Antony Lusekelo (Mzee wa upako) anawauliza hivi:
1. Mchakato wa Katiba mpya mlionekana kurasa za mbele za magazeti na kofia (viongozi wa dini kubwa kubwa-kwa maneno yake) , sasa watu wnakufa mbona hamkemei wanaoua watu kwa kudai posho na mishahara- Maandiko yanasema madaktari wana ruhusa ya kuua?
2. Kuna tofauti gani kati ya wauaji wa albino wanaoua li kupata fedha na madaktari wanaoua ili nao kupata fedha?
3. Kuna tofauti gani kati ya jambazi anayeua kupata fedha na madaktari wanaoua kupata fedha?
Source: channel Ten 8/02/2012 at 9.30 PM
Maaskofu/ Mashehe mjibuni.
Mimi siyo Askofu/Shehe/Mchungaji. Lakini napenda kumjibu huyu Anthony Lusekelo a.k.a Mzee wa Upako.
Kwanza kabisa nianze na nanukuu ya Biblia Takatifu inayosema hivi;
''HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU'' Matayo 5:9
Sasa basi Anthony Lusekelo akiwa Mchungaji wa kondoo wa Bwana napenda kumwuliza yeye anasimamia wapi katika ANDIKO HILI?Mpaka sasa amechukua hatua gani katika KUPATANISHA kati ya Madaktari na Serikali kwa upande mwingine ili aweze kustahili KUITWA MWANA WA MUNGU?
Inasikitisha kuona kwamba Mzee wa upako badala ya KUWA MPATANISHI amekaa pembeni na kuanza KULAUMU UPANDE MMOJA WA MGOGORO, yaani upande wa Madaktari! Hakika huo siyo upatanishi ambao Biblia takatifu inaozungumzia. Kwa hili Mzee wa Upako amepotoka na anapashwa kuwaomba msamaha Madaktari na Watanzania kwa kuwadhalilisha na kuwatukana Madaktari wetu.
Mimi napenda kusema Mungu na amsamehe kwa uropokaji wake maana inaonekana HAJUI ALITENDALO. Katika hili Lusekelo amejidhihirisha kuwa ni kiongozi wa kidini aliye mnafiki wa hali ya juu. Inasikitisha kuwa Anthony Lusekelo amewalaumu Maaskofu na Masheikh ambao nao ni wahudumu wa Kiroho kama alivyo yeye. Kama angetumia hekima ya Biblia ambayo najua hana angeliwaita hao Maaskofu na Masheikh akakaa nao na kuzungumzia huu mgomo badala ya kuanza kulaumu.
Pengine tumwulize Mzee wa Upako. Hivi kule kanisani kwake hakuna Daktari yeyote anayesali huko? Kama yupo au wapo amewahi kukaa na kuongea nao ili kujua kiini cha mgomo wao???
Nimalize kwa kusema kwamba Anthony Lusekelo hafai kuwa Mchungaji,Askofu wala padre maana amejaa unafiki na ubinafsi wa hali ya juu. Ni aibu kwa kiongozi wa kidini kukosa ushirikiano na viongozi wa Serikali na hasa Viongozi wenzake wa kiroho. Katika hili Anthony Lusekelo NAYE AMECHANGIA KATIKA MAUAJI YA WATANZANIA WALIOKUFA KWA KUKOSA HUDUMA YA MADAKTARI. Kulingana na Biblia DAMU YA WATU HAO WALIOKUFA BASI ANTHONY LUSEKELO ATADAIWA MBELE YA MUNGU KWA KUSHINDWA KUWA MPATANISHI!