Maoni yangu ya man city vs Chelsea

innocent dependent

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Messages
2,013
Points
2,000

innocent dependent

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2019
2,013 2,000
Leo kutawakutanisha team ya man city vs Chelsea na inategemewa itakuwa game nzuri. tuanze kuona strength na weakness za Kila timu.

Strength ya Chelsea
Bahati nzuri kwa Chelsea leo trio midfilder wao wakali yaani kante,jorginho na kovacic wote wapo fit na inategemewa wote wataanza kwa pamoja.Mara nyingi linapofika game kubwa mmoja Kati yao anakuwa injury either ni kante or kovacic.Eneo hili ndio nguvu ya Chelsea wote wa3 wanajua kukaba na kucontrol na kusoma mchezo na kutengeneza nafasi.kama mnakumbuka vizuri game ya Chelsea vs Liverpool super cup kante,jorginho na kovacic wote kwa pamoja walianza ndo match pekee waliocheza kwa pamoja na hiyo game Chelsea walidominate game kwa kiasi kikubwa na waliwazuia Liverpool counter attack zao na game iliisha 1-1 ndani ya dk 90 kutokana na strong midfilders ya Hawa wa3.

Lakini pia wapo vizuri Sana upande wa mbele wanna winga wazuri Sana pulic na willian pamoja na central forward kijana Abraham.upande wa willian anakuoffer vitu viwili with ball and without ball huku pulisic ni mzuri kwenye pace na Kasi pamoja na ability of scoring.

Weakness ya chelsea
Upande wa beki ya Kati kufanya makosa ya kitoto sometime yanaigharimu team ingawa nimeona sasa hiv kidogo Kuna improvement tofauti na mwanzo.

Strength ya man city
Kwenye midfilders na wingers wana kiungo mmoja mbunifu de bruyne hatari lakini kukosekana kwa bernado Silva kumepunguza ladha lakini still wanna winga wazuri Sterling na mwenzake mahrez kwa kiasi fulani wanaweza kuwapa chafya mabeki wa Chelsea pamoja na mnyama aguero.

Weakness ya man city
Beki ya man city inakatika Sana na wanaruhusu magoal for funny.Hili ndio tatizo litakalo waangusha kwenye mechi ya leo tokea Laporte awe injury beki ya man city imekuwa ya ovyo Sana wamekuwa wabovu Sana kwenye Hili eneo kuliko Chelsea.

Nani atashinda?
Kwa mtazamo wangu mkeka wangu nampa Chelsea atamfunga man city

Kwasababu zifuatazo
1.city sasa hiv wanabeki mbovu Sana kitu ambacho angalau kinapunguza kutokufungwa magoal mengi ni mfumo wao wakupossess kwa muda mwingi bahati mbaya wanakutana na midfilders nayo ni wazuri kwenye kupossess ya jorginho ambaye ana average ya 93% ya pass accurate na kovacic ana average ya 90% ya pass accurate huku kante akifanya free run.kutokana na Chelsea kuwa wazuri kwenye kufunga na aina ya mabeki ya man city italeta madhara Sana kwa man city

2. Kukosekana bernado Silva
Huyu ndio mchezaji Bora wa man city na kiungo anaye anaunganisha team mzuri kwenye kucreate chance na kufunga pia.kukosekana kwake ni pengo kubwa Sana kwa man city.

3.form nzuri ya Chelsea away
Hi ni moja ya sababu inayofanya niwape Chelsea point 3 wamekuwa wakipata ushindi mfululizo away na wakicheza vizuri kuliko uwanja wa kwao.

TUKUTANE GAME IKIISHA.
 

Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Messages
8,354
Points
2,000

Consultant

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2008
8,354 2,000
Most likely Chelsea watapigwa maana kwenye hizi games against “top 6”, wamekuwa wakisuasua mno. As much as defence ya City ipo depleted kwa sababu ya majeruhi, defence ya Chelsea nayo mashaka matupu.

It is a make-or-break game kwa City maana wakipigwa leo na Liverpool akashinda, points 12 gaps hawatoliziba.
 

Forum statistics

Threads 1,382,054
Members 526,258
Posts 33,818,472
Top