Maoni ya Wadau baada ya Hotuba ya Rais Kikwete kwa 'Wazee wa Dar' kuhusu Sakata la Tegeta Escrow

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,158
144,684
Kwa jinsi swala hili la Escrow lilivyokuwa kubwa na kwa namna raisi Kikwete alivyolimaliza jioni ya leo,bado una hamu na moyo wa kuendelea kufuatilia hatima nzima ya "saga" hili kwa watuhumiwa waliobaki?

Je,si kweli kuwa swala hili lilipaswa kuchunguzwa na chombo huru kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na taasisi za hapa nchini?

Je,maamuzi haya yatasai kurudisha imani ya wanachi kwa Kikwete na CCM kwa ujumla?

Je,nchi wafadhili wataridhika na maamuzi haya?

Je,likitokea saga lingine(mungu aepushie mbali),utakuwa na hamu ya kulifuatilia kama ulivyofanya kwa saga hili la Escrow?

Je,bado una hamu ya kufuatilia siasa za nchi hii?

Nawasilisha.

Je hotuba ya leo ya JK unaionaje ukihusisha na kiu ya wananchi waliokuwa wakiisubiri kwa hamu? Tiririka tu!

Jk au familia yake imehusika moja kwa moja na uchotaji wa fedha hizi....amepata kigugumizi kikubwa kwenye hotuba yake na kushindwa kuwajibisha watu waliotajwa kuanzia ikulu....hamna la maana alilofanya...mambo ni yale yale

Katika Hotuba ya JK kwa Taifa kuhusu Escrow, kupitia wazee wa Dar es Salaam, Mh, JK ameonesha busara iliyojaa hofu na mashaka, katika muktadha ufuatao:-
1. Kukiri kwamba serikali yake haiwezi kutaifisha moja kwa moja mitambo ya IPTL, ili hali deal zima limetawaliwa na harufu ya Ufisadi. Eti wawekezaji watakimbia, ni hofu na shaka dhidi ya dhamira ya kweli ya kupambana na rushwa kubwa.
2. Kukiri kwamba serikali yake haiwezi kuweka wazi mikataba ya madini na nishati kwa hofu ya kuwakera wawekezaji. Eti itafutwe njia nyingine nzuri (hapa analenga kuwafurahisha akina Escrow), na kuficha 10% za viongozi wa juu.
3. Kuanza kuhesabu idadi ya wabunge wa chama chake kwenye kamati ya PAC dhidi ya wale wa Upinzani badala ya kujikita kwenye content za mapendekezo ni dalili ya Hofu na shaka ya kuanguka kwa chama na serikali yake.
4. Kushindwa kumuwajibisha Mtumishi aliyemteua (Katibu Mkuu, Maswi) mwenyewe na kusingizia upelelezi na Tume ya Maadili ni hofu na shaka ya usaliti kwa Network yake, na udhaifu wa ki mamlaka ya Kiongozi.
5. Kukiri kwamba Fedha ya Escrow si fedha ya Umma, na kwamba ilitoka kihalali, na wakati huo huo unadai uchunguzi unaendelea, ni busara iliyojaa hofu na shaka ya kukiri udhaifu katika serikali yake. Pia ni kuwavuruga wananchi.
6. Kukiri kwamba hawezi kuanzisha mchakato wa kiuchunguzi wa majaji waliotuhumiwa katika Escrow na kudai eti ni suala la kimahakama, ni hofu na shaka ya kimaadili ya Kiongozi wa nchi.
KWA KIFUPI KIONGOZI WETU MKUU ANAJUA UDHAIFU ULIOPO NA ANAONA SI BUSARA KUUKUBALI MOJA KWA MOJA UDHAIFU HUO, ESCROW NI UFISADI WA AKILI NYINGI!
NAWASIRISHA KWA MJADALA ZAIDI.

Ni wazi kwa waliofuatilia hotuba ya rais ameendelea kuibua maswali lukuki kutokana na kuacha masuala mengi yakielea.kutokana na kuendelea kuchelewa kuchukua maamuzi suala hili litakigharimu chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu mwakani.

Ni wazi kwa waliofuatilia hotuba ya rais ameendelea kuibua maswali lukuki kutokana na kuacha masuala mengi yakielea.kutokana na kuendelea kuchelewa kuchukua maamuzi suala hili litakigharimu chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu mwakani.
No tutakua tumeshasahau....2015 mbali ivo..

Leo kamshangaza mama prof Tibaijuka.

Nimemuona Mwasi akiachwa mdomo wazi.

Imemfanya prof jk awe anapiga miayo sana.

Kwa mara ya kwanza nimemuona mkuu akiwa na glass mbili tofauti za maji.

Kanishangaza alivyopotezea kuhusu umiliki wa PAP.

Na mwisho nimegundua kuwa rais ni mtaalamu wa kiwango cha juu katika masuala ya hali ya hewa, hasa katika kupima upepo. Vyuo vikuu mbalimbali viangalie uwezekano wa kumpa uprof wa heshima katika taaluma hii ya kupima upepo.

bado hatujaridhika na tushamchoka na maamuzi ya taratibu nawapongeza vijana walotuwakilisha vizuri ukumbini.kwa kuonyesha wazi kuwa Maswi Muhongo Tibaijuka hawapendwi na Wananchi.

Back
Top Bottom