Mapadre/mashehe/wachungaji: Mmemsikia Lusekelo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapadre/mashehe/wachungaji: Mmemsikia Lusekelo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHUAKACHARA, Feb 9, 2012.

 1. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,825
  Trophy Points: 280
  Antony Lusekelo (Mzee wa upako) anawauliza hivi:
  1. Mchakato wa Katiba mpya mlionekana kurasa za mbele za magazeti na kofia (viongozi wa dini kubwa kubwa-kwa maneno yake) , sasa watu wnakufa mbona hamkemei wanaoua watu kwa kudai posho na mishahara- Maandiko yanasema madaktari wana ruhusa ya kuua?
  2. Kuna tofauti gani kati ya wauaji wa albino wanaoua li kupata fedha na madaktari wanaoua ili nao kupata fedha?
  3. Kuna tofauti gani kati ya jambazi anayeua kupata fedha na madaktari wanaoua kupata fedha?
  Source: channel Ten 8/02/2012 at 9.30 PM

  Maaskofu/ Mashehe mjibuni.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mzee wa upako amepaka!
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mzee wa upako anatafuta nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na JK
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Aongee yeye kutimiza wajibu wake, na sio kuangalia nani hajaongea!
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Watu hufa kwa siku zao kutimia, kushindwa kupata huduma sahihi au kukataliwa huduma sahihi.
  Asilimia kubwa walikuwa wanakufa kimya kimya kwa kukosa huduma sahihi yani serikali kushindwa kuweka kipaumbele kwenye kuboresha huduma katika mahospitali yake.
  Hawaweki vifaa, wakiweka hawavitunzi. haweki wataalam wakiweka hawawatunzi.
  Hawanunui dawa, wakinunua wanachakachua wenyewe..
  Mnaosema warudi kazini, huwa mnatibiwa huko?
   
 6. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mwehu huyo!
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  kama yeye mchungaji wa mungu kweli...asikusanye sadaka za watu halafu aendelee kuhubiri
   
 8. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huu ndo unafiki!!! Kajadili hili swala mwishoni... Angeuliza amekuaje hadi madaktari wakagoma.... Madaktari hawakuanza kugoma out of Nowhere, walianzia wizarani na wizara ikavurunda katika kutoa maamuzi, then akaja waziri mkuu nae akaharibu... Alitaka madaktari wafanyaje ili wapate stahili zao???? ni upungufu wa akili kufananisha mgomo wa Madaktari na kuuawa kwa Ma albino au ujambazi....
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti gani mwanasiasa anayeuwa wananchi kwa njaa huku yeye akiambulia vinono katika jina la posho?
   
 10. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Mimi siyo Askofu/Shehe/Mchungaji. Lakini napenda kumjibu huyu Anthony Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako.

  Kwanza kabisa nianze na nanukuu ya Biblia Takatifu inayosema hivi; ''HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU'' Matayo 5:9

  Sasa basi Anthony Lusekelo akiwa Mchungaji wa kondoo wa Bwana napenda kumwuliza yeye anasimamia wapi katika ANDIKO HILI?Mpaka sasa amechukua hatua gani katika KUPATANISHA kati ya Madaktari na Serikali kwa upande mwingine ili aweze kustahili KUITWA MWANA WA MUNGU?

  Inasikitisha kuona kwamba Mzee wa upako badala ya KUWA MPATANISHI amekaa pembeni na kuanza KULAUMU UPANDE MMOJA WA MGOGORO, yaani upande wa Madaktari! Hakika huo siyo upatanishi ambao Biblia takatifu inaozungumzia. Kwa hili Mzee wa Upako amepotoka na anapashwa kuwaomba msamaha Madaktari na Watanzania kwa kuwadhalilisha na kuwatukana Madaktari wetu.

  Mimi napenda kusema Mungu na amsamehe kwa uropokaji wake maana inaonekana HAJUI ALITENDALO. Katika hili Lusekelo amejidhihirisha kuwa ni kiongozi wa kidini aliye mnafiki wa hali ya juu. Inasikitisha kuwa Anthony Lusekelo amewalaumu Maaskofu na Masheikh ambao nao ni wahudumu wa Kiroho kama alivyo yeye. Kama angetumia hekima ya Biblia ambayo najua hana angeliwaita hao Maaskofu na Masheikh akakaa nao na kuzungumzia huu mgomo badala ya kuanza kulaumu.

  Pengine tumwulize Mzee wa Upako. Hivi kule kanisani kwake hakuna Daktari yeyote anayesali huko? Kama yupo au wapo amewahi kukaa na kuongea nao ili kujua kiini cha mgomo wao???

  Nimalize kwa kusema kwamba Anthony Lusekelo hafai kuwa Mchungaji,Askofu wala padre maana amejaa unafiki na ubinafsi wa hali ya juu. Ni aibu kwa kiongozi wa kidini kukosa ushirikiano na viongozi wa Serikali na hasa Viongozi wenzake wa kiroho. Katika hili Anthony Lusekelo NAYE AMECHANGIA KATIKA MAUAJI YA WATANZANIA WALIOKUFA KWA KUKOSA HUDUMA YA MADAKTARI. Kulingana na Biblia DAMU YA WATU HAO WALIOKUFA BASI ANTHONY LUSEKELO ATADAIWA MBELE YA MUNGU KWA KUSHINDWA KUWA MPATANISHI!
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo anataka madaktari waendelee kufanya kazi katika mazingira duni na malipo madogo ili wafe wao?
   
 12. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Call a spade spade....Hongera mchungaji sijawahi kukufagilia hata siku moja lakini kwa hili umepasua jipu. Huu ndio ukweli ambao wenye mawazo mepesi hawauoni.... Unawalaumu wabunge kwa kujiongezea posho wakati unawaunga mkono madaktari kwa kudai mil 17.
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama yeye hataki pesa,mbona huwa anaweka namba za m-pesa na tigo pesa kweye tv
   
 14. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Usihukumu Usije ukahukumiwa.
   
 15. N

  Nyumisi JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Aache kutukana madaktari huyo. Mbona yeye anakufuru kwa kujiita mzee wa upako. Ni wapi katika biblia hilo daraja la uzee wa upako limetolewa. Yeye hajui kwamba kupotosha watu katika neno la Mungu unawaua kiroho. Afadhali mtu akuue kimwili kuliko kukuua kiroho. Zile pete kubwakubwa ambazo amekuwa anavaa zinaashiria nini.
   
 16. k

  kiche JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa ana tuhuma kuwa ni member wa freemanson asiwaumize kichwa,yupo kisanii tu.
   
 17. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kekundu kekundu.
   
 18. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaliyomkuta Askofu Kakobe na yeye yatamkuta,
   
 19. collycool

  collycool Senior Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  jabulani
  "Aongee yeye kutimiza wajibu wake, na sio kuangalia nani hajaongea!"

  Nakuunga mkono mkuu yeye aongee kwa nafasi yake na sio aangalie nani kasema nini, halafu hivi ikitokea waumini wake hawatoi sadaka tena ataweza kuliendesha hilo kanisa lake tena.
   
 20. g

  greenstar JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tulipinga posho za wabunge pia tupinge ongezeko la mishahara ya madaktari kwa nguvu zaidi......wapewe ukweli ili watambue nchi yetu ipo kwenye mpito wa maisha magumu.Serikali ishughulikie kushusha mfuko wa bei ili kila mtanzania anufaike na nchi bila ubaguzi wowote !!!!
   
Loading...