Maoni ya Wadau baada ya Hotuba ya Rais Kikwete kwa 'Wazee wa Dar' kuhusu Sakata la Tegeta Escrow

Well,there is no point!Kama kina Mramba, Yona na wengine walitimuliwa na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kulitia taifa hasara na matumizi mabaya ya madaraka,nini kinachozuia kutowafungulia mashitaka hawa waliotajwa?

Is there really a point ya kufanya uchunguzi juu ya uchunguzi?Hii yote inaniaminisha kuwa we have been trying to solve this whole issue from a completely wrong perspective. Cha kufanya we should've found out the source ya hii IPTL.Knowing that can possibly answer a lot of questions kama tuendelee au vipi.Barua ya kujiuzulu AG ipo kimipasho pasho tu; as a President, nimedharau maamuzi laini yake na kwa kuwatukana wananchi waliyoiweka serikali yake kwenye madaraka. CAG na PCCB ni taasisi zilizo chini ya aliyewateua na zinalindwa na katiba,yes? Sasa iweje these institutions leo hii zisiaminiwe? What is the point of having them in the first place? Kama wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, na maamuzi waliyofanya ni mtazamo wa wananchi, kuna haja ya kuwaweka pale bungeni kama hata chochote wanachosema hakitekelezwi? Our rights and wealth vyote tumeibiwa.

I want to believe that kura yako tu ndio silaha unayoweza kuitumia kuondoa all these injustices but again sina uhakika sana na hili. It is very possible hata hiyo silaha ikapokonywa na wananchi wakakubali tu kwa sababu tunaibiwa kila siku,viongozi wetu wanatutukana tena hadharani na sisi tunapiga makofi kushangilia, hakuna chochote tunafanya. Ni jambo la aibu mpaka sasa 50+ years after 'independence' bado hatujui hata vision ya nchi yetu. What do we really stand for? Kweli aliyetuloga needs to set us free.
 
huu mtandao ni mpana ndo maana anauogopa Rugemalira ni nani mpaka aisumbue serikali huu mtandao ambao ni ngumu kuuvunja ghafla ndo maana anakwepa.
 
Kwa jinsi swala hili la Escrow lilivyokuwa kubwa na kwa namna raisi Kikwete alivyolimaliza jioni ya leo,bado una hamu na moyo wa kuendelea kufuatilia hatima nzima ya "saga" hili kwa watuhumiwa waliobaki?

Je,si kweli kuwa swala hili lilipaswa kuchunguzwa na chombo huru kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na taasisi za hapa nchini?

Je,maamuzi haya yatasai kurudisha imani ya wanachi kwa Kikwete na CCM kwa ujumla?

Je,nchi wafadhili wataridhika na maamuzi haya?

Je,likitokea saga lingine(mungu aepushie mbali),utakuwa na hamu ya kulifuatilia kama ulivyofanya kwa saga hili la Escrow?

Je,bado una hamu ya kufuatilia siasa za nchi hii?

Nawasilisha.

1. Kuhusu uchunguzi kutoka chombo huru nje ya nchi je chombo hicho kitaletwa na nani? kwani kwenye Bomu la Soweto na Mauaji ya Padri kule Zanzibar tuliaminishwa kuwa walikuja wapelelezi wa Kimataifa yaani FBI na wengine kutoka China je umeishawahi kupata matokeo yeyote ya uchunguzi kutoka kwa wachunguzi hao? achana na lile la FBI kuchora katuni kule Zanzibar.

2. Maamuzi haya hayataweza kurudisha imani ya wananchi kwa CCM kwani wengi wao hata bila hii ESCROW wameishaichoka CCM kwani matukio ni mengi ambayo hayajatatuliwa hadi sasa EPA, RICHMOND, MEREMETA,KAGODA

3. Kwa upande wa nchi wafadhiri kuridhika na utekelezaji huu sidhani kama wataridhika kwa hiyo tutarajie kutokuwa na mabadiriko yeyote ya vikwazo vya misaada tulivyowekewa.

4. Kuhusu kuendelea kufuatilia any saga litakalotokea ni vema tukaendelea kwani kwa kuacha kulifuatilia tutakuwa tumetoa mwanya kwa haya maCCM kuendelea kutafuna mali zetu

5. Siasa ndio maisha ya kila siku hivyo basi hauwezi kusema utaacha kufuatilia siasa za nchi yako eti kwa sababu tu ya matokeo ya hotuba hii ya JK, kwani kwa udhaifu wa hotuba hii ni vema tukaendelea kujadili siasa ikiwa pamoja na hotuba hii ili wananchi wenye upeo mdogo wa kulewa waelewe ni wapi wamepigwa changa la macho.
 
Baada ya kusikiliza hotuba ya POROJO tunaomba mwongozo maana huyu RAIS wetu anawabeba wezi

Nchi inapoelekea sio kuzuri

Rais anakaa meza moja na mafisadi kujadili jinsi ya kufanya maamuzi

Tuseme Ukweli RAIS WETU ana mapungufu makubwa yaani kila kitu TUME, UCHUNGUZI

MOD tueshimiane this is independent thread Naomba usiunganisha na thread nyingine
 
Mwizi ni mwizi tu. Hata yeye kachota alafu anaenda kumtoa kafara kale ka maza!!! Hii nchi kweli inaviongozi wanaojua kula.
 
Baada ya kusikiliza hotuba ya POROJO tunaomba mwongozo maana huyu RAIS wetu anawabeba wezi

Nchi inapoelekea sio kuzuri

Rais anakaa meza moja na mafisadi kujadili jinsi ya kufanya maamuzi

Tuseme Ukweli RAIS WETU ana mapungufu makubwa yaani kila kitu TUME, UCHUNGUZI

MOD tueshimiane this is independent thread Naomba usiunganisha na thread nyingine
Tungane kwenye ku delete ccm Tanzania
 
Mie pamoja na kuwa sijaridhishwa na DHAIFU lakini sitaacha kufuatilia kwani bado kuna maswali mengi yasiyo na majibu kama vile hatima ya hawa wezi wote wakiwemo Wabunge na wale ndani ya Ikulu, kama watafilisiwa ili kurudisha pesa za walipa kodi na pia kupandishwa kizimbani ili kujibu mashtaka ya kupokea pesa za wizi au kuhusika kwa kuruhusu pesa kuchukuliwa BoT kwa kutumia forged documents. Na je, Wafadhili wataamua kuendelea na mgomo wao wa kutotoa $1 billioni katika mwaka huu wa fedha 2014/2015. Hivyo ni muhimu kuendelea kufuatilia sakata hili mpaka kieleweke.
 
Je hotuba ya leo ya JK unaionaje ukihusisha na kiu ya wananchi waliokuwa wakiisubiri kwa hamu? Tiririka tu!

Rais ameniacha njia panda pale aliposema Tanzania si nchi ya Ujamaa Hama kweli niwatake radhi wanafunzi wangu ambao niliwafundisha kuwa katiba yetu inatamka kuwa Tanzania ni nchi ya Demokrasia; Vyama Vingi na Ujamaa 1977 kumbe niliwapotosha na copy niliyotumia inawezekana imekosewa. Samahani saana wanafunzi wangu il à Rais kawapa majibu nadhani ni sahii.
 
Je hotuba ya leo ya JK unaionaje ukihusisha na kiu ya wananchi waliokuwa wakiisubiri kwa hamu? Tiririka tu!
Nisawasawa ukienda na choklet gerezani ukawapa wale mahabusu alafu ukawauliza ni tamu unategemea jibu gani? Delete futa kabisa ccm
 
Kwa kweli hawa watu wanakera, wanabebana hivi hivi na ni dhairi huyu jamaa kachota mzigo pia. Hawa watu hawafai kwa kweli.
 
.mimi na amini mijizi haiwezi kuwajibishana kama wasikia mfanyakazi wa ikulu kachukua pesa ya wizi tutegeme nini kwa jk?
 
Well,there is no point!Kama kina Mramba, Yona na wengine walitimuliwa na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kulitia taifa hasara na matumizi mabaya ya madaraka,nini kinachozuia kutowafungulia mashitaka hawa waliotajwa?

Is there really a point ya kufanya uchunguzi juu ya uchunguzi?Hii yote inaniaminisha kuwa we have been trying to solve this whole issue from a completely wrong perspective. Cha kufanya we should've found out the source ya hii IPTL.Knowing that can possibly answer a lot of questions kama tuendelee au vipi.Barua ya kujiuzulu AG ipo kimipasho pasho tu; as a President, nimedharau maamuzi laini yake na kwa kuwatukana wananchi waliyoiweka serikali yake kwenye madaraka. CAG na PCCB ni taasisi zilizo chini ya aliyewateua na zinalindwa na katiba,yes? Sasa iweje these institutions leo hii zisiaminiwe? What is the point of having them in the first place? Kama wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, na maamuzi waliyofanya ni mtazamo wa wananchi, kuna haja ya kuwaweka pale bungeni kama hata chochote wanachosema hakitekelezwi? Our rights and wealth vyote tumeibiwa.

I want to believe that kura yako tu ndio silaha unayoweza kuitumia kuondoa all these injustices but again sina uhakika sana na hili. It is very possible hata hiyo silaha ikapokonywa na wananchi wakakubali tu kwa sababu tunaibiwa kila siku,viongozi wetu wanatutukana tena hadharani na sisi tunapiga makofi kushangilia, hakuna chochote tunafanya. Ni jambo la aibu mpaka sasa 50+ years after 'independence' bado hatujui hata vision ya nchi yetu. What do we really stand for? Kweli aliyetuloga needs to set us free.

Ngugu, umeongea ukweli mtupu na kwa uchungu na ni kweki inauma sana.
 
Back
Top Bottom