwa sababu wanatamani mabadiliko ya haraka.

  BAK

  Wananchi wana jukumu kubwa sana la kubadilisha hali ilivyo Tanzania. CCM unayoiongelea wewe ni ile ya kusoma kwenye magazeti, sio CCM halisi. Mkuu ukiijua CCM yenyewe utakubaliana na mimi kuwa kama Chama, CCM haina matatizo ambayo wananchi wanayaona kwenye Serikali. Hakuna mtu ndani ya CCM anayethubutu kuifanyia CCM ufisadi ambao unafanywa Serikalini.!! Hela ya CCM ni chungu sana haitafunwi ki-rahisi kama ilivyo Serikalini. Sasa jiulize, kwanini hali inakuwa hivyo; jibu lake ni kuwa kwenye CCM taratibu za kuathibiwa ndani ya Chama ziko wazi kwa kila mwana CCM kuzielewa na kuzifuata kama inavyotakiwa, wanaziogopa. Ndio maana hata utakuwa wabunge wetu wanakuwa na waoga sana mpaka wakati mwingi wanaonekana kulinda maslahi ya chama zaidi ya Taifa. Amini usiamini, Wanachama na viongozi wa CCM wanajuwa kulinda rasilimali na maslahi ya chama chao. Tena wanapiga vita rushwa ndani ya chama chao; unakumbuka Manji alishinda kura za maoni ya Ubunge kule Kigamboni 2005, na wale viongozi wa Arusha waliokamatwa na PCCB, Uchaguzi wa UVCCM n.k? Hii inaonyesha wana CCM wanatimiza majukumu kwenye CCM yao.

  Umesema kuwa ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wa CCM wananunua kura; hizo kura lazima ziwe na wauzaji kabla hazijanunuliwa na mtu yoyote..!! Hii inathibitisha kuwa ili mradi wagombea bado wanashinda uchaguzi kwa kuhonga hela nyingi, ni lazima washindi watafanya kila liwalo warudishe hela zao. Wananchi tuna uwezo wa kukataa kuuza kura zetu. Mifano ya kukaa huko ninakozungumzia ipo wazi; jimbo la Moshi Mjini, Tarime na kwingineko ambako Wapinzani wameshinda zaidi ya mara moja.

  Wananchi kwa ujumla tunatakiwa kutimiza majukumu yetu dhidi ya adui rushwa kwenye Serikali na vyombo vyote vya umma. CCM itawawajibisha wanachama wake walioko Serikali pale itakapoona inatishiwa maslahi yake kwa namna moja au nyingine. Ni fikra potofu kutegemea CCM watagombana na wana CCM wenzao kulinda maslahi ya Wananchi wakati ambapo Wanachi walio wengi wala hawajui jinsi ya kutetea maslahi yao. Wale wachache walioko mijini hawataki/ wavivu kujisumbua kutetea haki. Mfano ni tatizo la umeme ambao unaathiri wakazi wa mijini zaidi kuliko vijijini; lakini ulisikia kikundi au mtu mmoja mmoja ametumia sheria zilizopo kulalamika kwa vitendo? Jibu ni Hapana..!!

  Mara kwa mara wala rushwa tunawaona ndio wajanja na wenye kustahili heshima kwenye jamii yetu. Tunawajua wala rushwa, ni ndugu zetu, jamaa na marafiki, tunaishi nao, tunafanya nao kazi n.k. Yes, inatakiwa tuanze na hawa kwa kuwashughulikia kwa vitendo. Tunaweza kuanza kwa kutokutamani mali walizochuma kwa njia za rushwa na kuwaonyesha dharau wanazostahili.
   
Loading...