Mapambano dhidi ya Ufisadi - wapi tunafanya makosa?

Ni maneno, malalamiko, manung'uniko, shutuma tu kila kukicha kulikoni?

Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.

Ewe Mwanamke mwema wa Shoka, ni njia ipi unaitumia kupambana na nafsi yako? Je, ni kwa kujipiga ngumi na vibao? Au ni kwa kujibana, kujinyima na kuikana nafsi?

Ni kosa kubwa moja tu tunalolifanya katika kupambana na ufisadi. Jana nilipita kwenye ofisi mpya ya Takukuru nikaangalia picha za viongozi wake wote wakuu toka enzi za Mwalimu Nyerere zilizobandikwa mapokezi. Je, unajua wako wangapi? Idadi yao haitofautiani sana na idadi ya marais ambao tumekuwa nao toka wakati wa uhuru. Kuna fumbo hapo.

Najaribu kusema nini hapo juu? Ni kile kile nachokisema kila siku. Kuwa ufisadi u ndani ya nafsi zetu. Hivyo hatuwezi kupambana nao bila kupambana na nafsi zetu!

Reference: Tanzania: What If Corruption is Within You?
 
QUOTE=WomenofSubstanc;536094]Ni maneno, malalamiko, manung'uniko, shutuma tu kila kukicha kulikoni? Tanzania haijawahi kupungukiwa na taasisi za kupambana na Rushwa. Wakati wa uhuru, Tanzania ilirithi Sheria ya wakoloni ya kupambana na Rushwa ya 1958, hadi 1971 wakati sheria ya Anti-corruption ilipopitishwa. Pia Permanent Commission of Enquiry ilianzishwa 1966 kuchunguza mienendo ya Rushwa iliyokuwa inafanywa na Viongozi wa juu wa Serikali na Siasa na kulalamikiwa na wananchi.Kutokana na kukuwa kwa tatizo la rushwa, mwaka 1975 serikali ikaanzisha kikosi cha kupambana na rushwa (Anti-Corruption Squad). Katikati ya miaka ya 1980, kikosi hiki kilionekana dhahiri kuwa hakifanyi kazi yake kikamilifu na hata watu kukibatiza “Corruption Squad”.

1983 jitihada nyingine zilifanyika – Mahakama ya wahujumu Uchumi ilianzishwa (National Anti-Economic Sabotage Tribunal) ili kushughulikia washtakiwa waliokuwa wanatuhumiwa kuhujumu uchumi. Mwaka wa kwanza tu, kati ya watuhumiwa 4,216 waliofikishwa kwenye tribunal hiyo iliyoongozwa na Jaji Mrosso, washtakiwa 424 walionekana na hatia, 2,155 wakaachiwa baada ya kuonekana hawana hatia. Hata hivyo ilikuja kudhihirika kuwa wengi wa waliokamatwa kwa uhujumu walikuwa ni watu wa kawaida mno na hakukuwemo na watu wazito au mapapa na manyangumi wa Ufisadi kama wanavyojulikana leo.

Miaka ya 1990 ilishuhudia hatua zaidi zikichukuliwa ambapo mwaka 1991 yakafanyika mabadiliko ya Kikatiba, na kubadilisha Anti-Corruption Squad kuwa the Prevention of Corruption Bureau (PCB). Mwaka 1995, ikaundwa Sheria ya maadili ya viongozi- the Public Leadership Code of Ethics kuwamulika viongozi wenye kutumia vibaya madaraka. Pia Sheria hii ikaunda Sekretariat iliyoongozwa na Commisioner wa Maadili.

Pamoja na kuundwa kwa utitiri huu wa taasisi na Sheria, hadi kufikia katikati ya miaka ya 1990, hali ya Rushwa ilionekana kutisha – ikiwa imeingia kila nyanja ya maisha ya Mtanzania. Ndipo Rais wa awamu ya Tatu Bwana William Mkapa alipotangaza kupambana na rushwa kuwa ni kipaumbele katika utawala wake. Alianza kwa kuunda Tume iliyojulikana kama Tume ya Warioba (the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption) mwaka 1996. Mwenyekiti akiwa ni Jaji Joseph Warioba. Tume hii ilifanya kazi yake kwa kuchambua na kutafiti tatizo la rushwa nchini na kuandika taarifa iliyojulikana kama Warioba Report.Humo walionyesha visababishi vya rushwa kwa kirefu sana, na kupendekeza nini kifanyike. Aidha ilibainisha kuwa rushwa imeenea kila mahali na imesababishwa na uzembe na kukosekana kwa uwajibikaji katika taasisi za umma, ukosefu wa huduma muhimu, mishahara midogo kwa watumishi wa umma ukilinganisha na hali ya maisha inavyozidi kupanda siku hadi siku, mmomonyoko wa maadili/uadilifu kwa

Ripoti ya Warioba ilipendekeza mambo kadhaa ambayo utekelezaji wake ulizaa urekebishwaji wa taasisi na mifumo mbalimbali ndani ya Serikali.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kusafisha safu ya juu ya uongozi na kuweka watu waadilifu, Rais kutoa Maagizo kwa viongozi wote kupambana na rushwa maeneo wanayoongoza, elimu kwa umma kufahamisha kuhusu haki zao, kuwaadhibu vikali wale wote walioonekana na makosa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao kisheria.

Serikali ilichukua hatua kadhaa kama utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo hayo kama kuweka mpango mkakati wa kupambana na Rushwa (Nation Anti-Corruption Strategic Action Plan (NACSAP) wa mwaka 1999. Hii ilifuatiwa na kuanzishwa kwa Kitengo cha kuratibu Utawala bora - Good Governance Coordinating Unit mwaka 2000 ili kiwe kinasimamia utekelezwaji wa NACSAP pamoja na mambo mengine.Sanjari na hili pia ikaanzishwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - the Commission for Human Rights and Good Governance mnamo mwaka 2001. Kulifuatiwa na maboresho mengine kadhaa pamoja na kupitishwa kwa Sheria kadhaa ikiwa ni pamoja na Finance Act na Public Procurement Act (2001) iliyorekebishwa 2004, sheria iliyolenga kuongeza uwazi na uwajibikaji (transparency and accountability). Hii ni kwa uchache tu.Sheria hii imeshafanyiwa marekebisho zaidi.

Nitaendelea kuwaletea mengine zaidi ila hadi wakati huo..tuchangie katika yafuatayo?
Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.

[/QUOTE]
Tuondoe siasa katika kupamabanab na rushwa tuta fanikiwa,
 
Bila kuondoa Siasa katika kupambana na rushwa itatuchukua miaka kupambana na rushwa,Kila atakae kamatwa tunamuonea haya kwa vile ni mwenzetu.wanaoteuliwa kupambana na rushwa ni walewale wenzao nani atamkamata mwenzake,pili ili tukomeshe Rushwa tufunge ofisi za kupambana na rushwa na kazi hiyo ifanywe na Polisi kwani watu wanageuza dili na hivyo kuendeleza rushwa.unapojenga majengo ya kudumu kwa ajili ya kupambana na rushwa maana yake umehalalisha iwepo maisha yote.
 
The answer is simple.Sisi wenyewe ni mafisadi kwa njia moja au nyingine.Huwezi kumnyoshea kidole mwenzio kwamba ni mchafu wakati wewe mwenyewe ni mchafu.Ili uweze kuwa na authority ya kumnyoshea mwenzio kidole ni lazima wewe mwenyewe uwe msafi.As long as sisi wenyewe ni wachafu kwa njia yeyote ile, hatuwezi kamwe kufanikiwa.Let us start with ourselves!

Ni maneno, malalamiko, manung'uniko, shutuma tu kila kukicha kulikoni? Tanzania haijawahi kupungukiwa na taasisi za kupambana na Rushwa. Wakati wa uhuru, Tanzania ilirithi Sheria ya wakoloni ya kupambana na Rushwa ya 1958, hadi 1971 wakati sheria ya Anti-corruption ilipopitishwa. Pia Permanent Commission of Enquiry ilianzishwa 1966 kuchunguza mienendo ya Rushwa iliyokuwa inafanywa na Viongozi wa juu wa Serikali na Siasa na kulalamikiwa na wananchi.Kutokana na kukuwa kwa tatizo la rushwa, mwaka 1975 serikali ikaanzisha kikosi cha kupambana na rushwa (Anti-Corruption Squad). Katikati ya miaka ya 1980, kikosi hiki kilionekana dhahiri kuwa hakifanyi kazi yake kikamilifu na hata watu kukibatiza “Corruption Squad”.

1983 jitihada nyingine zilifanyika – Mahakama ya wahujumu Uchumi ilianzishwa (National Anti-Economic Sabotage Tribunal) ili kushughulikia washtakiwa waliokuwa wanatuhumiwa kuhujumu uchumi. Mwaka wa kwanza tu, kati ya watuhumiwa 4,216 waliofikishwa kwenye tribunal hiyo iliyoongozwa na Jaji Mrosso, washtakiwa 424 walionekana na hatia, 2,155 wakaachiwa baada ya kuonekana hawana hatia. Hata hivyo ilikuja kudhihirika kuwa wengi wa waliokamatwa kwa uhujumu walikuwa ni watu wa kawaida mno na hakukuwemo na watu wazito au mapapa na manyangumi wa Ufisadi kama wanavyojulikana leo.

Miaka ya 1990 ilishuhudia hatua zaidi zikichukuliwa ambapo mwaka 1991 yakafanyika mabadiliko ya Kikatiba, na kubadilisha Anti-Corruption Squad kuwa the Prevention of Corruption Bureau (PCB). Mwaka 1995, ikaundwa Sheria ya maadili ya viongozi- the Public Leadership Code of Ethics kuwamulika viongozi wenye kutumia vibaya madaraka. Pia Sheria hii ikaunda Sekretariat iliyoongozwa na Commisioner wa Maadili.

Pamoja na kuundwa kwa utitiri huu wa taasisi na Sheria, hadi kufikia katikati ya miaka ya 1990, hali ya Rushwa ilionekana kutisha – ikiwa imeingia kila nyanja ya maisha ya Mtanzania. Ndipo Rais wa awamu ya Tatu Bwana William Mkapa alipotangaza kupambana na rushwa kuwa ni kipaumbele katika utawala wake. Alianza kwa kuunda Tume iliyojulikana kama Tume ya Warioba (the Presidential Commission of Inquiry Against Corruption) mwaka 1996. Mwenyekiti akiwa ni Jaji Joseph Warioba. Tume hii ilifanya kazi yake kwa kuchambua na kutafiti tatizo la rushwa nchini na kuandika taarifa iliyojulikana kama Warioba Report.Humo walionyesha visababishi vya rushwa kwa kirefu sana, na kupendekeza nini kifanyike. Aidha ilibainisha kuwa rushwa imeenea kila mahali na imesababishwa na uzembe na kukosekana kwa uwajibikaji katika taasisi za umma, ukosefu wa huduma muhimu, mishahara midogo kwa watumishi wa umma ukilinganisha na hali ya maisha inavyozidi kupanda siku hadi siku, mmomonyoko wa maadili/uadilifu kwa

Ripoti ya Warioba ilipendekeza mambo kadhaa ambayo utekelezaji wake ulizaa urekebishwaji wa taasisi na mifumo mbalimbali ndani ya Serikali.Baadhi ya mapendekezo ni pamoja na kusafisha safu ya juu ya uongozi na kuweka watu waadilifu, Rais kutoa Maagizo kwa viongozi wote kupambana na rushwa maeneo wanayoongoza, elimu kwa umma kufahamisha kuhusu haki zao, kuwaadhibu vikali wale wote walioonekana na makosa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao kisheria.

Serikali ilichukua hatua kadhaa kama utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo hayo kama kuweka mpango mkakati wa kupambana na Rushwa (Nation Anti-Corruption Strategic Action Plan (NACSAP) wa mwaka 1999. Hii ilifuatiwa na kuanzishwa kwa Kitengo cha kuratibu Utawala bora - Good Governance Coordinating Unit mwaka 2000 ili kiwe kinasimamia utekelezwaji wa NACSAP pamoja na mambo mengine.Sanjari na hili pia ikaanzishwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora - the Commission for Human Rights and Good Governance mnamo mwaka 2001. Kulifuatiwa na maboresho mengine kadhaa pamoja na kupitishwa kwa Sheria kadhaa ikiwa ni pamoja na Finance Act na Public Procurement Act (2001) iliyorekebishwa 2004, sheria iliyolenga kuongeza uwazi na uwajibikaji (transparency and accountability). Hii ni kwa uchache tu.Sheria hii imeshafanyiwa marekebisho zaidi.

Nitaendelea kuwaletea mengine zaidi ila hadi wakati huo..tuchangie katika yafuatayo?
Ni wapi tunakosea katika vita dhidi ya rushwa kwa maana Rushwa imekuwepo toka ukoloni ndio maana sheria ilikuwepo; baada ya uhuru tunaona jitihada chungu nzima lakini rushwa bado inaibuka kidedea.

Sidhani kama kuna ulimbukeni kuilaumu CCM chama ambacho kimekuwa madarakani tangu tupate uhuru miaka 48 iliyopita. Bunge kama watunga sheria zetu na Serikali kama waangalizi wa kuhakikisha sheria zetu zinafuatwa wote wamezembea na matokeo yake sasa hivi nchi inaendeshwa kama haina sheria.

Angalia jinsi tume zinavyoundwa kila kukicha kuchunguza ufisadi mbali mbali ndani ya chama na serikali. Tume hizo zinapomaliza kazi zao na kutoa recommendations zao Serikali ya chama tawala inakuja na maamuzi yao ya kuendelea kukingia kifua wahusika mbali mbali ndani ya chama na serikali.

Angalia akina Rostam, Mkapa, Karamagi, Lowassa, Mramba, Msabaha, Chenge na wengineo wengi ambao kwa maoni yangu walistahili kufukuzwa CCM kutokana na madhambi yao makubwa waliyoyafanya ndani ya nchi yetu lakini hadi hii leo bado CCM imewakumbatia na hata kuwapigia debe kwamba watu hawa ni safi kabisa. Sasa hapa wa kulaumu ni nani kama si chama tawala!? ambacho kinaendekeza kulea maovu mbali mbali yanayofanywa na wanachama na viongozi mbali mbali hata wale ambao wamewahi kuwa na nyadhifa za juu katika chama hicho au serikali.

Kwa hiyo kwa maoni yangu ushahidi chungu nzima uliokuwepo unaonyesha dhahiri kwamba CCM haioni umuhimu wowote wa kupambana na ufisadi ndiyo maana mafisadi chungu nzima ndani ya chama na serikali hadi hii leo hawajashughulikwa na baada ya uchaguzi wa 2010 wote hawa wataachiwa huru kwa kukosekana 'ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani'

Hivyo kwa serikali ya CCM kutoona umuhimu wa kuwaadhibu pamoja na kuwafilisi mafisadi wote ndani ya chama chao na Serikali iliyoundwa na chama chao kwa kutumia sheria zetu tulizonazo wanastahili kabisa kulaumiwa kwa kuendelea kuwakumbatia mafisadi na hivyo kushindwa kupambana na mafisadi maana wanajua mafisadi na ufisadi ndiyo vitu viwili vinavyoendelea kuiweka CCM madarakani na kamwe hawatafanya lolote lile ili kuhakikisha sheria kali za nchi zinatumika dhidi ya mafisadi.

]

Babu ataka Kusema!

Umeweka mjadala sawa sawa. Nakushukuru sana kwa niaba ya watu makini wote hapa jamii.
Mfumo mbaya uliojengwa na CCM kuanzia kabla ya uhuru ikiwa TANU hadi leo CCM ndilo tatizo kubwa na kila mara wamekuwa wakibadili majina na maneno tu ili waendelee kula starehe,

Ukweli ni kwamba rushwa,mlungula ,kitu kidogo,asilimia kumi,takrima na mlolongo wa majina kibao yamekuwa yakibuniwa na waunda mipango /sera na mikakati wa CCM.

Rushwa imekuwepo tangu wakati wa Jesus Christ wa Nazareth aliyeuzwa kwa vipande 30 vya pesa ya wakati huo na YUDA Iskariote aliyekuwa mwanafunzi wake!

CCM kwa dhati kabisa haina mpango wa kupambana na rushwa period!

Mfano uliotoa hapo juu uko wazi ona swala la RICHMOND serikali ilikuwa inajua kinachoendelea nina maana Kikwete alikuwa na taarifa laikini badala ya kuchukua hatua akamwagiza Hosea achunguze na ripoti ya wachunguzi wa PCCB ilibadilishwa na Hosea kwa maslahi ya Lowasa na Rostam Aziz -pamoja na Nizar Karamagi , RAIS kama mcha mungu hilo aliambiwa lakini kama ilivyokuwa tabia ya CCM bunge likamwokoa na kuunda tume iliyofanya uchunguzi huru na kutoa mapendekezo murua ambayo wale wahusika vinara waliachia Ngazi,

Kama serikali ya CCM ingekuwa haipo kulinda rushwa ilipaswa kuwatimua wote walitajwa na KAMATI ya Mwakyembe kwani hizo nafasi walizo nazo walipewa tu na sio haki yao ya kuzaliwa! kuanzia John Mwanyika, Edward Hosea, Arthur Mwakapugi na wengineo wote hata kama ni kwa bahati mbaya ili kuonyesha kwamba CCM iko makini.

Pamoja na hayo Kikwete anaogopa nini kuwafukuza uanachama walijihusisha na hizi kashfa kuanzia akina Chenge, Msabaha, Lowasa , Karamagi, Mramba na kadhalika kama sio kulea rushwa. Hamtaweza kunihakikishia kwamba Kikwete sio mla rushwa tena mzuri tu mbona kuna mifano hai Kwa mfano Dr.Idris Rashid alitolewa BOT kwa scandal akaenda kuganga njaa kule NBC( Sijawahi kuona hapa duniani Gavana wa Benki kuu kuijdhalilisha na kwenda kufanya kazi Benki ya kawaida alipaswa tu kwa hadhi ile apumike aombwe ushauri) wakaiuza akiwa na Yona na alipewa asilimia akarudi mtaani ! Mwaka 2006 November JMK kwa ushauri wa RA AKAMPATIA mkataba wa miaka mitatu ili aiue TANESCO huku akijua waligawana na Chenge pesa za RADA!!

LEO HII TUNASIKIA KUNA UFISADI MKUBWA TANESCO lakini yule bwana mdogo waziri Ngeleja alitakiwa amsimamishe kazi mara moja kufanyike uchunguzi na akiwa Mwanasheria anaunda tume na waziri mkuu kilaza Pinda anacheka including the smiling president hapo rushwa itadumu. Hamkumbuki jinzi akina Zitto walivyopewa pesa na Dr. Idris ili Mitambo ya Bosi wake RA inunuliwe na kutishia kuleta giza nchi nzima ifikapo Agosti na bado rais akimsifu!!

Tuache mchezo CCM wana ndoa na RUSHWA mpaka kifo kitakapowatenganisha!!
 
Bila kuondoa Siasa katika kupambana na rushwa itatuchukua miaka kupambana na rushwa,.

Siasa ni kila kitu... kwa kifupi maisha ya binadamu ni siasa kuanzia mtu na mtu/mke/mume, familia, na jamii kwa ujumla ni siasa tupu.Tunaondoaje siasa?

Isitoshe katika mazingira yetu yalivyo, hutaweza kufanya kitu bila kuwepo na utashi wa kisiasa ( political will).Nadhani kinachotakiwa ni kwa uongozi wa juu kuvalia njuga kwa nia ya kweli bila kumuonea haya mtu yeyote na kuuma risasi( bite the bullet..simaanishi kumuua mtu ni msemo tu).Sasa basi kila tukiangalia nguvu kubwa sana inawekwa kuanzisha vyombo na kutunga sheria. Humo ndani vyombo/ taasis hizo hupewa uwezo na mamlaka ya kutosha sana tu yet kunakuwa na kigugumizi linapokuja suala la grand corruption.Tukiangalia mabadiliko yaliyofanywa kwenye Sheria ya PCB na kuleta PCCB (kuongeza "C" nyingine)..lengo lilikuwa pamoja na mengine kuipa Sheria na Taasisi nguvu za ziada za kuwabana wala na watoa Rushwa. Lakini matumizi ya nguvu hizi hatuyaoni. Hili lilijitokeza hata wakati wa uchunguzi wa EPA ambapo kulitolewa kauli to the effect kwamba wakishtakiwa na kufungwa hao wahusika, nchi haitatawalika!
 
Serekali, wahusika inabidi wawe wakali zaidi, jameni. Hakuna haja ya kubembeleza watu wanaoibia nchi waziwazi. Wafukuzwe kazi, mali zao zifungiwe (assets, bank accounts frozen?) maana tukiwaona bado wanapeta mjini nakuendelea kubuni njia nyingine za kuibia nchi, kweli hasira zinapanda. Matokeo yake ni apathy, civil unrest au sisi wenyewe tunaingia mkumbo nakua mafisadi wadogo. Hebu angalia Nigeria, it has huge oil reserves yet its one of the poorest countries in the world! sasa kuna civil unrest, rampant corruption,poverty, sorcery, witchcraft, fundamentalism! Yaani kila aina ya mkorogo kwasababu hiyo hiyo ya kulea rushwa na ufisadi katika high levels of government!!!!
 
Mi naona tupo kosea ni pale tu sisi wenyewe wapiganaji tunapo nyosheana vidole hapa kuna watu wamekuja na tuhuma kuwa Sitta ni fisadi na ufisadi wake huu na huu lakini kuna watu wananyosheana vidole basi mafisadi nao wanachukua advantage hapo hapo askari mnapo gombana wenyewe kwa wenyewe.
 
Na hili la kunyoosheana vidole wakati mwingine linakuja baada ya ama mnyoosha kidole anapokosana na huyo anayemtuhumu - kwa hiyo ni kupakana matope na kisasi.Kupakana matope hakutapunguza rushwa bali kutachochea kwa sababu mbili:
1. Unapompaka mtu matope unakuwa unafanya mambo kwa jazba bila kukusanya ushahidi mzuri. Matokeo yake, tuhuma hizi zinapanguliwa kiurahisi na kumwona mtuhumiwa ni victim tu wa kisasi.
2. Tuhuma zisizokuwa na ushahidi zenye kuelekezwa kwa kundi fulani la jamii hasa viongozi, zinachangia kuua nguvu vita dhidi ya rushwa.Hivyo basi ni vema wananchi tukaelewa kuwa tunajivunja nguvu wenyewe kwa chuki, wivu, visasi.Tuepuke majungu kama tunataka kuishinda rushwa.

Tuhuma zisizo na msingi, zinafurahisha kusikia/kusoma lakini hazina mashiko yoyote.
 
Rushwa imeshageuka utamaduni..njia ya maisha kwa watanzania. Pamoja na kuwa watu "wanachukia" rushwa, bado wanaiendekeza.....wanashiriki..kutoa na kupokea..kuanzia wasio na kitu hadi wenye vitu.

Mbona unajitoa? Au wewe sio Mtanzania? Pengine hujaisoma ile ripoti ya The Citizen inayoonesha kuwa kila Mtanzania ameshiriki katika ufisadi wa namna moja au nyingine kuanzia tumboni mwa mwa mama yake. Ulipataje cheti cha kuzaliwa wewe? Vyeti vya shule je? Na ile pasipoti uliipataje? Kiwanja cha nyumba nacho umekipataje? Na kazi uliyonayo je? Na ile nanii?
 
Serekali, wahusika inabidi wawe wakali zaidi, jameni. Hakuna haja ya kubembeleza watu wanaoibia nchi waziwazi. Wafukuzwe kazi, mali zao zifungiwe (assets, bank accounts frozen?) maana tukiwaona bado wanapeta mjini nakuendelea kubuni njia nyingine za kuibia nchi, kweli hasira zinapanda. Matokeo yake ni apathy, civil unrest au sisi wenyewe tunaingia mkumbo nakua mafisadi wadogo. Hebu angalia Nigeria, it has huge oil reserves yet its one of the poorest countries in the world! sasa kuna civil unrest, rampant corruption,poverty, sorcery, witchcraft, fundamentalism! Yaani kila aina ya mkorogo kwasababu hiyo hiyo ya kulea rushwa na ufisadi katika high levels of government!!!!

Haki ya Kishairi bado uko juu ya mwezi tu? Lini utashuka chini duniani? Ati? Hivi wahusika watawezaje kujifukuza kazi? Je, wanawezaje kufungia mali zao wenyewe? Tanzania yenye mafisadi bila ufisadi inawezekana?
 
Mbona unajitoa? Au wewe sio Mtanzania? Pengine hujaisoma ile ripoti ya The Citizen inayoonesha kuwa kila Mtanzania ameshiriki katika ufisadi wa namna moja au nyingine kuanzia tumboni mwa mwa mama yake. Ulipataje cheti cha kuzaliwa wewe? Vyeti vya shule je? Na ile pasipoti uliipataje? Kiwanja cha nyumba nacho umekipataje? Na kazi uliyonayo je? Na ile nanii?
Haya mambo siyo personal ndugu yangu.Ukiniuliza maswali kama haya yenye kunilenga mimi na maisha yangu binafsi... nitakupa majibu yafuatayo tena very frankly:
1.Cheti cha kuzaliwa - sikukishughulikia mimi bali wazazi wangu
2.Vyeti vya shule - kila nilipohitimu nilipata cheti changu kihalali bila kutoa KK yotote kwa maana nilifaulu kihalali..sikuhitaji kuiba cheti cha mtu au kubadili chochote kwenye cheti
3.Passport niliiipata zamanni mno kupitia wazazi wangu sijahonga mtu hata kwenye ku renew mara zote nafuata utaratibu.Sijaenda kutafuta passport bila kuwa na safari yenye uthibitisho.
4.Kiwanja - nilinunua kwa mtu wa pili na hapo ni transaction ya kibiashara hivyo rushwa ya nini? ( kununua kwa maana ya compensation for unexhausted improvements)
5.Kazi niliyonayo - sijahonga bali nilipambana thru due process
6.ile naniii - ipi?
Kutokana na hayo hapo juu ndugu utaona kuwa siyo lazima kutumia rushwa kupata huduma.Ila inatakiwa ujue wapi, nani, muda gani.INFORMATION IS POWER.
 
Rushwa sio personal? Si umesema kila kitu ni political? Sasa hujui kuwa the personal is political? Na kuwa the public is also personal?

Ina maana wewe hujafaidika na rushwa toka uzaliwe? Even indirectly? Hata kupitia skewed privileges? Are you Tanzania's outlier?
 
Tunafanya makosa tukidhania kuwa watu wale wale wale, wenye fikra zile zile, na malengo yale yale wanaweza kubadilika wasiwe watu wale wale!
Mkuu Mwanakijiji yuko right sana kwasababu kinachofanyika sasa hivi ni sawasawa Kesi ya nyani kumpelekea ngedere, unategemea nani atamuhukumu mwenzie? kama ikifikia wananchi hatuiyamini hata hiyo PCB yenyewe coz its corrupted sasa nani atamshitaki nani? na kila mmoja ana madhambi na anaogopa yake yasifichuliwe.
Huuu upuuzi wanaotuchezea kiini macho tunajua kama ni geresha. ukweli unabaki palepale kwamba watu ni walewale wenye fikra zilezile na malengo yaleyale ya kuhujumu nchi. finito.
 
6.ile naniii - ipi?

Labda leseni ya kuendesha gari:)(joke!).

Maadili ya jamii yetu kwa ujumla yameporomoka. Watu wanaomba na kupokea rushwa bila woga. Kama walivyosema wengine watanzania wengi kwa namna moja ama nyingine tunashiriki katika kufanya rushwa iendelee. Ni watu wachache ambao wapo tayari kupambana na ufisadi at an individual level.

Sina hakika tunanzia wapi kwa sababu naona suala la ufisadi ni kama vile limetengeneza 'vicious circle'.
 
Rushwa sio personal? Si umesema kila kitu ni political? Sasa hujui kuwa the personal is political? Na kuwa the public is also personal?

Ina maana wewe hujafaidika na rushwa toka uzaliwe? Even indirectly? Hata kupitia skewed privileges? Are you Tanzania's outlier?

Umeniuliza maswali nikakujibu.... huenda ulichokiuliza kisingekufanikisha kuthibitisha Hypothesis yako....
Rushwa is personal yes, and the personal is political - this is common knowledge ila mazingira ya rushwa yako dynamic and ever changing..mengine yako wazi na common, mengine yako discreet and uncommon.Rushwa nyingine ni local specific, nyingine zinategemea rent seeking tendencies, Hivyo basi unapotaka kuzungumzia rushwa iko wapi, inafanywa na nani, huwezi ku generalise kama ulivyofanya kwenye maswali uliyoniuliza kuhusu my personal life. Nafikiri ndio maana kuna rushwa ambazo ni common katika nchi zetu maskini na rushwa zinazopatikana zaidi kwenye nchi zilizoendelea.Sidhani kwenye nchi zilizoendelea ukitaka kumwandikisha mtoto shule unapaswa/au hata utaombwa rushwa? Kadhalika hapa TZ siyo kila shule utakayoenda kumwandikisha mwanao utatolewa upepo kwa maana kuna shule hata zina marketing strategies kuweza kuvutia wazazi wapeleke watoto wao kule.

Kwamba nimefaidika na rushwa ama la, hiyo ni ishu nyingine..pengine labda tuanzishe thread ya kubadilishana uzoefu wa ni vipi tumefaidika au kupata hasara through rushwa.
 
Rushwa imeshageuka utamaduni..njia ya maisha kwa watanzania.Pamoja na kuwa watu "wanachukia" rushwa, bado wanaiendekeza.....wanashiriki..kutoa na kupokea..kuanzia wasio na kitu hadi wenye vitu.

Yaani Imekithiri inatia kichefu chefu.

mwaka '96 kachero mmoja wa kituo cha polisi oysterbay alipewa taarifa kuwa mimi niko na dola mfukoni, huyu kachero bila kuchelewa akafika hapa kwangu saa kumi nambili ya asubuhi, akajitambulisha kuwa yeye ni ofisa wa jeshi la polisi na yuko hapa kunipeleka kituoni-sababu wamepata fununu kuwa hapa kwangu kunauzwa madawa ya kulevya kwani vi corrola, cressida, 505 na hata stout! vinaingia na kutoka!

Akaomba kusachi, akasachi, akanikuta na dola kama mia tatu na kitu, akadai kuwa hiyo ni evidence kwa hiyo kuna ulazima wa kwenda kituoni-nilimwaga mke wangu:D na mtoto wetu, hapo alikuwa na miaka minne:D, anyway, kufika kituoni nikapitishwa moja kwa moja nyuma, aliniacha hapo na kunieleza kuwa niko under arrest sasa na hivyo anaenda kuongea na mkuu wa investigation hiyo au faili halafu niandike statement:eek: kiroho juu! ndi ndu....! ndi ndu...! kijasho ndugu zangu najiuliza ya nini hiyo statement?

Nilivyopata hekima nilienda deski mbele kuulizia yule kachero yupo wapi! Nilifurumushwa hati mie mualifu-kwa hiyo nisubiri au niende ndani! Ooowi mwanangu! Yalinitoka haya!
baada ya kaa lisaa akaja na makaratasi-jedwali langu; na kunipeleka juu-nafikiri huku ndiko kulikuwa upelelezi-niliwaelezea ni jinsi gani nivyopata hizo hela corolla ya nani suzuki ya nani 403 ya nani basi stori-huyo mkuu wa upelelezi akaniachia, kwa mshangao wangu

Yule kachero aliyekuja kuniamsha mie na mwanangu na mke wangu, bila aibu tulivyofika nje akawageuka huyu mkuu wa upelelezi-mwenye jedwali langu na aliye fanya conspiracy hiyo! Jirani! Jirani kahonga polisi waje waniharrass-nikonde, nitoe vijisenti! Toba. Huyu kachero alidiriki kuniomba hela anunue vitunguu hapo msasani-nilikataa kata kata

sikutoa hongo, sikuvunjika kama jirani alivyofikiri, nilipiga moyo konde na kuapa hakuna mtanzania yeyote yule atakayechukua hongo toka kwangu kamwe! Haijawahi kutokea na haita tokea kamwe!

thanks to sheria zilizoruhusu kuwa na fedha za kigeni...

Sina uhakika lakini nakumbuka miaka ya mwisho ya tisini nchi za Afrika mashariki zilikubaliana na kuruhusu utumiaji wa hela za nje...hii sheria au makubaliano yaliiluruhusu mtu kukutwa na dola kadhaa mfukoni haudondokei kwa wahujumu uchumi, kwa namna moja au nyingine ilinisaidia kwa vile nilikuwa na ndondoo kuhusu hili nilitumia kipasavyo wakati wa maongezi/upelelezi pale kituoni, niliwakazia mimacho!

Niliweza kutumia uamuzi wangu wakutokuogopa na bila kuwa na mfadhaiko wa juu ya hali halisi wa rushwa. Siipendi. Hivyo basi hata marafiki zangu sasa nao hawatoi rushwa-kukiwa kuna tendo kama hili huwa mara nyingi nawapa nasaha ndugu zangu ambao wanakuwa wanaonewa kwa kutojua sheria, ulimbukeni, na hata kutokuwa na subira-subira ni muhimu.

Tuelimishane pale panapoonekana kuna mwanya, tuelimishane haki zetu sote, tuelimishane madhara-huwa sio rahisi kuonekana(individually per se) tunaweza kubadilika na kuondokan na hii jadi mpya.

Tukome Watanzania! Tukome!

Makosa ni ya Kwetu tunajifisadi kwetu kwa familia zetu kwa wanetu kwa wajukuu wetu ni aibu isiyo kifani! TUKOME
 
Labda leseni ya kuendesha gari:)(joke!).

Sina hakika tunanzia wapi kwa sababu naona suala la ufisadi ni kama vile limetengeneza 'vicious circle'.
SMU pamoja na kuwa unatania... hapa pia ni mahali pa kuzungumza na kubadilishana mawazo kuhusu ni vipi tunaweza kushinda rushwa hasa zile ndogondogo...
Hili la leseni, binafsi huwa linanichekesha na kunishangaza.Ni kweli nasikia hadithi nyingi za kuhonga upate leseni.Binafsi sikuhonga - nilienda nikafanya test pale makao makuu ya Traffic nikapata leseni yangu tena siku hiyohiyo bila kutoa hata senti moja! Ila pia niseme ukweli kuwa inabidi ufanye homework yako vizuri ujue highway code na traffic regulations vema maana utata unaanziaga hapo.Mtu hajui sheria za barabarani halafu anataka leseni.mambo ya short cut hayo- yanaleta opportunity for rushwa.
 
Umeniuliza maswali nikakujibu.... huenda ulichokiuliza kisingekufanikisha kuthibitisha Hypothesis yako....
Rushwa is personal yes, and the personal is political - this is common knowledge ila mazingira ya rushwa yako dynamic and ever changing..mengine yako wazi na common, mengine yako discreet and uncommon.Rushwa nyingine ni local specific, nyingine zinategemea rent seeking tendencies, Hivyo basi unapotaka kuzungumzia rushwa iko wapi, inafanywa na nani, huwezi ku generalise kama ulivyofanya kwenye maswali uliyoniuliza kuhusu my personal life. Nafikiri ndio maana kuna rushwa ambazo ni common katika nchi zetu maskini na rushwa zinazopatikana zaidi kwenye nchi zilizoendelea.Sidhani kwenye nchi zilizoendelea ukitaka kumwandikisha mtoto shule unapaswa/au hata utaombwa rushwa? Kadhalika hapa TZ siyo kila shule utakayoenda kumwandikisha mwanao utatolewa upepo kwa maana kuna shule hata zina marketing strategies kuweza kuvutia wazazi wapeleke watoto wao kule.

Kwamba nimefaidika na rushwa ama la, hiyo ni ishu nyingine..pengine labda tuanzishe thread ya kubadilishana uzoefu wa ni vipi tumefaidika au kupata hasara through rushwa.

Acha kuzunguka. Hoja iko wazi. Sijawahi kukutana na Mtanzania ambaye hajawahi kunufaika kwa namna moja au nyingine na rushwa/ufisadi. Hata wapambanaji wakuu wanaoheshimika Tanzania ambao nimebahatika kuwafahamu nao pia wamewahi kunufaika japo kwa shingo upande.

Ndio maana nasisitiza kuwa wakati umefika sasa tuliangalie hili suala kama suala binafsi pia. Utamaduni wa kifisadi unaanza kujengwa nafsini toka Mtanzania anapozaliwa. Ile ripoti ya The Citizen imeonesha hatua kwa hatua ni mara ngapi kila Mtanzania analazimika kutoa rushwa maishani. Ni kweli upatikanaji wa taarifa unasaidia ila unaweza ukawa na taarifa na bado ukajikuta unatoa au unatolewa rushwa kwa shingo upande.

Swali langu bado linasimama: Je, haujawahi kunufaika na rushwa/ufisadi?

"An ordinary Tanzanian is likely to part with a staggering Sh1 million as the minimum cost of bribes in his or her entire lifetime" (The Citizen, 5 April 2008) - The Citizen's 'National Bribe Index'.
 
Back
Top Bottom