..kilichotokea Misri ni tofauti na utabiri wa JK pamoja na conclusions zako.
..Misri kulifanyika mapinduzi ya kiraia ambayo yalifuatiwa na uchaguzi uliokiweka chama cha Muslim Brotherhood madarakani.
..baada ya Muslim Brotherhood kushika dola palitakiwa kufanyika mabadiliko ya katiba. sasa tatizo Muslim Brotherhood wakatumia wingi wao na mabavu kukandamiza hoja za vyama vingine ktk mabadiliko ya katiba.
..kwa kifupi Muslim Brotherhood na Raisi wao Mohamed Morsi walikuwa wanatumia hoja hizihizi wanazojenga CCM leo ktk mchakato wa katiba. Kwamba wao wako wengi hivyo maoni yao tu ndiyo yasikilizwe.
..Sasa Muslim Brotherhood wakafanikiwa kupitisha katiba waliyoitaka wao, lakini kukawepo idadi ya kutosha ya Wamisri ambao hawakukubaliana na katiba iliyopitishwa.
..Wananchi wengi waliingia mitaani na kuanza kupinga ukandamizaji uliokuwa ukifanywa na Muslim Brotherhood. Hali ya usalama Misri ilianza kuwa mbaya. Jeshi likaona kwamba nchi inaelekea kutokutawalika, na likatoa amri kwamba wanasiasa wamalize matatizo yao, na ikiwa watashindwa jeshi litalazimika kuchukua "hatua stahiki."
..Mlolongo niliouleze hapo juu ndiyo uliomuingiza madarakani Field Marshal Al-Sisi.
..Kiburi na vitimbi vya chama tawala cha Misri ktk mchakato wa katiba ndiyo sababu ya msingi ya kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
cc
ZeMarcopolo,
Kishimbe wa Kishimbe,
ANDREW SMITH,
Kobello,
Nguruvi3